Waungwana Wakiahidi, Wanatekeleza!, Rais Samia Aliahidi Kuanza Mchakato wa Katiba Mpya, Ndani ya Siku 100 za Kwanza, Je Atatekeleza?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,101
Reaction score
128,716
Wanabodi

Hii ni makala yangu ya kufungulia mwaka kwenye gazeti la Leo la Mwananchi


Makala hii pia imetoka kwenye gazeti la Nipashe Asante Rais Samia Hotuba Mwaka Mpya, Kubwa Kuliko Yote ni la Kuanza kwa Mchakato wa Katiba Mpya Ndani ya Siku 100, Itawezekana?

Hii ni Makala yangu ya kwanza kwa mwaka huu, 2026, hivyo naomba kuanza kwa kuwatakia heri ya Mwaka Mpya na kumshukuru Mungu kwa kutujalia neema kuuona mwaka.

Nauanza mwaka kwa kuidurusu sehemu ya hotuba ya Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Samia Suluhu Hassan ya kufungia mwaka 2025 aliyoitoa siku ya mkesha wa mwaka mpya, Jumatano iliyopita, kwangu ndio mada ya kuanzia mwaka.

Kwenye hotuba hiyo, kuna vitu vingi muhimu rais Samia amevizungumzia, ila vingine muhimu zaidi, rais Samia hakuvizungumzia, hivyo hii ni makala ya swali kuwa kwa mwaka 2026, kitu muhimu kuliko vyote ni kuanza kwa mchakato wa katiba mpya, ambapo Rais Samia akilihutubia Bunge aliahidi mchakato wa katiba mpya utaanza ndani ya siku 100 za kwanza za awamu hii, lakini kwa vile mambo ni mengi umebaki mwezi mmoja kutimia siku 100 za kwanza je hili la katiba litakuwepo?.

Rais Samia amezungumzia uchumi wa nchi yetu, amesema nchi yetu inaendelea kupiga hatua kubwa za kimaendeleo katika sekta mbalimbali kuboresha maisha ya watu kwa shughuli mbalimbali za maendeleo.

Serikali yetu imekuwa ikiendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha uchumi wa Taifa, ikiwemo kudhibiti mfumuko wa bei hasa bei za bidhaa kikiwemo chakula na pato la taifa kukua kwa asilimia 6% kutoka asilimia 5.2% mwaka 2024 mpaka asilimia 5.8% mwaka 2025.

Hata hivyo ukuaji huu wa uchumi hauakisi uchumi wa mtu mmoja mmoja, hivyo huku mtaani, hali ni ngumu.

Hali hii ya ugumu wa maisha mtaani, inatokana na ukuaji huu wa uchumi umetokana na uwekezaji wa serikali katika miradi mikubwa ya kimkakati ya miundombinu, pamoja na mchango mkubwa wa sekta za madini, ujenzi, na sekta ya fedha na huduma, ikiwemo utalii, ambako karibu kote wakandarasi ni kampuni za kigeni ambazo fedha hizo zinakwenda kurejea makwao badala ya kuingia kwenye mzunguko wetu, uwekezaji wenye mrejesho mkubwa ni kwenye sekta ya kilimo ambayo ndio sekta tegemeo kwa wengi bado sio mkubwa kivile.

Kitu kizuri kuhusu mwaka huu, ni mwaka wa kuanza utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2050, ambapo serikali itaendelea kutekeleza Mkakati wa Muda wa Kati wa miaka mitatu (2026, 2027 na 2028), wa kuongeza mapato ya serikali kwa kuimarisha matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika kukusanya mapato, katika kufanya malipo, na kuongeza umakini katika usimamizi wa fedha na rasilimali za umma, hili ambalo ni jambo jema.

Jambo moja kubwa linalosubiriwa kwa hamu kubwa ni kuanza kwa mchakato wa katiba mpya kama ilivyoelezwa kwenye Dira ya Taifa, na kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo Rais Samia akilihutubia Bunge, alisema mchakato huu utaanza ndani ya siku mia moja (100) za kwanza za awamu hii ambazo zitatimu mwezi Februari mwaka huu, japo kwenye hotuba hii, Rais Samia hakurejelea kuanza kwa mchakato wa katiba mpya ndani ya siku 100 za kwanza, sasa kumeibuka mchakato wa kuundwa kwa tume ya maridhiano, hivyo hili la mchakato wa katiba ndani ya siku 100 za kwanza sijui kama litawezekana, ila katiba mpya ndilo jambo muhimu zaidi kwa taifa letu kwa sasa kuliko jambo jingine lolote.

