Wazazi tunafeli sana kulea watoto

Wazazi tunafeli sana kulea watoto

Emar

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2018
Posts
1,786
Reaction score
3,092
Habari wakuu,

Bila kupoteza mda hebu nijikite kwenye mada

Jamii yetu imezungukwa na utamaduni tofauti katika kukuza na kulea watoto, wapo wanaoamini kuwa hatupaswi kuiga tamaduni za kimagharibi za kuwapa uhuru watoto badala yake wanawafunza watoto katika kufanya kazi za nguvu na kuwa na elimu na maarifa ya kujitegemea ila wapo pia wanaohisi Zama hizo zimepitwa na wakati na kuamini katika kumpa uhuru na kumpa kila atakacho mtoto wakiamini ndio malezi bora, yote kwa yote sawa hebu tusiende huko sana.

Kuna msemo unasema usikosee vitu vitatu katika maisha
1.MUNGU wa kumwabudu 2. Mke wa kuoa 3. Malezi ya mtoto

Kwenye hili la tatu limekuwa sugu sana, unaeza kuona kijana mtu mzima anauwezo mkubwa tu wala hana mchango na hata hakumbuki kwao na mda mwinine amejishikiria kwa upande wa mwanamke (mkew/mchumba)

Watu wengi hulaumu matokeo bila kuangalia misingi au chanzo na shina la tatizo na hukosoa husema vibaya bila kujua nini sababu hasa

Pili unaweza kuona moja ya watoto toka udogoni wanachuki baina yao haswa kiasi ya kwamba hata kutishiana maisha na hawawezi kukaaa pamoja kupanga maendeleo kwasababu wenyewe hawajazoeshwa kuwa hivyo, nini sababu?

Sababu kubwa hapa ni wazazi kipo kisa nitakileta changu mimi mwenywe kikihusiana na haya mambo ila leo ngoja nijikite kwenye mada.

Katika jamii zetu unaweza kuta Mzazi anampendelea mtoto mmoja waziwazi , unaweza kuta kwenye kusoma mfano ada,nguo, safari wakati wengine au mwingine hapewi kipaombele hasa wale wa rika linaloendana, hii mbaya sana uamsha chuki kati ya mzazi na mtoto

- Unaweza kuta mzazi ana shabikia mtoto mmoja ampige mwingine au aonewe bila sababu hata kama kukiwa na sababu nayo hii siyo nzuri kabisa

- Wazeza kuta mzazi yupo kumtamkia mtoto mmoja maneno ya kmkatisha tamaa mbele ya wenzake kila mara tofauti na wengine hii huasili sana saikolojia ya mtoto.

- Unaweza kuta Baba anampiga mke wake au kumtukana mbele ya watoto, aisee Jomba kama huko hivi jiandae na komeshwa ya uzeeni

- Waweza kuta Mzazi ana mpa huduma mtoto mmoja anamwacha mwingine bila sababu yoyote ile, kisa mmoja yupo favoured sana au yupo na sifa furani ambayo wengine hawana. Hili ni Bomu kubwa unaliandaa

- Au kuonesha mapezni kwa mmoja wa watoto kutokana na uzuri wa sura, akili au kipaji

Kuwa mzazi ni kuwa kiongozi hutakiwi kuonesha aina yoyote ya ubaguzi , upo ubaguzi wa kisasa wa wazazi na hasa wazazi wa kike kuwatenga watoto wao kutokana na vipato vyao.

Kwenye Malezi tuwe makini sana, kuna msemo wanasema watoto wadogo ni wepesi kusahau huu msemo si sahihi watoto wadogo ni wazuri kutunza kumbukumbu hasa pale wanapotendewa jambo lisilofaa na mtu wa karibu

Wazazi wengi wamekuja na nyuzi za kulaumu watoto kama wewe ulifanya moja kati ya hayo hapo juu kaa utulie hayo ndo malipo yako.

NAWATHILISHA.................
 
Back
Top Bottom