Wawakilishi Nao!

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wametaka kutengewa fedha maalumu kwa ajili ya kujengewa nyumba katika majimbo yao kama ilivyokuwa zimetengwa fedha hizo na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inayo nia ya kujenga ofisi za wajumbe wa baraza la wawakilishi katika majimbo ya uchaguzi kwa Unguja na Pemba kama ilivyokuwa kwa wabunge.

“Napenda kuwahakikishi wajumbe kwamba serikali ya mapinduzi Zanzibar inayo ni ya kujenga nyumba kama hizo kwa ajili ya waheshimiwa wajumbe wa baraza la wawakilishi majimboni mwao, hali itakaporuhusu kwa muda huu tunawaomba waheshimiwa wawe na subira mpaka uwezo wa kufanya hivyo utakaporuhusu” alisema Waziri huyo.

Hata hivyo baadhi ya wawakilishi wamemwambia Waziri huyo kwamba serikali ya mapinduzi Zanzibar haina nia ya kuwajengea ofisi na ndio maana hadi leo hii hakuna michoro ya ujenzi wa nyumba hizo wala kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya kazi hiyo.

“Pamoja na majibu mazuri ya mheshimiwa waziri lakini mimi nina wasi wasi na aliyoyaeleza kama kweli kuna nia basi angalau kungekuwepo na michoro au vifungu vilivyotengwa angalau lini au mwaka gani lakini sio kuambiwa kuna nia ya serikali ya kujenga wakati hakuna hata huo mpango uliopwangwa” alisema Ame Mati Wadi Mwakilishi wa Jimbo la Matemwe (CCM).

Waziri Juma aliyasema hayo wakati akijibu maswali mbali mbali ambapo swali la msingi liliulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujuwa lini serikali ya Zanzibar itawajengea wawakilishi wake majengo kama hayo ambayo yatasaidia kwa kisi kikubwa wananchi kushughulikia kero zao.

Waziri Juma alisema ni ya kujenga majengo hayo ipo lakini kutokana na hali ya kifedha bado kazi hiyo haijafanywa lakini kwa hivi sasa wanaweza kushirikiana na nyumba zinazojengwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambazo ni za wabunge kuweza kushiriana nao.

Mwakilishi huyo alisema hivi sasa bunge la jamhuri ya muungano wa tanznaia limeanza ujenzi wa afisi za wabunge majimboni zinzotarajiwa kugharamu shilingi 40,000,000 milioni ambapo baadhi ya nyumba hizo yatari zimeshakamika na kumtaka waziri atoe maelezo iwapo anafahamu suala hilo ambapo Waziri Juma alisema kwa ufupi kwamba analifahamu.

Mwakilishi huyo alisema jimbo la Chake Chake Pemba na Jimbo la Chaani Unguja tayari nyumba hizo zimeshajengwa pamoja na kutengewa fedha kwa ajili ya mfuko wa maendeleo wa jimbo na kuwekewa bima ambapo alitaka kwa nini ikiwa mbunge amepatiwa huduma hiyo huku mwakilishi akiachwa akidhalilika.

Waziri Juma alikiri kuwa serikali ya mapinduzi ya zanzibar inayo taarifa ya kuwepo kwa kazi za ujenzi wa ofisi za wabunge katika majimbo ya uchaguzi ambayo kazi hiyo imeanza katika majimbo ya Chake Chake Pemba na Koani Mkoa wa Kusini Unguja.

Alisema ujenzi wa ofisi za wawakilishi katika majimbo ua uchaguzi ni muhimu kwa sababu zitajenga mahusiano mazuri zaidi kati ya wawakilishi pamoja na wananchi katika majimbo ya uchaguzi.

Juma alisema nyumba hizo zitarahisisha utekelezaji wa malengo ya kazi katika majimbo ya uchaguzi kwa wabunge,wawakilishi na wananchi kwa ujumla katika kushughulia matatizo yanayojitokez akatika majimbo yao.

Hata hivyo Waziri huyo alisema hali itakaporuhusu kwa upande wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar basi itajenga ofisi hizo kwa upande wa wajumbe wa baraza la wawakilishi lakini kwa sasa wanaweza kushirkiana na wabunge katika kutumia ofisi hizo.

waziri huyo aliwataka wabunge katika majimbo ya uchaguzi kutumia ofisi hizo sambamba na wajumbe wa baraza la wawakilishi ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao ambayo ni kuwatumikia wananchi wa jimbo husika bila ya kujali kuwa ofisi hizo zimejengwa na bunge.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mustafa Mohammed Ibrahim alisema wapo baadhi ya wabunge walikaa pamoja na wawakilishi na kutengeneza ramani ili kuongeza chumba kimoja kiwe cha wmakilishi lakini matokeo yake michoro ile ilipopelekwa bungeni ilikataliwa.

“Mimi nilikaa na mbunge wa mwakilishi wa jimbo la Koani lakini na kukatengenezwa michoro ya kuongeza chumba kimoja lakini matokeo yake michoro ile ilipopelekwa kule bungeni ilikataliwa sasa hebu tuelezwe hili ndio vipi” alihoji Mkuu huyo wa Mkoa.

Alisema kubadilishwa kwa ramani hiyo hakukuwa kwa nia mbaya bali ilikuwa ni kuongeza chumba kimoja tu katika jengo hilo kwa ajili ya kutumiwa na mwakilishi lakini bahati mbaya wenzao wamewakatalia kubadilisha chochote katika michoro ya mwanzo waliopewa na bunge.

Mkuu wa Mkoa aliyesema hayo kufuatia Waziri kusema kwamba kuwepo kwa mashirkiano kati ya mbunge na mwakilishi katika matumizi ya nyumba hizo wakati serikali ikilifuatilia suala hilo kwa karibu la kuwapatia wawakilishi nyumba zao.

