Wazazi tekelezeni wajibu wenu

Jpinduzi

Senior Member
Feb 26, 2011
136
68
AfricanChildren%255B1%255D.jpg
​
malezi ni kati ya maswala nyeti yanayopaswa kupewa uzito unaostahili miongoni mwa wazazi, familia, jamii na Kanisa/msikiti kwa ujumla. Hii inatokana na uwepo wa mabadiliko makubwa katika ulimwengu wa utandawazi na maendeleo ya sayansi na teknolojia ya mwasiliano ya habari, ambayo yanaendelea kuufanya ulimwengu kuwa kama kijiji.Maendeleo haya yanawafanya watu kuwa na mwingiliano wa tamaduni, mila na desturi, hali ambayo kama watu hawatakuwa makini zaidi, wanaweza kujikuta wakikokotwa bila kuwa na msimamo thabiti katika masuala yanyogusa imani, maadili na utu wao. Kuna hatari ya kuiga kila jambo,hali ambayo kimsingi haina tija wala mafao kwa malezi na maendeleo ya watoto kwa Kanisa/msikiti na Jamii kwa ujumla. Matokeo yake yanaweza kuonekana katika kumong'onyoka kwa tunu msingi za kimaadili, kiutu, kikristo na hata pengine zile za kiafrika zinazoheshimiwa na kuthaminiwa kama sehemu ya utambulisho wa kiafrika.

Licha ya taabu, magumu na mahangaiko ya maisha wanayokabiliana nayo wazazi na walezi katika maisha yao ya kila siku, lakini malezi kwa watoto wao yanapaswa kupewa msukumo wa pekee. Ikumbukwe kwamba, watoto wanahitaji malezi ya kiroho, kimwili, kiakili na kisaikolojia, kwa kutambua na kuheshimu kwamba, hii ni dhamana nyeti inayopaswa kutekelezwa na wazazi ndani ya familia, kwani wao ndio waalimu wa kwanza ndani ya familia. Misingi ya malezi ikiyumba. kuna hatari ya kupata jamii isiyokuwa na misingi bora ya malezi.
kila mtu anapaswa kuwajibika barabara katika malezi ya watoto, bila kutegeana wala kuviachia vyombo vya mawasiliano ya jamii kuifanya kazi hii kwa niaba ya wazazi au jamii . Utu na heshima ya kila mtoto vizingatiwe na kupewa kipaumbele cha kwanza kabisa, kila mtu akitekeleza wajibu wake, kwa hakika watoto wapafanikiwa kuwa na malezi bora.
 
Back
Top Bottom