Waumini wa Serikali Mbili Sasa ni Wakati Wetu wa Kujipanga Kujibu Mapigo The Damage Was Done Today!!

... sisi tusiotaka Serikali 3 mtupe nafasi ya kutusikiliza kama tuliuvyowapa leo,..
Msikilizwe mara ya ngapi? Tayari Jaji Warioba na wajumbe wake waliishapita huku na huku na wakawasikiliza, ndio maana akaleta majumuisho kwenye rasimu ya katiba. Ukumbuke kwamba Jaji Warioba hakuwa anaongea mambo ya upande mmoja jana, alikuwa anaongea ujumla wa mambo ya pande zote, kwa hiyo ndugu yangu ninyi wa serikali mbili mlishasikilizwa!
 
Zama za funika kombe mwanaharamu apite zimepitwa na wakati
Issues sio kujua kujenga hoja au hapana kuhusu Muungano
Issue ni wananchi wanataka nini kuhusu Muungano...........that's democracy
 
- Kaka aemsema yake amesikilizwa sasa ni zamu ya kumjibu, na atajibiwa u know that na Muungano wa Serikali 2 hautakufa, NEVER!! Heshima kwa Demokrasia kwamba leo ameongea namna ya kuuvunja Muungano atajibiwa namna ya kuimarisha Muungano, tatizo lipo wapi kaka yaani wewe ukiwa na mawazo tofauti na yangu nikuite Cameron sasa huo sio ustaraabu na samahani sana kama nimekukwaza kwa kukuita Cameron!!

Le Mutuz
Baada ya maelezo yale ya kina na mazito yaliyotolewa Jaji Warioba kwa niaba ya Tume nilitarajia leo Wajumbe wangepiga kura kuikubali au kuikataa rasimu ile.

Hatua hii ingeokoa sana kodi zetu ambazo zitaendelea kuteketea bure kwa kuwa hakuna jipya watakaloibua kwenye mjadala huu.

Serikali MBILI hazipo siku nyingi na ZANZIBAR hawataki hata kuzisikia. Mtawalazimisha kubadili KATIBA yao? Tayari zipo NCHI MBILI.
 
Nafahamu pia Mzee wetu JSM asivyoiva na Jaji Warioba. Kwa hili la KATIBA MPYA atakuwa anamuunga mkono Jaji Warioba.
 
Hivi leo yule mmasai asiyekuwa na shule alikuwa pale wakati jaji anawasilisha maoni ya watz?teh!

Alikuwepo mkuu,huwa anajifanya mjuaji mbele ya anaodhani anaweza kuwashikia akili zao,lakini mbele ya wenye hekima,busara na elimu iliyoshiba kama kina Warioba anaufyata mkia.Si unaona hata mleta maada leo anaomba usaidizi wa kumjibu Jaji Warioba.
 
- Sasa hivi naelekea Chalinze kwanza so usiwe na wasi wasi subiri Ijumaaa majibu yanakuja hii majibu ya leo ya Kingunge na Kificho ni rasha rasha tu masika yanakuja Ijumaaa!!

Le Mutuz

kwa hiyo unaprove ule msemo wa Raisi wetu ni mtu wa mipasho na tukae kusubiri hiyo Ijumaa kusikia mipasho na siyo "uzinduzi" wa Bunge la Katiba?
 
Malecela kwanza kwa kuanzia kumjibu Warioba soma paper ya Shivji amemjibu warioba na kwa kuanzia ni zile data zake anazodai kuwa wengi wetu tumesema tunataka muungano wa serikali tatu isome vizuri paper ya Shivji. Pitia hapa ujielimishe
https://www.jamiiforums.com/katiba-...e-wa-bunge-la-katiba-someni-ili-msiyumbe.html

