Wazanzibari Somalia walalamika

Cha Moto

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
945
153
  • 111011111819_zanzibar_304x171_bbc_nocredit.jpg
Wakimbizi kutoka visiwa vya Zanzibar wamekwama katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, wakidai serikali ya Tanzania imeshindwa kutoa kibali kwa shirika la wakimbizi duniani UNHCR ili kuwarejesha makwao.
Wakimbizi hao walikimbilia Somalia miaka kumi iliyopita baada ya machafuko ya baada ya uchaguzi wa urais wa Zanzibar mwaka wa 2000.

Wakimbizi hao kutoka visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania wameiambia BBC kuwa mwezi Januari mwaka huu, shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR lilianzisha uratatibu wa kuwasajili kwa lengo la kuwarejesha makwao kwa hiari.
Wakati huo shirika la UNHCR liliwafahamisha wakimbizi hao wapatao 100 kuwa watarejeshwa nyumbani baada ya miezi mitatu, lakini hadi sasa mpango huo haujatimia.
"Baada ya muda huo wa miezi mitatu kumalizika, UNHCR ilituambia kuwa serikali yetu ya Tanzania haijatoa kibali cha kutuwezesha kurejea nyumbani na haitowezekana kuendelea na safari bila ya kupata kibali hicho. amesema mmoja wa wakimbizi hao Mohamed Adam Suleiman.
110807172939_dagaal.jpg
Mogadishu kuna mapigano


Bw Suleiman ametoa wito kwa serikali ya Tanzania kutoa kibali cha safari kwa UNHCR ili waweze kurejea nyumbani.
"Tunatoa wito kwa serikali ya Tanzania kutufahamisha sisi na Watanzania wengine sababu ya kushindwa kutoa kibali hicho. Pengine wana sababu zao za msingi, lakini sisi ni wakimbizi ambao tuna haki ya kurejea nyumbani."
Wakimbizi hao walikimbia machafuko ya baada ya uchaguzi visiwani Zanzibar mwaka wa 2000, baada ya kuzuka kwa mzozo juu ya matokeo ya uchaguzi wa urais, ambapo mgombea wa CCM aliibuka mshindi.
Wengi wa wakimbizi hao walikuwa wafuasi wa chama cha upinzani cha CUF, na walipitia Kenya na kuishi kwa muda mfupi, kabla ya kuelekea Somalia mwezi Septemba mwaka 2001.
Kufuatia muafaka wa kisiasa visiwani Zanzibar mwaka uliopita, na uchaguzi ambao ulimpa nafasi kiongozi wa CUF, Seif Shariff Hamad kuwa makamu wa rais, wakimbizi hawa wameamua kukubali kurejeshwa makwao.
Awali idadi ya wakimbizi hawa waliokwenda Mogadishu ilikuwa mia mbili, lakini baadhi yao wamerejea nyumbani na wengine kwenda katika mikoa mingine nchini Somalia kufanya kazi mbali mbali

source: BBC World News
 
Hii habari inahitaji kutafakari zaidi. Yaani wazazibari walikimbilia SOmalia kupata hifadhi ya ukimbizi? Walipita Kenya, wakashindwa kuja Tanzania? Hii ni siasa isiyokuwa na maana yoyote.
 
Wacha kwanza nipite .Yaani hawa wanarudi lini waliambiwa kwamba hali ya Zanzibat si kama Somalia hadi wameamua kurudi ?
 
Back
Top Bottom