Wazanzibari kuitolea kauli rasimu leo

Wazanzibari kuitolea kauli rasimu leo

Jamhuri ya Zanzibar

Senior Member
Joined
Jul 17, 2012
Posts
127
Reaction score
195
TANGAZO!

Haya haya wazanzibari! Kumekucha! La mgambo likilia kuna jambo! Chama cha wananchi CUF kinawatangazia wanachama, wapenzi na wazanzibari wote wa mikoa mitatu ya Unguja, wazalendo na wapenda nchi yao kwa jumla kuhudhuria kwa wingi katika mkutano mkubwa wa hadhara wa aina yake na wa kihistoria utakaofanyika leo Jumapili ya tarehe 12/10/2014 katika viwanja vya Kibanda maiti, Unguja.

Mageni rasmi katika Mkutano huo ni Simba wa nyika, tishio la vibaraka wauza nchi yetu, kipenzi cha wazanzibari, mwenye uzalendo wa hali ya juu na mapenzi makubwa kwa Zanzibar na wazanzibari, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
.
Mkutano utaanza saa 8:00 barabara za mchana mpaka saa 12:00 jioni.

Ni sasambusasambu ya rasimu yenye majina mengi:

a) Rasimu ya vijisenti.
b) Rasimu ya Sitta
c) Rasimu ya vitisho.
d) Rasimu iliyopendekezwa na CCM, iliyojadiliwa na CCM na iliyopitishwa na CCM.
e) Rasimu ya uchakachuaji.
f) Rasimu ya fax, sms, twiter, facebook, viber, skype na tango
g) Rasimu ya kura za Hamad Rashid.

Hivi Rasimu hii ndio imeshapita? Hivi biashara ya kuiuza Zanzibar na wazanzibari ndio imekamilika? Nini kinachofuatia?

Maswali yote hayo yatapatiwa majibu pamoja na mambo kadhaa muhimu.

Hatumwi mototo!

Shime wazanzibari wote kuhudhuria kwa wingi bila ya kukosa!
Mkutano utarushwa moja kwa moja kupitia
1. Kituo cha televisheni cha SIBUKA katika king'amuzi cha Startimes.
2. Kituo cha Radio cha chuchu FM 90.9.
3. Mtandaoni katika live stream ya chuchu FM radio www.chuchufm.com.
Ni leo Jumapili saa 9 mchana huu.

CHUCHU.jpg sibuka.jpg
 

Attachments

  • MAALIM 2.jpg
    MAALIM 2.jpg
    3.2 KB · Views: 6,729
Kila la kheri. Kumbuka katiba mpya ya Zanzibar imefutwa na katiba pendekezwa ya ccm. Reference zote ktk katiba pendekezwa ni za Katiba ya Zanzibar ya mwaka 198...
 
Wawakilishi wa Z'Bar wameshanena kwenye BMK
 
Wawakilishi wa Z'Bar wameshanena kwenye BMK

Kwani wao ni MIUNGU hivyo kauli yao haipingwi na mwengine!??

Wale ni vipapa kunuka wanaoendekeza dhiki na ujinga wao kwa kuiuza Zanzibar kwa maslahi yao na familia zao! Tena maslahi yao ni ya muda Mfupi!!

Umeona wapi MTU kuweka REHANI nyumba yake kwa ajili ya kukopa kilo ya Mchele!!!??? Wale ni mbwa koko wasioitakia mema Zanzibar.
 
Mwenyezi Mungu awaajalie mmalize salamu huo Mkutano muhimu kw maaslahi ya Zanzibar.

Pasije tokea Police CCM kuharibu huo Mkutano...,
 
..wazingatie uhuni aliofanyiwa mwanasheria wao,alikubali yote kwa maslahi yao...
 
Umeniacha hoi mkuu kwenye majina ya hiyo katiba
 
Si waongee na STAR tv ili huku Tanganyika tuone mnavyomsasambua SITTA na fisadi CHENGE
 
Hapo kwenye g.
Wazanzibari msiwe na wasiwasi huyo jamaa "ba Hamadi" Tanganyika ikirudi tutamrudisha kwao Zanzibar hivyo mtapata nafasi ya kumhukumu kwa mikono yenu wenyewe.
Hata huku Tanganyika anatusumbua sana mara atupangie ni aina ngapi ya serikali tuwe nazo, mara hivi mara vile ahh!
 
jamhuri ya zanzibar

hiyo chuchu fm inashika huku Dar au mwisho Chumbe?