Namnukuu hapa ambapo na mie naungana na professor shivji kuwa hoja ya kuwa wengi wametaka kuwepo serikali 3 haina mashiko.
"Pili, ukiangalia kwa makini takwimu zilizotolewa na Tume yenyewe, wala sio sahihi kusema kwamba wananchi walio wengi walitaka serikali tatu. Kwa jumla, waliotoa maoni mbele ya Tume ni watu 351,664 (ang. Jedwali 3, uk. 9 ). Kati ya hao, 47,820 tu (asimilia 14) ndiyo waligusia muundo wa muungano. Asilimia 86 hawakuzungumzia muundo wa muungano kwa maana yoyote - ya serikali moja, mbili, tatu au muungano wa mkataba. Wao walikuwa na mambo tofauti kabisa kuhusu maisha yao. Isitoshe, kati ya waliogusia muundo, asilimia 30 walitaka serikali mbili, asilimia 37 walipendekeza serikali tatu, na asilimia 25 walitaka muungano wa mkataba; asilimia nane walitaka serikali moja.

Kwa hivyo, waliopendekeza serikali tatu ni theluthi moja tu ya waliogusia muundo wa muungano, na ni asilimia 5 tu ya waliotoa maoni. Waliotaka serikali mbili na muungano wa mkataba ni asilimia 55, yaani zaidi ya nusu ya waliotoa maoni juu ya muundo wa muungano. Hata ukichanganya waliotaka serikali moja na serikali mbili ni asilimia 38, inazidi kidogo wale waliotaka serikali tatu. Kwa takwimu hizi za Tume yenyewe, utasema je kwamba serikali tatu ni chaguo la wananchi na ni ‘taswira, dira na ndoto za wananchi’? "
 
- Well, hatimaye ile siku waliyokuwa wanaitafuta kwa muda mrefu wale wote wasaliti wasiotaka Mungano imetimia, sio siri the damage was done today sas wale wote tunaoamini in Serikali 2 huu ni wakati wa kujipanga hatuwezi kumjibu Warioba kiholela holela tukumbuke kwamba amesoma maneno yaliyoandikwa na wenzake wengi wasiotaka Muungano ni haki ya kidemokrasia ya Taifa hili,

- Sasa tujipange na ajibiwe kwa hoja moja baada ya nyingine bila kubabaisha maneno, binafsi nashindwa kuamini kwamba Muungano ndio sababu ya Rais kuamua kurekebisha katiba, maana kama umemsikiliza sana Warioba leo ni Muungano tu ndio waliokuwa wanautafutia maoni, sasa tumemsikia sana, sasa ajibiwe na credible people and then wengine tutafuatia, kilichofanyika leo ni Demokrasia at work, sasa wale waumini wenzake na Warioba naomba na sisi tusiotaka Serikali 3 mtupe nafasi ya kutusikiliza kama tuliuvyowapa leo,

- KWA WALE WENZANGU WOTE TUNAOAMINI IN SERIKALI 2 NI VYEMA SANA LEO HUYU KIONGOZI WAO WA SERIKALI 3 AMEPEWA NAFASI, SASA NI ZAMU YETU TUJIPANGE, OTHERWISE THE DAMAGE WAS DONE LEO SO TUJIPANGE JAMANI WALE WOTE WA SERIKALI 2, TUTASHINDA TU MAANA HISTORIA IPO WAZI HAKUNA MSHINDI ANYEVUNJA MAMBO YA MAZUIR YA WANANCHI, ATAISHIA KUSHINDWA YEYE KWANZA, MUUNGANO WA SEIRIKALI 2 HAUTAKUFA KAMWE, NEVER!!

Le Mutuz

Eti Kikwete anakuja kujibu mapigo ya Warioba. Thubutu! Unadhani Kikwete hana akili? Kwa hiyo sasa hhuyu kikwete unamfananisha na Nape NNauye sasa? Kwa nini mnamdharau sana rais wenu jamani?
Binafsi sidhani km kikwete atakuwa mjinga kiasi hicho. Yeye haoni watu walivyomsifia warioba? kwa hiyo yeye atakuwa anawazungumzia wananchi gani kwa utafiti gani aliofanya?

