Wazanzibari kuitolea kauli rasimu leo

Wazanzibari kuitolea kauli rasimu leo

Seif Shariff anamaanisha kuwa dr. Shein ni kibaraka wa bara....anasema kuwa yeye ni kiongozi wa kwanza Zanzibar kuridhia kuwa raia wake akashtakiwe kwenye mahakama kuu ya Tanzania bara ambapo ni kinyume na katiba ya Zanzibar inayoitambua Tanzania bara kama nchi nyingine...Anasema kuwa enzi za Amani Abeid Karume wale wazee waliopekeka barua UN kudai mamlaka ya Zanzibar walipelekwa kushtakiwa Tanzania bara yeye akiwa Marekani na aliporudi alimuuliza Othman aliyekuwa AG wake akamjibu kuwa wamemwambia awashtaki akawaambia haoni kosa la kuwashtaki ndipo wakachukuliwa kupelekwa bara. Amani Karume aliamuru warejeshwe na wakarejeshwa Zanzibar mara moja!
 
Wazanzibar kwa kujitambua tu wapo mbele sana. MACCM lakini hawatajali wapo radhi hata damu imwagike ili katiba ya MACCM "ipate kura ya ndiyo" hata Zanzibar. Watapelekwa wanajeshi wengi sana wakapige kura ya ndiyo. Mchezo kwisha.

Mzee moyo Hassan: Ni tatu na sii vinginevyo. Hatutakubali nchi itwaliwe.
Mzee Moyo Hassan Nasoro ameahidi kuandaa konganano kuelezea kila kitu kuhusu mapinduzi na muungano.
 
Ukawa mbele kwa mbele hadi Ikulu. Intarahamwe itakula kwao.
 
Mkutano mkubwa nashangaa wazanzibar hamtupi updates

wazanzibar bwana kwa kulega lega hawajambo sasa mkutano kama huu wanashindwa kutupa updates zozote za maana hovyo kabisa hawa watu.

UKAWA daima .
 
Seif Shariff anamaanisha kuwa dr. Shein ni kibaraka wa bara....anasema kuwa yeye ni kiongozi wa kwanza Zanzibar kuridhia kuwa raia wake akashtakiwe kwenye mahakama kuu ya Tanzania bara ambapo ni kinyume na katiba ya Zanzibar inayoitambua Tanzania bara kama nchi nyingine...Anasema kuwa enzi za Amani Abeid Karume wale wazee waliopekeka barua UN kudai mamlaka ya Zanzibar walipelekwa kushtakiwa Tanzania bara yeye akiwa Marekani na aliporudi alimuuliza Othman aliyekuwa AG wake akamjibu kuwa wamemwambia awashtaki akawaambia haoni kosa la kuwashtaki ndipo wakachukuliwa kupelekwa bara. Amani Karume aliamuru warejeshwe na wakarejeshwa Zanzibar mara moja!
 
Akihutubia maelfu ya wananchi kibanda maiti leo maalim seif amesema kuwa licha ya tume ya warioba kutumia bil 94 kukusanya maoni ya wananchi lakini cha kushangaza bunge la katiba wamepuuza maoni ya wananchi na kuya weka kando lakini kubwa sana kuifuta znz kama nchi
 
Kitatokea nini wazanzibar wakiipigia kura CUF mwakani na kuipa madaraka ya kuongoza Zanzibar na wakaamua kukabidhiana madaraka kwa amani? Au ccm bara watapeleka jeshi kuleta vurugu?
 
Hamna kitu hapo Zanzibar wameilewa katiba ya nzuri iliyopendekezwa.
 
Hicho sasa ni kiherehere si uende hukohuko Kibanda maiti au subiri uangalie taarifa ya habari
 
Back
Top Bottom