Si wengi wanakijua chanzo halisi cha zile vurugu za October 29, zilichangiwa na kutokufanyika kwa minimum reforms za katiba ambacho ni kitu kidogo, lakini matokeo yake ndio kile kilichotokea.

Rais Samia ametusisitiza kufanya kazi kwa bidii, mshikamano, na uzalendo, na kutimizwa kwa malengo tuliyojiwekea, kuleta uendelevu wa maendeleo yetu, hivyo serikali itachukua hatua za kimkakati kuweka mazingira rafiki ya kisera, kisheria na kiutendaji yatakayoongeza fursa za biashara, uwekezaji na fursa nyingine za kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa Watanzania wote huku tukiendelea kuvutia wawekezaji kutoka nje ya nchi bila kusahau wajibu wetu wa kulinda rasilimali za nchi ili zitumike kwa manufaa ya Taifa.

Rais Samia amesisitiza uwepo wa utulivu wa kisiasa na hali ya amani na usalama kwa kukumbushia changamoto na mitihani iliyotugusa mwezi Oktoba, kwenye uchaguzi mkuu wetu, amekiri ni tulipitia nyakati ngumu zinazohitaji subira, mshikamano na uzalendo, japo kwa maoni yangu zile vurugu zilikuwa zinaepukika kama serikali yetu ingekuwa sikivu na kusikiliza ushauri.

Rais Samia amevishukuru kwa dhati vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na wananchi wote kwa ujumla, kwa kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Taifa letu. Tumeweza kuuthibitishia ulimwengu kwamba Tanzania ni Taifa imara, himilivu na lenye uwezo wa kushughulikia changamoto zake bila kuingiliwa na mataifa ya nje.

Rais Samia amesisitiza mwaka huu 2026, Serikali imejipanga kujenga umoja wa kitaifa nchini kwa kuunda Tume ya maridhiano ambapo serikali itashirikiana na wadau wote katika kukubaliana kuhusu muundo wa Tume, aina ya wajumbe, majukumu yao, na muda wa kazi wa Tume hiyo ili Watanzania turidhiane, tuwe wamoja, tusonge mbele pamoja.

Rais Samia ametoa rai kwetu sisi Watanzania, tusikubali tofauti zetu za kiitikadi, kiimani, kidini, na kimitizamo zitugawe na kutupotezea malengo yetu ya maendeleo na ustawi wa Taifa letu kwa fahamu kuwa, tofauti ni sehemu ya demokrasia, lakini zisitumike kuligawa Taifa letu la Tanzania.

Rais Samia amerudia msisitizo, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi moja tuu, ndani ya Jamhuri hiyo kuna uraia mmoja tuu, uraia wa Tanzania na Watanzania wote ni watu wamoja ambao wamejengwa na itikadi ya kuamini kwamba Amani, Umoja na Mshikamano hujenga Uzalendo na ndio virutubisho vinavyotuletea maendeleo endelevu na ustawi wa Watanzania.

Mwaka 2026 Tanzania itaendelea kuimarisha na kudumisha ushirikiano wa kimataifa na kikanda. Vilevile, Tanzania itaendelea kutumia Diplomasia ya Uchumi kuvutia uwekezaji, kukuza biashara na kujenga ustawi wa watu wake, sambamba na kusimamia ulinzi wa Taifa na mchango wake katika amani na usalama barani Afrika na Duniani kwa ujumla.

Moja kubwa lililonigusa ni jinsi Rais Samia, alivyozungumzia vifo vilivyotokea mwaka 2025 kwa kusema "Watanzania tumepoteza wapendwa wetu", kauli hii ya kuwaita wote waliotangulia mbele ya haki mwaka 2025 kuwa ni wapendwa wetu ni kauli ya faraja sana, kwa Watanzania wote waliopoteza wapendwa wao, kutoka kwa Mriji Mkuu, haijalishi hao wapendwa walikufa katika mazingira gani, binadamu wote ni sawa na ni wapendwa wetu.

Mungu ibariki Tanzania!
Paskali
 
Huyo Samia ni nani kwanza??

Halafu Samia atawapatiaje watanganyika katiba wanayoitaka ?