Kikwete atakuja kuzindua bunge na sana sana atasema wabunge wazingatie maslahi ya Taifa ingawa moyoni huwa hamaanishi hivyo. Hatutugemei kikwete kuja na jipya, labda ashukiwe na roho mtakatifu awe na udhubutu km wa warioba wa kuzungumza ukweli; kwamba ccm tukubaliane na maoni ya wananchi basi. hata watu watamsifu km walivyomsifu warioba. na attacha historia ktk nchi hii. Kinyume cha hapo ataishia kujiabisha tu.
 
Baada ya maelezo yale ya kina na mazito yaliyotolewa Jaji Warioba kwa niaba ya Tume nilitarajia leo Wajumbe wangepiga kura kuikubali au kuikataa rasimu ile.

Hatua hii ingeokoa sana kodi zetu ambazo zitaendelea kuteketea bure kwa kuwa hakuna jipya watakaloibua kwenye mjadala huu.

Serikali MBILI hazipo siku nyingi na ZANZIBAR hawataki hata kuzisikia. Mtawalazimisha kubadili KATIBA yao? Tayari zipo NCHI MBILI.

Ni kweli kabisa. jaji warioba amerahisha sana kazi ya wajumbe. hakuna jipya watakalokuja nalo. Wakiamua kumaliza hii kazi kwa mwezi mmoja tu wanaweza. Warioba amewaprempty wajumbe na sijui kwa hakika watakuja na lipi jipya. Hoja zote za for and against, warioba kaziexhaust zote!
 
Malecela kwanza kwa kuanzia kumjibu Warioba soma paper ya Shivji amemjibu warioba na kwa kuanzia ni zile data zake anazodai kuwa wengi wetu tumesema tunataka muungano wa serikali tatu isome vizuri paper ya Shivji. Pitia hapa ujielimishe
https://www.jamiiforums.com/katiba-...e-wa-bunge-la-katiba-someni-ili-msiyumbe.html

Namnukuu hapa ambapo na mie naungana na professor shivji kuwa hoja ya kuwa wengi wametaka kuwepo serikali 3 haina mashiko.
"Pili, ukiangalia kwa makini takwimu zilizotolewa na Tume yenyewe, wala sio sahihi kusema kwamba wananchi walio wengi walitaka serikali tatu. Kwa jumla, waliotoa maoni mbele ya Tume ni watu 351,664 (ang. Jedwali 3, uk. 9 ). Kati ya hao, 47,820 tu (asimilia 14) ndiyo waligusia muundo wa muungano. Asilimia 86 hawakuzungumzia muundo wa muungano kwa maana yoyote - ya serikali moja, mbili, tatu au muungano wa mkataba. Wao walikuwa na mambo tofauti kabisa kuhusu maisha yao. Isitoshe, kati ya waliogusia muundo, asilimia 30 walitaka serikali mbili, asilimia 37 walipendekeza serikali tatu, na asilimia 25 walitaka muungano wa mkataba; asilimia nane walitaka serikali moja.

Kwa hivyo, waliopendekeza serikali tatu ni theluthi moja tu ya waliogusia muundo wa muungano, na ni asilimia 5 tu ya waliotoa maoni. Waliotaka serikali mbili na muungano wa mkataba ni asilimia 55, yaani zaidi ya nusu ya waliotoa maoni juu ya muundo wa muungano. Hata ukichanganya waliotaka serikali moja na serikali mbili ni asilimia 38, inazidi kidogo wale waliotaka serikali tatu. Kwa takwimu hizi za Tume yenyewe, utasema je kwamba serikali tatu ni chaguo la wananchi na ni ‘taswira, dira na ndoto za wananchi’? "

Mwaka huu, mutaweweseka sana, lakini serikali3 na kwa maana hiyo Tanganyika haviepukiki!
 
Mwaka huu, mutaweweseka sana, lakini serikali3 na kwa maana hiyo Tanganyika haviepukiki!

