Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,982
Kumekua na hii hadithi ya kuwa muuaji wa karume Humoud alilipa kisasi cha kuuliwa baba yake na Karume...huu ni uongo mwengine kuficha kisa kizima cha kuuliwa Karume.
Baba yake Humoud huyo mwarabu unayemsema alikamatwa kwa kesi ya mauaji ya kiongozi mmoja aitwaye Mugheir..inasemekana alimchoma kisu mbele ya hadara na hii ilikuwa ni kabla ya Mapinduzi..
Kesi yake ikaendeshwa na serikali iliyokuwapo chini ya muingereza na baba yake akahhukumiwa kifo
Wakati hukumu inatolewa katika kipindi kifupi znz ikapata uhuru wake na baada ya mwezi mmoja mapinduzi.
Humoud akiwa mwanajeshi alikua upande wa kina karume kwenye mapinduzi .kama yalivyo mapinduzi ya kumwaga damu basi wafungwa huwa wanatilowa kwa lengo la kujiunga na movement ya mapinduzi na walipotolewa jela baba yake humoud hakuwa mmoja ya alie tolewa kwani hukumu yake ya kuuwawa ilishatekelezwa kabla ya mapinduzi.
Hivyo karume hahusiki na ndio maana karume hakuwa na wasi wasi na humoud na humoud naye hakua ma chuki na karume kwa sababu ya baba ake..
Hivyo muuaji wa karume alikua na motives nyengine nje ya hizo
Ok mkuu asante kwa hiyo historia ila asisingiziwe tu bure mzee wa watu Nyerere!