Wazazi msitukane matusi mbele ya watoto

kibovu kichwa

Senior Member
May 17, 2019
145
106
Wakubwa habari Zenu!

Nichukue nafasi hii kuwakumbusha ndugu zangu mliobahatika kuwa wazazi japo mimi sina mtoto bado lakini hiki kitu kinanisikitisha. Kuna jirani yangu ni Single mama, anawatoto wanne wote ni wadogo chini ya miaka 7, wawili kati yao ni mapacha.

Huyu Dada yeye ni mtu kucharuka charuka hovyo unakuta anawatukana watoto wake matusi makubwa kabisa. Huwa tunamwambia anaharibu watoto na kiukweli tayari majibu yameanza kuonekana.

Nimekasikia katoto kake ka kike kanamtukana mwenzake aliyeenda kucheza hapo kwao eti " B..l.. la baba ako na mama ako anat..mb.. " kiukweli nilibaki mdomo wazi kusikia mtoto wa miaka 5 anatukana matusi mazito namna hiyo. Hivi wazazi wa siku hizi mbona wanakuwa wa hovyo namna hii.

Ni bora mtoto asikie hayo matusi huko nje lakini kitendo cha wewe mama kuwavurumishia matusi watoto wako mwenyewe unategemea nani aje awafundishe kwamba matusi ni mabaya. Jamii ya sasa inasikitisha sana tafadhali wazazi tusijisahau namna hiyo kuanza kuharibu maadili sisi wenyewe!
 
Wazazi wenyewe ndio hao baba na mama wote wanyoa viduku, mbaya zaidi wakiwa faragha tena kwenye vyumba vya kupanga wanatukana na kipiga makelele kama wapo club.
 
Umeskia hilo huku uswahilini kwetu mama hajui mtoto analala wapi wanapishana kama mtu na mke mwenza,matusi yamegeuka kiunganishi cha neno na neno
 
Back
Top Bottom