Hatuforce tunaenda kwa hoja hadi sumu yenu igeuke kuwa maji muyanywe wenyewe!!!! Swali ni kwanini Warioba hakutaka kuzungumzia hawa asilimia 95 ambao hawakugusia muungano wa nchi hii????
 
Malecela kwanza kwa kuanzia kumjibu Warioba soma paper ya Shivji amemjibu warioba na kwa kuanzia ni zile data zake anazodai kuwa wengi wetu tumesema tunataka muungano wa serikali tatu isome vizuri paper ya Shivji. Pitia hapa ujielimishe
https://www.jamiiforums.com/katiba-...e-wa-bunge-la-katiba-someni-ili-msiyumbe.html

Namnukuu hapa ambapo na mie naungana na professor shivji kuwa hoja ya kuwa wengi wametaka kuwepo serikali 3 haina mashiko.

"Pili, ukiangalia kwa makini takwimu zilizotolewa na Tume yenyewe, wala sio sahihi kusema kwamba wananchi walio wengi walitaka serikali tatu. Kwa jumla, waliotoa maoni mbele ya Tume ni watu 351,664 (ang. Jedwali 3, uk. 9 ). Kati ya hao, 47,820 tu (asimilia 14) ndiyo waligusia muundo wa muungano. Asilimia 86 hawakuzungumzia muundo wa muungano kwa maana yoyote - ya serikali moja, mbili, tatu au muungano wa mkataba. Wao walikuwa na mambo tofauti kabisa kuhusu maisha yao. Isitoshe, kati ya waliogusia muundo, asilimia 30 walitaka serikali mbili, asilimia 37 walipendekeza serikali tatu, na asilimia 25 walitaka muungano wa mkataba; asilimia nane walitaka serikali moja.

Kwa hivyo, waliopendekeza serikali tatu ni theluthi moja tu ya waliogusia muundo wa muungano, na ni asilimia 5 tu ya waliotoa maoni. Waliotaka serikali mbili na muungano wa mkataba ni asilimia 55, yaani zaidi ya nusu ya waliotoa maoni juu ya muundo wa muungano. Hata ukichanganya waliotaka serikali moja na serikali mbili ni asilimia 38, inazidi kidogo wale waliotaka serikali tatu. Kwa takwimu hizi za Tume yenyewe, utasema je kwamba serikali tatu ni chaguo la wananchi na ni ‘taswira, dira na ndoto za wananchi'? "

Kwa hiyo prof. Shivji yeye kapendekeza serikali ngapi na namna gani ya kuondoa kero za muungano? Kumbuka pia kwamba hata km hizo data za shivji zingekuwa kweli warioba alisisitiza kwamba hawakufikia uamuzi wa serikali tatu kwa kuangalia tu idadi ya watu waliopendekeza mfumo huo, bali wamezingatia maoni mengi ikiwa ni pamoja na yale yaliyotoka ktk baraza la wawakilishi, ofisi ya makamu wa raisi na, ofisi ya waziri mkuu, bunge la jmt , taasisi mbali mbali za dini. wote hawa wamependekeza serikali tatu. Hapo hujazungumzia mapendekezo yaliyotolewa na tume, na kamati nyingine zaidi ya tano kwamba mfumo unaofaa ni serikali tatu. hapo pia hujaongelea uvunjaji wa katiba uliofanywa na zanz. kwa kubadilisha muundo wa muungano kuwa nchi mbili, serikali mbili, badala ya nchi moja serikali mbili.
Kwa hiyo hoja za shivji kwa sasa hazina mashiko.
 
