Wazazi katika hali mbili tofauti.

Wazazi katika hali mbili tofauti.

Maserati

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2014
Posts
11,602
Reaction score
20,098
Habari wana jamvi,
Natumaini wote wazima na mmekuwa na Eid Njema.

Niende kwenye mada sasa.
Namfahamu Jack kwa muda mrefu ni mrembo na mkarimu,lakini Jack alikuwa na mahusiano mazuri tu na mvulana wake Kimwe toka wapo chuoni. Weekend zote walishinda pamoja Am to Pm,Walipendana kweli kweli. Hatimaye wakamaliza chuo,Kimwe au Mr.K baada ya kuajiriwa na ofisi Fulani ya madini hapa Dar akaomba kumuoa Jack,jack akakubali na kumruhusu aonane na wazazi wake. Wote wawili wakapata nafasi ya kuonana na wazazi wa mwenzie.

Balaa lilianza baada ya kuwakutanisha wazazi wao yaani wa Jack na Kimwe. Jack ni wa hali ya kawaida na Kimwe ni mboga saba,wazazi wa pride na Ego hasa mama zao. Mama Kimwe hataki mtoto waje aoe binti yule wa hali ya chini na kabila Fulani (sitalitaja) eti ni Malaya sana huko mikoa ya kagera na kuzunguka huko kote wanalijua. Mama Jack hakupendezwa na kauli zile,akamjia juu mama Kimwe,wakachambana kila mtu akala kona ake.

Jack na Kimwe wakakutana,wakajaribu kuongea wao kama wao na kila mmoja akadhihirisha kumpenda mwenzie,na wanataka waoane hawajali ya wazazi. Lakini hawawezi kuoana ikiwa mama zao hawana mahusiano mazuri na hawataki kuishi ile ya karibu pangu pana nafasi tuishi sote. Wakakubaliana waongee na wazazi wao,wawaelezee kama wanapendana na wanataka kuoana,waweke mbali tofauti na kusameheana,kisha waende vacation na wazazi wao,Kimwe atasimamia show.

Wote wakajikuta wamefika Serengeti National Pack na kukutana na familia ya wenzao,wakasalimia vizuri na kuombana msamaha,mama Kimwe akatoa pochi yake na kumpa Zawadi ya hereni mama Jack,mama jack akapokea,akazisifia na kuzifurahia. Mama Kimwe akamwambia hizo ni za bei ghari sawa sawa na ela yenu ya kula mwaka mzima. Mama Jack akamtulia usoni,hasira zikawapanda wakajikuta wanavaana na kugalagazana chini.
Wakati huo wababa walikuwa pembeni wanaongea,hawana tatizo kabisa. Wakashtushwa na makelele,kuokoa ugomvi mama Kimwe anavuja damu puani,vacation ikafa.

Kimwe na jack ndio victims,maana wao wanapendana sana,na wanataka waishi pamoja. Lakini wazazi wao hasa mama zao,wanawapa wakati mgumu sana kutokana na hali zao. Kila mmoja akiapia kumpa radhi mwanae ikiwa atakiuka maneno,yake kwa kuoa au kuolewa mpenzi wake Huyo. Baba zao hawana tatizo kabisa na wameruhusu watoto wao waoane,wana hofu kwa maneno ya wazazi wao hao...

Jack ni rafiki yangu wa karibu sana,kaniomba ushauri. Nikijaribu kufikiria umuhimu wa mama naishiwa nguvu,nashindwa nimshauri Nini. Jack Analia tu kila siku,akitaka jaribu kumuomba mama yake waongee mama anadai hawezi kuvumilia udharirishaji na uonevu,wanaishia kugombana and the vice versa kwa Kimwe mama mtu anadai hawana adabu na wakorofi sana,na wao wakijadili hili wanaishia kugombana na mama ake. Jack anatafutiwa kijana wa kuolewa nao lakini hataki kabisa,anamtaka Kimwe.

Kama wewe unashauri Nini katika hali kama hii???
Karibuni kwa michango yenu
 
madhali mababa wameridhia hapo ni kuoana tu,hao wamama watapatana mbele kwa mbele.
 
Aseeh hayo mahusiano hayatakuwa na amani mpaka pale wazazi wa kike watakapopatana na kuondoa kinyongo
 
unaonaje ukafanya ka movie ka story yako

katanoga kama nn uyo mwanaume niwe mm alafu jack awe wema sepetu ukienda mbali sana nchukulie joketi ila simtaki uwoya kashazaa yule

kwani siwalikuwa wanafanya sex heeeeeh
 
Hapa duniani ukiwa humbled siku zote Mungu atakuinua lakini ukiwa kiburi na majivuno Mungu atachukua hata kile kidogo alichokupa
 
Tatizo ni moja tuu...Kimwe hajafundishwa kuwa yeye ni mwanaume na anatakiwa ajiunge na mwanaume waenzake kuongea akina baba Jack ...baba yake na yeye mwenyewe ...Mwanaume ndo mwamuzi awaache akina mama Kimwe na Mama Jack wagombane watachoka ...Jack hatakiwi kuongea yeye ni victim

carnte himself
 
Hapa duniani ukiwa humbled siku zote Mungu atakuinua lakini ukiwa kiburi na majivuno Mungu atachukua hata kile kidogo alichokupa
Tu assume we ndo Jack nami ndo Kimwe... we ungechukua maamuzi gani??
 
hapo wazazi wakiume waongee na wake zao tu naamini hakuna linaloshindikana.
 
Back
Top Bottom