Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,914
- 16,528
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, amesema hayo Mei 11, 2026, wakati akiwasilisha uchambuzi wa chama hicho kufuatia ripoti ya Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu 2025.
"Vilevile swala la ukiukwaji wa haki za binadamu, Tume imedogosha madai ya utesaji ilihali TLS kupitia msaada wake wa kisheria imebaini kuwa watuhumiwa wengi waliteswa, kunyimwa haki zao na kushikiliwa kinyume cha sheria.
Wengi mliona watu wamefika wamevunjwa mikono, wengine wamefungwa na katani na miti—umewahi kuona mtu amevunjwa mkono akafungwa na katani na miti? Mwingine yuko uchi, kafika na boksa mahakamani. Mwingine kavaa kadera, unamuona kabisa huyu alikuwa nyumbani amelala, kakurupushwa mwanamke hajasitiriwa, anafikishwa mahakamani. Kuna watu hawawezi kutembea wamevunjwa miguu yote miwili, wengine wamevunjwa mikono; Tume haijasema chochote kuhusu ukiukwaji huu mkubwa.
Vilevile kukosa mapendekezo ya fidia stahiki kwa waathirika, ambapo Tume ilienda kana kwamba mtu aliyevunjwa mkono labda apewe mkono wa bandia alafu aondoke. Lakini tunasahau kwamba kuvunja ule mkono au ule mguu umempunguzia uwezo wa kupata kipato, uwezo wa kushindana katika kuzifikia fursa. Kwa hiyo tulitarajia Tume iseme jambo.
Katika swala la kuhimiza ukweli, haki na uwajibikaji ili kufikia maridhiano; Tume inazungumzia maridhiano lakini haizungumzii msingi wa ukweli, haki na uwajibikaji ambao ndiyo kiini ambacho kingeweza kuliponya na kulileta taifa pamoja. TLS tunaamini kwamba tukiwa na ukweli, kwamba 'samahani, mimi ndiyo nimefanya jambo fulani na ninawajibika kwa hili', ile ni hatua kwenda uponyaji wa taifa.
Kila mtu anakataa na shutuma kubwa zimekuwa zikielekezwa kwa vijana... wengine wanawaita 'Gen Z'. Jambo ambalo si kweli; sababu zote zilizosababisha vurugu za Oktoba kama mnavyoziona ni sababu za wazee—kushindwa kuwajibika na kuandaa mfumo wa kisheria. Hakuna sababu yoyote inayohusiana na vijana kwa sababu tulizozibainisha mbele yenu kama TLS. Tume katika hotuba yake haijatoa mwongozo wa fidia... yaani imetoa kitu ambacho kwa kweli ukijiuliza ni kwamba they don't care."
Soma pia Tathmini ya TLS kuhusu Ripoti ya Tume ya Jaji Chande na Kesi za Jinai zinazomkabili Tundu Lissu