Wavamizi wa madale; god have mercy! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wavamizi wa madale; god have mercy!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bouncer, Sep 10, 2012.

 1. Bouncer

  Bouncer JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Labda kwa ufupi niwaeleze kuhusu hili sakata la huko Madale. Hawa wavamizi bana wakija kwenye eneo lako hawajalishi ulisha liendeleza kwa vipi. Wao wakifika kama ni wewe au ni mlinzi wanampiga mapanga na mkewe na watoto wakiwepo wanabakwa na wanataifisha mali zote wanazokuta hapo kwako.

  Unfortunately ukiripoti kwa polisi Wazo back then kabla ya huyu OCD wa sasa hajaja wanakwambia huko hawawezi kwenda kwani kunahitajika operesheni maalum na wale watu ni wengi na wana silaha za jadi!Hivyo cha kufanya ni kufungua tu RB unakaa nayo ukisubiri hiyo operesheni maalum.

  Hayo yametokea in between 2007-2011, alipokuja huyu OCD mpya ndo yakaanza kupungua. Yule aliekuwepo alidiriki kuweka matangazo Polisi Wazo kuwa hawasikilizi matatizo na migogoro ya ardhi na yeyote mwenye hayo matatizo aende baraza la ardhi. Na tiba kwa waliotaifishwa mali zao ikawa ni kufungua RB tu basi.

  Sasa basi wakisha taifisha hiyo mali yako na kusikia umeenda kwenye baraza la ardhi kufungua kesi, wao wanabomoa any structure uliyo erect kwenye hilo eneo lako na kama una miti wanaikata yote na kama una mifugo wanachinja na kuila yote (kama hawataiuza!) na mwisho wa siku wanaanza kukomaa kwamba wamekuta pori wamelisafisha na kuanzisha makazi!!

  Kibaya zaidi wanatumia yaleyale material kutoka kwenye nyumba zako na miti yako kujengea vibanda vidogo vidogo kuzunguka eneo lako lote. Kama kwamba hiyo haitoshi.. ukionekana tena kwenye hilo eneo lako kama wewe ni mwanamme utatekwa na kupewa kipigo kitakatifu ikiwemo na kupigwa mapanga e.g Mwanasheria wa Manispaa ya kinondoni yaliyomkuta Mr. Mahenge. na kama ni mwanamke utabakwa na virusi wakuachie!

  Kuna familia moja ya baba, mama na mtoto wao wa kike wa miaka 5 walikwenda kwenye eneo lao kama mwezi mmoja uliopita na ukiacha kipigo alichopata baba vile vile walimlawiti mbele ya mkewe na mwanawe na mama akabakwa na mtoto wao wa kike only 5 yrs old alibakwa na hao wavamizi na kuharibiwa kizazi kabisa. God have mercy! Hiyo familia ipo na ukitaka muulize OCD wa Kawe Mr Muroto kwa simu no. +255767190990. Bado wapo hospitali.

  Baada ya hii operesheni hata matukio ya ujambazi na uporaji maeneo ya Tegeta, Boko, Bunju na majirani zao yamepungua sana. Hii ni ripoti ya OCD kawe kwenda kwa wahanga wa uvamizi.

  Kuna mama anaitwa Anna Hangaya au Anna Luvanda aka Mama Makete. Yeye ni mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kinondoni na yeye ndo mfadhili mkuu wa hawa wavamizi. Na analo genge lake la kufanya huu uovu mchana kweupee na nnashangaa ni kwa nini hachukuliwi hatua. Huyu mama ukiacha kwamba ni mvamizi kwenye eneo la mzee Chacha lililopo Nyakasangwe, lenye hati miliki no. 45968. Ni mmiliki wa malori ya kubeba vifusi, kokoto na mawe kama anavyokiri mwenyewe kwenye gazeti la Tanzania Daima la tarehe 3 Sept, 2012 uk. 4.

  Huyu mama na genge lake hilo kwa sasa wamevamia maeneo yote yenye mawe na kifusi huko Nyakalekwa, Nyakasangwe na boko magereza na kwa habari isiyo rasmi ni kwamba anasupply hivyo vifusi na mawe kwenye ujenzi wa barabara ya Mwenge-tegeta. Na hayupo tayari kuyaachia hayo machimbo yanayomsupply materials free of charge.