“Mjumbe nimefurahi kujua kuwa tuna mashirikiano mazuri katika serikali zetu mbili seriakli ya mapinduzi Zanzibar na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania” alisema Waziri huyo.

Waziri huyo aliwaambia wajumbe hao kwamba serikali zote mbili zitashirikiana kwa karibu katika kuleta maendeleo ya wananchi wake kwa kuzingatia ukweli huo serikali ya mapinduzi Zanzibar itaendelea kushirikiana na serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania ili kuleta ufanisi katika suala hilo kwa kadiri itakavyowezekana.

SOURCE: ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
 
Kuna mwandishi mmoja wa habari zanzibar aliwahi kuandika makala katika gazeti moja la kila siku akihoji kama viongozi wa serikali zetu, yumkini na wanasiasa kama wanajuwa vipaombele vya taifa, yaani hawa wawakilishi kuna shule ngapi hazina madawati ya wanafunzi na ofisi za walimu seuze nyumba, walimu wanakwenda makazini kwa usafiri wa ajabu, kwa macho yangu nimeshawashuhudia walimu wa shule ya kibele mkoa wa kusini Unguja, wakipanda magari ya mawe, mchanga, kokoto na kuni wakija na kurudi kutoka shuleni hapo. Zahanati ngapi za vijijini huko zipo katika hali mbaya na nyengine zimefungwa kabisa na kugeuzwa mabanda ya mifugo...hakuna hatua zozote zinazochukuliwa,leo wawakilishi wanataka wajengewe nyumba za ofisi!
Yaani mjengo mpya wa BLW kule Chukwani unaotarajiwa kumalizika karibuni tokea hapo hakuzingatia walau kuwa na afisi za wawakilishi kwa nia ya kuwawezesha kufanya kazi zao hapo, wwakilishi waache kujifanya "wateule maalumu" kuwa vipaombele vyengine kujifanya wamevisahau na kukimbilia mambo kama ya kianasaanasa hivi ambayo hayaathiri sana utendaji wa kazi zao kama yatacheleweshwa.
 
wao wameoana hicho ndio kipaumbele chao, kuliko shule wanajali maisha yao zaidi
 
jamani, hata wa Tumbatu ambaye anawakilisha around 1000 people,na sehemu ambayo haina hata gari na yeye anataka??? anyway, me nadhani tuwe na busara kwa ajili ya maendeleo, Unguja iwe na majimbo matatu tu, Pemba iwe na mawili..utitiri na msururu wa Wabunge na Wawakilishi unaongeza zigo la kiuchumi na mifarakano ya kisiasa.....ikibidi alichosema Mh. Pinda kifanyiwe kazi, muungano ufe, Unguja na Pemba ziwe mikoa tu....
 
jamani, hata wa Tumbatu ambaye anawakilisha around 1000 people,na sehemu ambayo haina hata gari na yeye anataka??? anyway, me nadhani tuwe na busara kwa ajili ya maendeleo, Unguja iwe na majimbo matatu tu, Pemba iwe na mawili..utitiri na msururu wa Wabunge na Wawakilishi unaongeza zigo la kiuchumi na mifarakano ya kisiasa.....ikibidi alichosema Mh. Pinda kifanyiwe kazi, muungano ufe, Unguja na Pemba ziwe mikoa tu....
A yuu siriasi?
 
jamani, hata wa Tumbatu ambaye anawakilisha around 1000 people,na sehemu ambayo haina hata gari na yeye anataka??? anyway, me nadhani tuwe na busara kwa ajili ya maendeleo, Unguja iwe na majimbo matatu tu, Pemba iwe na mawili..utitiri na msururu wa Wabunge na Wawakilishi unaongeza zigo la kiuchumi na mifarakano ya kisiasa.....ikibidi alichosema Mh. Pinda kifanyiwe kazi, muungano ufe, Unguja na Pemba ziwe mikoa tu....



Unaonaje tukawa na mawaziri tu bila Bunge? Nafikiri millioni 12 mara kama miatatu wanzolipwa wabunge kwamwezi zitatusaidia sana kuliko uwanja ule wa mapambano eti ufisadi vs wapiganaji. Unaonaje hilo kuliko Zanzibar kuwa na wawakilishi watano tu, kama lengo ni kujali matumizi?
 
Bongo politics imepewa kipaumbele sana! Kila mtu ni mwanasiasi. Wanasiasi wanataka kulipwa kuliko kazi wafanyayo. Inaudhi kweli. Tukiongelea hizi commission za kwenye mikutano ya kipuuzi, ndo watu wanasema ni haki yao. Ujinga mwingi! Sirudi ng'oo
 
jamani, hata wa Tumbatu ambaye anawakilisha around 1000 people,na sehemu ambayo haina hata gari na yeye anataka??? anyway, me nadhani tuwe na busara kwa ajili ya maendeleo, Unguja iwe na majimbo matatu tu, Pemba iwe na mawili..utitiri na msururu wa Wabunge na Wawakilishi unaongeza zigo la kiuchumi na mifarakano ya kisiasa.....ikibidi alichosema Mh. Pinda kifanyiwe kazi, muungano ufe, Unguja na Pemba ziwe mikoa tu....

Too late....wewe na Pinda mtabakia na ndoto yenu hiyo ya abunuasi...Kwanini usiseme muungano uvunjike Zenji iwe kivyake na Tanganyika iwe kivyake?Yaonekana Tanganyika haiwezi kujiendesha bila ya Zenji he?
 
MrFroasty,Zanzibar haiwezikuwa nchi kamwe,labda useme Unguja na Pemba ziwe nchi independently......honestly speaking, chuki kati ya Wapemba na Wazanzibar ni zaidi ya siasa...
 
Back
Top Bottom