Wazazi wa kisasa msijisahau kwenye Malezi, hawa kina junior wamekuwa mizigo hawawezi hata kujioshea vyombo ni mizigo, ni kero kubwa wakiwa ugenini

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,451
Sijui ni nani aliwadanganya baadhi ya wazazi, hasa wale waliotoka kwenye familia duni, kwamba mara tu wakipata vijisenti basi watoto wao hawapaswi tena kufanya majukumu ya kujitegemea wala ya nyumbani.

  • Watoto wakila waache vyombo kwenye sinki house girl ataosha
  • watoto wakitoka shule watupe nguo kwenye tenga hg atafuta
  • watoto wakiamka wajianda tu kwenda shuleni hg atafagia uwanja
  • watoto wakichezea vitu wasivirudishe walipovikuta
  • mazingira ya nyumbani yakiwa machafu hayawahusu wanasubiri mkata majani
  • watoto wakunjiwe nguo
  • n.k.

Kuna baadhi ya ndugu zetu wnalea watoto hivi, watoto wakija kututembelea weekend majumbani hadi tunahisi wana matatizo ya kiafya kumbe ni malezi. Na sisi ni waelewa itakuwaje sasa wakiwa huko ugenini ?
 
Mtoto anatakiwa ajifunze mambo akiwa mdogo, miaka mitatu tu inatosha kuanza kujifunza kupiga mswaki,mi4 anaanza kuoga mara mojamoja na kuendelea, ndio kazi ndogo ndogo zote awe anazoeshwa ili asiwe mzigo baadaye..
 

Kwa sister daslamu
 
Hmm kwanini?
Sasa mkuu una mabiashara makubwa, mabilioni ya pesa, una uwezo wa kumpeleka mtoto IST, HOPAC, Aga Khan na bado akimaliza high school unamsomesha nje full price bila ufadhili...

Mtoto wako hawezi kuja kuishi maisha ya kawaida.

Kwahiyo mtoto wa namna hiyo hafundishwi survival anafundishwa delegation ili aje kuwa mratibu mzuri sana.
 
Nani kakwambia kwamba watoto wote wa matajiri hawafanyi kazi za nyumbani ?

Kuna wazazi wana pesa nyingi kuzidi bajeti za wizara lakini kwenye malezi hawataki mchezo,

Uje kwetu sasa huku mtu ana kajiuwezo hata ka kununua IST basi naona mtoto kufanya hizo kazi ni kumtesa 😂
 
Tu Junior Jau sana wazazi wao hawajui tu tunavyoteseka navyo vikija kutusalimia,nje ya mada Kuna hako kamoja kalikuja December nikaenda Nako mjini,kufika huko kakang'ania kwenye gari hakashuki nikashusha vioo nikakaacha!
Narudi sikakuti kwenye gari aisee nilikatafuta mpaka jasho la meno likanitoka,kumbe kamejificha kwenye buti ghafra kanaibuka kanacheka Cheka eti odo odo🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Sawa ila sikubaliani nao! Ushawahi kuwa karibu na aina hii ya hawa watoto? Utawahurumia, ila kwa sababu pesa mbele hapo sina neno mkuu!
 
Ningekawasha banzzz😂
 
Matajiri wa jf wakijadiliana malezi ya akina junia😂😂,haya tulioeteleza watoto kitaa tukutane kwenye Uzi wa kula tunda kimasihara
 
Hamna kitu kama hicho, labda kama una watumwa kama karne za nyuma.Self reliance ni basic kwa kila mwanadamu, kinyume cha hapo ni utahira.Mtoto/mtu lazima ajifunze kujifulia, chupi zake huko na nguo sensitive, ajue kujitegemea, kutandika kitanda, kufanya arrangement basic kwenye chumba chake etc.Na kwa taarifa yako watu waliofanikiwa pia wako smart kwenye hivyo vitu, huwezi kuwa na akili ya kutengeneza mamilioni huku huwezi hata kujifanyia basic arrangement.
Wewe kama mzazi ukiona umelea mitoto hivyo, ujue hiyo ni ishara moja wapo but wataharibu hata biashara n.k
 
Ni kweli usemalo Mkuu kikubwa wazazi na walezi tupunguze huruma kwa watoto na roho mbaya kwa wanaotulelea watoto kwa kuhisi kwamba kwa kuwa yupo msaidizi na analipwa kila mwezi basi kazi zote za ndani na za nje ni za kwake.

Kumbe kwa upande mwingine watoto ndo wanaharibika.
 
Na wakiajiriwa huwa hawachukui round either wanafukuzwa au wanaacha kazi.

Na ni mizigo hatari kwenye ufanyaji kazi.

Ni mitoto flani mizembezembe isiyotaka kujishughulisha.
 
Haujui hata unachoongea😀

Hauwezi kudelegate kazi ambayo hata ww mwenyewe kuifanya ni ngumu kwako.

Na nikuambie tu huwa hawaji kuwa waratibu, na huwa wanakuja kuishi kwa survival na dependence ya hali ya juu kutoka kwa wazazi wao.

Ni watoto ambao hawana self discipline, self reliance.

Ni watoto ambao kuhandle hata ndoa au mahusiano kwao ni ngumu.

Ni watoto ambao hata kupanga life budget yao tu huwa hawawezi.

Ni watoto ambao wako FRAGILE in every aspect of life.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…