  Kwenye mkanda wa mauaji ya mabaunsa huyu mama na genge lake hilo anaonekana live akitoa command na kuhamasisha genge lake hilo wawauwe hao mabaunsa angalau hata mmoja siku hiyo. Na kweli mabaunsa wawili walikufa bila hatia yoyote kwani hawakupiga wala kujeruhi mtu yeyote siku hiyo.

  Ngoja niishie hapa ntatupia mkanda wa testimony ya haya niliyoandika midamida.

  Kuna vitu vitatu visivyofichika milele. JUA, MWEZI na UKWELI. by mwanafalsafa flani hivi wa Kichina..
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Haya yanatokea tanzania?!
  Jeshi la polisi liko busy na kuua wandamanaji bila kibaki,hao watakuwa na kibali.
  God have mercy indeed! Mwaka jana nadhani niliona hili sakata kwenye news,alienda mkuu wa wilaya nadhani. Nikajua yaliisha!
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  huyo mwanamama mmiliki genge ni kiongozi wa UWT?
  ndo maana.......
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Kwa swala la falsafa nikuongezee yangu!
  "TABIA YA MUNGU INAFANANA NA TABIA YA MUDA"
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  wana itikadi hiyo eh?
  Kama sophia simba nikimuangalia tu ule wanja wa macho namuogopa!
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  ndo maana yake, kukwapua ni kawaida yao...ila naona siku hizi wameongezea kutoa roho?
  imagine mtu anakuja nyumbani kwako si tu kuwa anakupiga na kukuibia bali anawabaka na kulawiti?
  ila kwa vile yupo kwenye mfumo aaaaaah mnyonge hana haki.....

   
 7. Bouncer

  Bouncer JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Ntaweka na movie clip ya unyama wa hawa wavamizi na testimony ya hiyo familia iliyolawitiwa na kubakwa. Ngoja niipunguze ukubwa. Mtoto wao anavyoeleza machozi lazima yakutoke if you have humanity in you!

   
 8. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  yesu na maria na yosefu
  tanzania hiii hii au ingine?
  Kenyela hajui hili? yewoomiii
  hao walimfanyia huyo baba,mama ,na kabinti kao hawajakamatwa hadi sasa?
  nadhani hao ni raia wa nchi jirani. lol God have mercy.
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Kigogo UWT atajwa uvamizi Kinondoni


  na Betty Kangonga  BAADA ya bomoa bomoa, yameibuka madai kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wilayani Kinondoni, Anna Luvanda ‘Mama Makete' amekuwa akiwatumia wananchi wanyonge kwa maslahi yake binafsi kuvamia maeneo yaliyopo katika wilaya hiyo.


  Agosti 22, mwaka huu Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na vyombo vya dola, ilibomoa nyumba zaidi ya 300 zilizojengwa katika Kata ya Mabwepande na Madale, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kwa madai ya kuvamia eneo hilo.


  Pamoja na hilo, Mama Makete anadaiwa kuwapa pesa kinamama na watoto na kuwapakia katika magari binafsi na kisha kuwatelekeza karibu na ofisi ya Ikulu.


  Akisoma taarifa ya umoja wa watu waliovamiwa maeneo yao jijini Dar es Salaam juzi, katika mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Kituo cha Polisi Kawe, Kaimu Mwenyekiti wa umoja huo, James Mramba, alidai Mama Makete amekuwa akitumia cheo chake kwa maslai binafsi.


  Mramba alidai kuwa Mama Makete aliwakodisha kinamama na watoto wao na kuwalipa ujira mdogo ili wafike katika ofisi za Ikulu waonane na Rais Jakaya Kikwete.


  "Huyu kigogo ndiye chanzo cha vurugu zote za uvamizi wa maeneo katika wilaya hii, amekuwa akiwatumia wanyonge na mbaya zaidi wakati wa bomoa bomoa aliwachukua wanawake na kuwapeleka karibu na Ikulu.


  "Aliwafikisha hapo ili waende wakaeleze kuwa wameonewa na manispaa na waweze kupatiwa maeneo hayo," alidai Kaimu Mwenyekiti huyo.


  Aidha, alidai Mama Makete amekuwa akifadhili wananchi waliovunjiwa maeneo hayo kwa sasa kwa kuwapatia hifadhi katika eneo la machimbo ya kokoto ambako wameweka kambi.


  Alibainisha kuwa, anashindwa kujitokeza hadharani kwa kuwa anajua eneo analomiliki hakulipata kihalali.


