Mkuu! Hali ya kiuchumi ya smz ukilinganisha na huku bara ni tofauti kubwa sana, moja, inatoa fursa kwa wabunge hawa kukopeshwa magari na uwezo wa kukopa mali tofauti, mshahara wa mbunge na marupurupu hapa kwetu (nakubali kusahihishwa) ni zaidi ya Tshs 7.2m, nina hakika wa thread hii watakuja wadau wenye takwimu rasmi na kuthibitisha kuwa wabunge wa znz huimba kile wananchi wao wasichokiimba hasa inapokuja suala la muungano.
Tizama hawa wa cuf kwa mfano; Lipumba na Mtatiro hawakubaliani na mswaada wa kuweka utaratibu wa kupata katiba, wao wanataka wananchi washirikishwe lakini kina Khalifa na Rashid wamefunga ndoa na ccm bungeni na siri yao kubwa ni kulinda maslahi yao kwani Kambi ya Upinzani inataka nafasi ya znz iangaliwe kwa umakini