Wazamiaji wa miaka ya 90

Hako kaneno ka kizungu ka mwisho kamenikumbusha mbongo mmoja alipigwa risasi na majambazi huko majuu
Kuna screenshot fulani zilikuwa zinatembea za fb akiongea na jamaa zake wanamuuliza mbona amepotea sana akajibu mambo hayajakaa sawa "I'm not in a confort zone"
Hapo ni mtu mzima na ana watoto wakubwa tu huku amezamia kule sijui nini kilitokea lakini ilibidi aolewe

Huku ukikwama utajua namna ya kufanya au utarudi kijijini lakini huwezi kufikia kulazimika mwanaume mzima kuolewa
Sisemi huku hakuna mafirauni lakini ogopa sana kufanya jambo kwa kuwa tu huna namna, huambatana na majuto

Huko hamjanishawishi
 
Exposure inajumuisha Kusikia, kusoma na kujifunza

Sio lazima nifike huko, naweza kupafahamu vizuri bila kufika
 

Mkifika huko mnaishi kama mabata tu, mnarisk sana maisha halafu mnapeana moyo kijinga hapa
 
Punguza stress mkuu, unaandika kwa stress sana , kuna mambo yanakutatiza?
 
Maisha kweli yana mengi dah.. hilo eneo ni gumu mno mno mkuu
 
Kuna jamaa yangu kaenda Kismayu Somalia kulikuwa na Kazi ya Kusimamia Boti, Kakaa mwezi amerudi mwenyewe maisha ya Kule yamemshinda.
 
Kuna jamaa yangu kaenda Kismayu Somalia kulikuwa na Kazi ya Kusimamia Boti, Kakaa mwezi amerudi mwenyewe maisha ya Kule yamemshinda.
Watu wanajilipua, miaka ya 2013/14 kuna jamaa flani alikuwa anasoma sauti alikuwa anaenda Somalia na Sudan huko kufuata bidhaa za magendo.
Jamaa alikuwa ashaanza kuwa vzuri ila kuna siku waliwanyanganya kila kitu
 
Ila kiukweli wazamiaji wengi wa enzi hizo walikuwa "wakurupukaji" sanaa labda ndio maana iliitwa "kujilipua", siku hizi mambo yanafanyika kwaakili zaidi kuliko kufuata mihemko.
Shukuru waliogundua mtandao, enzi hizo hakukuwa na vitu hivi.
 
Kuna mtu anaitwa Kaka Vale huyo.

Jamaa mweupe pee ukimuangalia utafikiri half cast.

Basi aliondoka Bongo kiajabuajabu miaka ya 1980 ya kati huko. Hapo airport walimbana anaenda wapi. Akasema yeye mtoto wa Gorbachev anarudi kwao, miaka hiyo Gorbachev anaongoza USSR. Basi watu wa airport wakaogopa wakamuacha apite.

Basi kazunguka sana Italy na Greece watoto wa Migomigo wa beach kawasaidia sana.

Kuna siku alikuja Bongo akatuachia Mercedes Benz atumie Aunt (Mama yake).

Basi yeye alivyoondoka, ile Benz tukawa tunapiga nayo misele Dar.

Siku moja tukawa tunapiga misele Magomeni. Kuna watoto wa Magomeni wakatufuata. Wakatuuliza hii gari ya Vale, nyie wadogo zake? Tukasema ndiyo sisi wadogo zake.

Basi wale jamaa walifurahi sana wakasema kaka yenu katusaidia saana Greece hapo beach. Wakapiga picha na sisi ikawa kama wamekutana na ma celebrities fulani wakawa wanaitana "Njooni muwaone wadogo zake Vale".

Nikasema kweli unaweza kumfanyia mtu wema halafu usijue huo wema utadumu vipi.
 
Wema ni akiba, japo siku hizi wana sema tenda wema nenda zako maana huchelewi kusagiwa kunguni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…