Nawatakia kila lililo la kheri mnapopigana na shetani (ccm) kupitia kwa agent wakuu Sitta, Chenge & Hamad Rashid
 
Last edited by a moderator:
Mtetezi halisi wa Zanzibar alikua Jumbe, hili lipenda vin'gola siyo la kuamini kabisa halichelewi kusaliti pale linapoona madaraka yatachukuliwa na mtu mwingne.
 
jamhuri ya zanzibar

hiyo chuchu fm inashika huku Dar au mwisho Chumbe?

Nawatakia kila lililo la kheri mnapopigana na shetani (ccm) kupitia kwa agent wakuu Sitta, Chenge & Hamad Rashid

Chuchu FM kwa kupitia Masafa ya FM hata Dar inafika ila si kwaubora sanaaaa ila unaweza ukatumia stream yao ukawapata popote pale duniani
 
Last edited by a moderator:
jamhuri ya zanzibar

hiyo chuchu fm inashika huku Dar au mwisho Chumbe?

Nawatakia kila lililo la kheri mnapopigana na shetani (ccm) kupitia kwa agent wakuu Sitta, Chenge & Hamad Rashid

Chuchu FM kwa kupitia Masafa ya FM hata Dar inafika ila si kwaubora sanaaaa ila unaweza ukatumia stream yao ukawapata popote pale ulipo katika dunia hii.

http://myradiostream.com/v1/mobile/chuchu
 
Last edited by a moderator:
Mleta mada hakikisha huku Bara unatujuza full datta mkuu,tuna usongo na hawa ma Interahamwe ile mbaya.
 
hao ccm pia ni wananchi na ndio wameaminiwa na waznz wengi

CCM hawajaaminiwa na wengi wa Wazanzibari ila ni uchakachuaji wao tu katika kila mambo kutokana na hofu yao ya kwamba wanajua siku wakianguka watapelekwa The Hague kuungana na Uhuru Kenyatta!

Uchaguzi wa kura ya maoni ya kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa waliosema NDIYO walikua 66%

Uchaguzi Mkuu 2010 Kura za Lipumba kwa upande wa Zanzibar pekee ni 67%

Utoaji wa maoni kuhusu katiba Mpya kwa mujibu wa takwimu za kitaalamu 66% Walitaka Muungano wa Mkataba (Takwimu za Warioba ni 61%)

Cha kushangaza pamoja na takwimu zote hizo lakini Tuliambiwa ushindi wa CUF uchaguzi wa 2010 ulikua ni 49.9%!!!!!

Lambda tuwaulize ZEC iweje Lipumba apate 67% na Maalim apate 49% wakati Mzanzibari akienda kupiga kura jambo la mwanzo anamuangalia Maalim Seif na mengine yanafaata baadae. Kama CCM mupo wengi Warioba. ameshasema TUTAKUTANA MTAANI
 
Mtetezi halisi wa Zanzibar alikua Jumbe, hili lipenda vin'gola siyo la kuamini kabisa halichelewi kusaliti pale linapoona madaraka yatachukuliwa na mtu mwingne.

Wewe ulitaka akupende wewe!!!!????

Maana kwa Tanzania ya leo simuoni ambayo hapendi ving'ora! Kila siku tunaona hapa Dar as salaam hadi mahabusu siku hizi wanasindikizwa na ving'ora!

Wewe utakuwa MTU wa ajabu sana kama hupendi ving'ora, mimi hapa ninavitaka sana ili vinisaidie kufika haraka kule ninakotaka kuenda
 
Ccm washenzo sana waliambiwa mapema san kuhusu ubora wa serekali tatu wakajiona wajanjanja kumbe mazuzu sas jamaa wanataka serekali ya mkataba imekula.sijuwi wataweka wapi sura zao na hii ya mkataba haitashindikanda maana kiranja wa dunia ndiye atakaye simamia huu mkataba bora mkoloni mweupe kuliko mkoloni mweusi!!
 
Back
Top Bottom