  Akichangia katika mkutano huo, Mbunge wa Viti Maalumu, Rita Mlaki (CCM), alisema serikali imeshafanya utafiti wa kina juu ya kuwepo kwa kigogo huyo na ripoti yake imeshafika mezani kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.


  "Hatuna haja ya kulalamika juu ya jambo hilo… ninajua Serikali ya CCM haiwezi kumkubatia mtu kama huyo," alisema.


  Mlaki alidai kwa sasa kuna uhuni unafanywa na wavamizi hao ambapo wanajipanga na kuandaa nyaraka, ili ionekane wazi kuwa maeneo hayo ni mali yao kihalali.


  Huku akikitetea chama chake, Mlaki alidai kuwa CCM haiwezi kukubali kigogo huyo aendelee kukichafua chama hicho, hivyo anaamini hatua zaidi zitachukuliwa kukomesha vitendo hivyo vya kifisadi.


  Hata hivyo, alisema ingawa wavamizi walikimbilia Tume ya Haki za Binadamu, bado wanayo nafasi ya kukutana na kiongozi wa tume hiyo ili kujua undani wa maeneo hayo.


  "Nasi tusimame imara, Tume ya Haki za Binadamu ninawafahamu viongozi wake na tunaweza kwenda kule na tumevumilia vya kutosha kwa kuwa tunaiheshimu serikali maana nasi tulikuwa na uwezo wa kuwa Mungiki," alisema.


  Naye Seif Magugu, alidai kigogo huyo anamiliki machimbo ya kokoto na ndiye mfadhili mkuu wa vijana wanaoendesha vitendo vya kibabe katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.


  Akizungumzia tuhuma hizo, Mama Makete aliziita ni za kisiasa na zina lengo la kumchafua.


  Alifananisha tuhuma hizo na methali ya ‘akutukanaye hakuchagulii tusi' na akasema hawezi kuitumia Ikulu kuendesha vitendo viovu.


  "Mimi nina malori matano na hayo sikai nayo, sasa ni muda upi niliwabeba hao watu na kwenda kuwashusha Ikulu?" alihoji.


  Alisema eneo analodaiwa kuvamia aliuziwa miaka nane iliyopita, hivyo kama kuna mtu ana umiliki halali wa eneo hilo, hana budi kujitokeza.


  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema, Jeshi la Polisi litafuatilia juu ya kuwepo kwa kikundi cha wavamizi kuweka kambi katika eneo la mchimbo ya kokoto.

  Source: Tanzania Daima
   
 10. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huu ni uzushi wa sumaye na wenzake ambao wamekununua ubadili ukweli sema na yule mama aliyezikwa kwenye nyumba yake akiwa hai na watoto wake baada ya bomoabomoa kuamua kumzika hai.....
   
 11. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #11
  Sep 10, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mbunge wenu jina lake nani?
   
 12. Bouncer

  Bouncer JF-Expert Member

  #12
  Sep 10, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Mwanaharakatihuru, kuna vitu viwili inabidi nikueleweshe, kwanza elewa kwamba wakati zoezi la kubomoa linaendelea watu wa LHRC (kituo cha sheria na haki za binadamu) walikua wanakuja kila siku chini ya dada aitwae Leticia na walifungua desk maalum kwa kazi hiyo na waliitolea ripoti, ambayo haikusema kuwepo kwa tukio kama hilo.
  Pili kuna mwandishi wa ITV nimemsahau jina alikuwa anaripoti hilo tukio kila siku na tulikuwa tunaona yanayojiri huko kwenye taarifa za habari na hamna kitu kama hicho kilichoripotiwa. Tatu, kwenye kipindi cha baragumu cha star tv hao wavamizi walipewa airtime ya kutosha na watu wa LHRC nao waliongea kwa kirefu tu na hapo ni baada ya kuisha kwa awamu ya kwanza ya ubomoaji, lakini pamoja na utumbo wooote walioongea hamna aliyesema kuwepo kwa tukio kama hilo.
  My Take:
  Tayari mmeshaua raia mwingine na mwanae na sasa mnataka kuichafua hii operesheni kwa kuibambikizia. Niamini mimi mtuhumiwa wa kwanza kama kweli itathibitika hicho kitu kuwepo ni lazima uwe wewe Mwanaharakatihuru!!

   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Sep 10, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280

  Jakaya Mrisho Kikwete
   
Loading...