Kwa hiyo prof. Shivji yeye kapendekeza serikali ngapi na namna gani ya kuondoa kero za muungano? Kumbuka pia kwamba hata km hizo data za shivji zingekuwa kweli warioba alisisitiza kwamba hawakufikia uamuzi wa serikali tatu kwa kuangalia tu idadi ya watu waliopendekeza mfumo huo, bali wamezingatia maoni mengi ikiwa ni pamoja na yale yaliyotoka ktk baraza la wawakilishi, ofisi ya makamu wa raisi na, ofisi ya waziri mkuu, bunge la jmt , taasisi mbali mbali za dini. wote hawa wamependekeza serikali tatu. Hapo hujazungumzia mapendekezo yaliyotolewa na tume, na kamati nyingine zaidi ya tano kwamba mfumo unaofaa ni serikali tatu. hapo pia hujaongelea uvunjaji wa katiba uliofanywa na zanz. kwa kubadilisha muundo wa muungano kuwa nchi mbili, serikali mbili, badala ya nchi moja serikali moja.
Kwa hiyo hoja za shivji kwa sasa hazina mashiko.

Ndugu muundo wowote serikali haukosi mapungufu na faida zake. Usipanic tuliza boli na data alizotoa Shivji ni kutoka katika tanbihi ya hao hao Tume ya Warioba ambao wametumia ujanja kwa kutozungumzia maoni ya wengi wakaamua kuchukua maoni ya wachache na kuyafanya ati ni maoni ya wengi. Kumbuka Warioba alidai ati 60% ya watanzania wanataka serikali 3 sasa tuanzie hapo kuwa hiyo 60% ameitoa wapi???
 
Mkuu Le Mutuz, Hon. Warioba alikuwa anawasilisha maoni ya watanzania wote!!! Wewe mwenzetu una miguu nje ya nchi na Tanzania!!! Tuache sisi wazalendo!!! Na mtu yeyote mwenye akili timamu anaona kabisa kuwa Serikali tatu ni lazima au kama ni mbili basi kila moja ni independent na suala la Muungano lijadiliwe muundo kwa referendum. Muungano uliopo ni makubaliano ya uongozi!!!! Unaweza kunipa maoni ya watanganyika na Wazanzibari ya kabla ya Muungano ambapo waliamua kwa pamoja (majority support) ? It is null and void!!!
 
Ndugu muundo wowote serikali haukosi mapungufu na faida zake. Usipanic tuliza boli na data alizotoa Shivji ni kutoka katika tanbihi ya hao hao Tume ya Warioba ambao wametumia ujanja kwa kutozungumzia maoni ya wengi wakaamua kuchukua maoni ya wachache na kuyafanya ati ni maoni ya wengi. Kumbuka Warioba alidai ati 60% ya watanzania wanataka serikali 3 sasa tuanzie hapo kuwa hiyo 60% ameitoa wapi???

Who is shivj ?
Ni mzalendo kweli wa Tanzania?
Namuona kama anaishi hapa kutokana na Muungano wa Tanganyika na India? Mana nao ni Muungano kama ulivyo wa Zanzibar na Tanganyika,mana India huwezi ukamkuta msambaa akitamba kama shivji kwenye maoni ya kisiasa!!!!Nyerere aliifanya hii nchi kuwa ya kila mtu alimradi asigombee nafasi yake ya urais.
Je, ni tume ipi iliyokua imependekeza maoni ya serikali mbili?Mana inaonekana hata hiyo serikali mbili haikuridhiwa sawasawa na mzee Karume kwani malalamiko mengi yalikua yanaibuliwa na wazanzibar.Sisi waafrika ni watu wa ajabu sana, tuna ubinafsi sana hatuna huruma na vizazi vijavyo; hakuna kijana wa baadae atakayekubali huu muungano wa chako ni changu na changu ni changu mwenyewe.Mking'ang'ania serikali mbili baada ya miaka kumi tutafanya marekebisho tena makubwa ya katiba mana hiki kizazi cha sasa wanaoanza shule na miaka 2 itakua ni vigumu sana kuwadanganya hasa upande wa Tanganyika mana wao ndo wamelala zaidi wakimsubiri Nyerere afufuke awaamulie mustakabali wa nchi yao.Rais Kikwete na Jaji Warioba wataheshimika daima kwa kutimiza wajibu wao.
 
