Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,794
- 165,533
Kila nikikaa na kuwaza kuhusu hatima ya grand corruption katika nchi hii, kwakweli sipati majibu mithili ya kukaa na kujiuliza Mungu alitoka wapi au kati ya kuku na yai kipi kilianza kuona jua.
Ukweli ni kwamba ni tuhuma za rusha kubwa katika nchi hii ni nyingi kana njiti za kiberiti na uwwzekano wa kupeka kesi hizo zote mahakamani kwa kifupi haupo na hata zikipelekwa baadhi zinaweza kufutwa kama ambavyo baadhi ya kesi kubwa kubwa zimewahi kufutwa.
Labda niulize,hivi kuna kesi ya wizi wa kuku au ya wizi wa simu iliyowahi kufutwa na DPP zaidi ya hizi kesi kubwa kubwa?
Mimi nafikri badala ya kupeana matumaini ambayo hayapo kwamba kuna mtu atafukua makaburi na wahusika wote watafikishwa katika vyombo vya sheria ni bora tukafikiria kuunda Tume ya kutafut ukweli na maridhiao kuhusu ufiasi katika nchi hii ila kwa kuweka sheria na mashariti maalumu katika kufikia maridhiano hayo.
Kabla sijaendelea labda niwape mfano mmja tu ambao kila mmoja wetu anapaswa kuutafakari.
Je,leo hii kama serikali itaamua kuchunguza mchakato wa ubinafsishaji wa mashirika yote ya umma na wahusika wote bila kujali vyeo vyao wachukuliwe hatua,jambo hili litawezekana?
Na labda tujiulize swali lingine:
Katika miaka hii miwili ya Magufuli, zimeshaibuliwa tuhuma ngapi na wangapi leo hii wako jela au mahabusu kwa tuhuma hizi?
Ukweli mchungu ni kuwa, kushughuliia tuhuma za ufisadi na watuhumiwa wa ufisadi ni jambo ambalo CCM hawawezi kulifanikisha sana sana watachagua tu baadhi ya kesi za kushughulika huku tuhuma zingine zitabaki kuwa historia labda mpaka siku CCM itoke madarakani.
Kwa kuzingatia ukweli huu,binafsi ndio maana nimekuja na hili wazo la kuunda hii Tume ya kutafuta ukweli na maridhiano ila kwa mashariti na taratibu zifuatazo.
1.Tume hii iwe ni ya muda maalamu na ipewe nguvu za kisheria na kikatiba ikibidi.
2.Tume hii ipewe mamlaka kisheria ya kutoa msamaha kwa wote wakaokiri kuhusika na vitendo vya ufisadi.
3.Tume iwajibike kisheria , tena bila mashariti,kutoa taarifa za wahusika kwa mwananchi yoyote atakaependa kujua findings za kamati.
4.Baada ya Tume kuvunjwa,Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikabidhiwe jukumu la kutoa taarifa hizi kwa mwananchi yoyote anaetaka kujua nani alihusika katika ufisadi fulani.
5.Tume hii ishughulike na makosa yaliyotendeka kabla ya tarehe ambayo Tume hii itakuwa imeundwa na kuanza kazi rasimi na si vinginevyo.
6.Tume hii iwe ni tume huru na iwe ni tume ya kijaji.
7.Tume ipewe mamlaka ya kisheria kuchunguza mtu yoyote na tuhuma yoyote bila kujali wadhifa wake.
8.Mtuhumiwa atakaekataa kutoa ushirikiano kwa maana ya kukiri makosa yake na kuomba msamaha mbele ya Tume aondolewe katika msamaha wa jumla na akajitete/ akajisafishe mahakamani kwa tuhuma zinazomkabili.
9.Kuwe na adhabu kali za kimahakama kwa watuhumiwa wote watakaokaata kutoa ushirikiana kwa Tume kwa kukataa kukiri makosa yao mbele ya Tume pale watakapopatikana na hatia mahakamani.
10.Wale wote watakaokiri makosa yao na kupata msamaha mali zao zote zitaifshwe na serikali.
11.Mtu yeyote atakaendelea na vitendo vya rushwa na ufisadi mara baada ya kuundwa rasimi kwa Tume hii,mtu huyo ahukumiwe adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela pasipo kulipa faini na kuachiwa au hata afungwe kifungo cha maisha.
12.Raisi asiwe na mamlaka yoyote ya kusamehe mtu yoyote atakaepatikana na hatia na kisha kufungwa jela baada ya kukataa kukiri makosa yake na kuomba msamaha mbele ya Tume.
Wapinzani,hata siku na nyinyi mkifanikiwa kushika dola,nawashauri mfanye hivi hivi maana mkiamua kufukua makaburi hakika miaka mitano itaisha mnakimbizana na makesi makubwa makubwa na mwisho wa siku mtajikuta mmetumia fedha nyingi sana na muda mwingi kuhangaika na kesi za aina hii badala ya kutimiza ahadi zenu kwa wananchi.
Tumefanya kosa kubwa sana la kutawaliwa na chama kimoja kwa miaka mingi na haya ndio matokeo yake.
Katika hili, najua kuna watu watanipinga ila nitawauliza maswali haya:
1.Je,wote wanaofutiwa kesi ni kweli hawana makosa?
2.Kama wana makosan,msamaha wa DPP utakuwa na tofauti gani na ule utakaotoewa na Tume hii?
3.Je,hakuna watakaoshinda kesi mahakamani hata kama walituibia na kubaki wakitanua na mali walizozipata isivyo halali?
4.Msamaha wa Tume hii utakuwa na tofauti gani na ule uliotolewa kwa wezi wa fedha EPA kwa shariti la kurudisha fedha walizoiba?
5.Pamoja na kelele za kupinga msamaha ule,nini kilifanyika?
Tafakari.