Hujui katiba ni mali ya wananchi na wao ndio wataamua wanaitaka iwe vipi .
 
Rubbish
Hizi siku 100 wameanza kusema kitambo

Wewe nawe sijui huwa unatuona hatuna akili! Hii nayo ni habari?

Uchafuzi wa October 29 ufutwe
Katiba - wananchi ndio waamuzi sio yeye
Tume ya uchafuzi ufutwe ndipo tuingie kwenye UCHAGUZI

Simple and clear!
 

Hivi Paskali nyie waandishi wa habari huwa mnafanya FACT CHECK kama wenzetu?

Tanzania vionhoxi huwa wanasema tu kutokana na wakati. Wakati wa kampeni sliahidi pia ataanza mchakato ndani ya siku 100. Sasa imebadilika kuwa ndani ya siku 100 baada ya nwaka mpya ama?

Tangu kampeni zianzebRais amesema mambo mengi tu hasa baada ya MO29. Kati ya hayo mengine amepotosha, amekosea au amesema uongo ( may be bila kudhamilia). Lakini hakuna mwandishi yeyote anayepitia, kusosoa au juhoji zaidi ya kureport tu.

Next time akienda kupokea report ya TUME YAKE anaweza tena kutoa ahadi hiyo hiyo na mkaireport tena bila kuquestion.
 
Pasco, ni lini tumeanza kuhaidiwa kumaliza kero ya maji?
Ni lini tumeanza kuhaidiwa kumaliza kero ya umeme?

Taifa hili ni taifa la ahadi, tuta, tuta, tuna mpango, tutateleleza, tutamaliza. Ndio ahadi zetu hizo.

Huyu mama hawezi kuleta katiba mpya tuwe wakweli na tukue. Huyu mama mpaka miaka yake inaisha atakuwa anapambana tuu na changamoto za uongozi wake. Kuua watu kwa namna ile lilikuwa ni kosa kubwa sana kwa utawala wa huyu mama. Atajikuta miaka mitano anapambana kinyago chake alichochonga mwenyewe.
Hatopata utulivu katika utawala wake kwa damu zile.

Taifa la miaka 60.
 
CCM wahuni tunasubiria Trump atuondolee
 
Hivi Paskali nyie waandishi wa habari huwa mnafanya FACT CHECK kama wenzetu?
Yes tunafanya facts check, na hili ni bandiko la facts check ili kutia shinikizo kuanza kwa mchakato wa katiba mpya ndani ya siku 100 za kwanza za awamu hii
Tanzania viongozi huwa wanasema tu kutokana na wakati. Wakati wa kampeni sliahidi pia ataanza mchakato ndani ya siku 100. Sasa imebadilika kuwa ndani ya siku 100 baada ya nwaka mpya ama?
Hapana, ni siku 100 toka kuapishwa, zinatimia sometimes in February 2026
P
 
Kila kitu hapa ni Just 'stupid!'
Paskali, tafuta namna nyingine ya kupata 'uteuzi.'
 
alipaswa kuahidi kuwa ANGEWAUA WATANZANIA WASIOKUWA HATA NA MAWE MIKONONI NDANI YA SIKU 100 ZA UTAWALA WAKE
Vipi mama huyu atangazwe kuwa ameshinda kwa 98% kisha akaapishwe mbele ya mitutu ya bunduki?
mama huyu, mungu asikie dua za waliouwawa na kupotea huko walipo
 
Hii nchi sio moja wewe mleta mada.

Tuache siasa za kinafiki.

Wapi umeona nchi 1 ina marais 2.

Yule wa Zanzibar sio kama rais wa TFF, ama shirikisho la riadha Tanzania.

Kama wao wanalinda utamaduni wao,wajue hata Tanganyika inahitaji kulinda utamaduni wake.

Wao wanamiliki hadi vitalu vya madini na uwindaji huku bara.

Mbara kumilika arshi tu ya sqm 230 ajipatie kibanda ni nongwa.

Hata kupewa kitambulisha cha Uzanzibari kama upo kule ni shida.

Hiyo kuhusu katiba sahau kabisa.
 
Angeanza na kumtoa Tundu Lissu kwanza Manake ile kesi alopewa ilikuwa ndio njia pekee ya ushindi wake Samia na kukosa mpinzani wa kweli wakati wa kampeni.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…