Mazingira yanaathari kubwa kwenye haya malezi! Tusiwalaumu sana hawa vijana kabla ya kujiangalia sisi wazazi tunaplay role gani kwenye malezi yao!
Hapa tuko tunajisifu jinsi tulivyokuwa lakini tunasahau kuwa tulikuwa vile kwa sababu ni wazazi wetu ndio waliotufanya tuwe vile, sio sisi wenyewe. Sasa utakuta sisi wazazi wa kiume tukitoka kazini ni moja kwa moja kwenye TV au laptop (kuperuzi JF), hatuwapi watoto wetu muda wa kuongea nao, sasa utakuta dogo anakimbilia kwa mama kwa sababu anampa muda wa kumsikiliza.
Angalau miaka yetu tulikuwa na kazi kama za shamba, bustani, nk ambazo tungeweza kuambatana na baba zetu huku tunaona jinsi wanavyofanya mabo yao, siku hizi mambo yote ofisini, huwezi kwenda na mtoto, tukitoka tunawaacha nyumbani, lini atajifunza uanaume?
Kuna mwanafalsafa kasema 'If your child needs a role model and you're not it then you're both fukced.'