Kama kuna jambo moja ambalo wazanzibari wameungana pamoja kulipigania bila kujali itikadi wala dini ni hili la kuitaka Zanzibar yao iliyo huru. Watanganyika wanapaswa kuiga mfano huo, wa kuungana bila kujali itikadi katika kuitaka Tanganyika yao iliyo huru. Ndipo nchi mbili huru zifanye Jamhuri moja (na serikali yake) yenye nchi mbili (kila moja na serikali yake).

Sasa hivi kuna kituko cha Jamhuri moja (na serikali yake) yenye nchi moja iliyojipambanua (Zanzibar na serikali yake) wakati upande uliobaki haueleweki ni kitu gani.
 
It is high time that the title of Professor of Constitutional Law is bestow upon Judge Joseph Sinde Warioba. His presentation of the proposed constitution in the CA was excellent. Cheers Judge Warioba

And Yet Le Mutuz does not get it by posting this "serekali mbili"rubbish without reasons like its a religion. Makes me wonder if he just borrowed that graduation gown to take a picture for his JF profile. Huwezi kutaka muungano wakati unataka serekali ya zanzibar yenye uhuru kamili. you just can't have it both ways unless you are person with fecal matter between your ears like Le Mutuz
 
- Muungano una matatizo yanatakiwa kurekebishwa sio kuuvunja kwenye Warioba anamsaliti MWalimu, dhambi yake ni mbaya sana itamtesa mpaka mwisho wa maisha yake!!

Le Mutuz

KUREKEBISHWA..!!! Miaka 50 Kaka imepita, matatizo ya muungano yapo tuuu...Wizara nzima imeundwa kurekebisha lakini matatizo bado yapo...na kana kwamba yote hayakutosha Zanzibar wamerekebisha Katiba, Wamefanya Referendum, Imepitishwa na Baraza la Wawakilishi na hatimaye kujitambua kama nchi kamili...viongozi wetu hawakurekebisha...LEO, MKUU NDIO UNATAKA WANANCHI TUAMINI KUWA HUU MUUNGANO UNA NAFASI YA KUREKEBISHA..??

- Warioba alitumwa kukusanya maoni sio kutengeneza maoni kama alivyofanya, ndio maana Ijumaa itakuwa ni siku nzuri sana kwangu maana atapatiwa majibu tena murua sana!! leo yameanza naona vilio tayari vimeanza sasa ijumaa sijui itakuwaje!

- Warioba hawezi kuvunja Muungano na maneno ya ujanja ujanja halafu yeye ni mtu mmoja tu!!

Le Mutuz

Mkuu, mbona hili suala la Muungano mnalifanye ni la MTU/WATU binafsi sana...ghafla wale wote mnaopendelea Serikali Mbili, mnamuona Jaji Warioba peke yake; yeye ndiye alimeandika ile Ripoti nzima? Yaani TUME nzima haikuwepo, Mabilioni yote yaliyotumika ni BURE, Wananchi wote zaidi ya 300,000 walio hojiwa na TUME ni bure isipokuwa CCM TU ambao idadi haifiki hata 300 kwenye Bunge Maalum la Katiba ndio mnataka Watanzania tuamini kuwa maoni yao TU ndio SAHIHI kwa Tanzania..??!!

"Siku Nzuri Kwangu"
Damn Man, you can't be serious??
 
Na ikitokea ''amepatiwa majibu mazito'' na akatoa hotuba ambayo itakua imeangalia muelekeo wa waTanzania waliowengi (akiangalia muelekeo wa upepo) ambao wanaunga mkono serikali tatu (ambazo kiukweli ndizo zitakazo udumisha muungano wa Tanzania), utarudi hapa kutueleza nini? Lets wait and see!!!

Hivi kwanini tuendelee kuudumisha muungano. Kwani unafaida gani. Wazenji washasema wanataka serekali yao yenye uhuru kamili alafu bado munaongelea muungano. Nisawa na kumbembeleza demu akupende wakati unajua akupendi. Na ukizidi kubembeleza atakufanya buzi la kuchuna.
 
Back
Top Bottom