Wauaji walitumia, chai miavuli na hata sumu kuwaangamiza wapinzani

The Certified

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
910
773
Hakuna jambo jipya kuhusu mauaji ya mtu maarufu.

Ni miongoni mwa njia zilizotumika kuwaondoa ulimwenguni watu waliokuwa na uwezo mwingi am watu hatari.

Lakini wauaji wengine walitumia njia za moja kwa moja kwa mfano Julius Caesar alidungwa kisu hadi kufa huku Abraham Lincoln akipigwa risasi.

Hivi sasa kuna uvumi kwamba kifo cha Kim Jong nam -ndugu wa kambo wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un huenda pia aliuawa.

Iwapo hilo limethibitishwa kuwa kweli, basi uvumi umezuka kwamba wanawake wawili waliomuwekea kitambaa cha kujifutia chenye sumu katika mdomo wake alipokuwa akitembea katika uwanja wa ndege mauaji yake yanaorodhshwa miongoni mwa watu wachache waliouawa kupitia njia zisizo za kawaida

Chai ya sumu ya Polonium
Kifo cha Alexander Litvinenko's kinadaiwa kuwa cha mtu maarufu katika miaka ya hivi karibuni.

Jasusi huyo wa Urusi alianza kuugua mnamo tarehe 1 mwezi Novemba 2006, saa chache tu baada ya kunywa chai katika hoteli ya Millenium huko Mayfair pamoja na majasusi wenzake wawili.

Baada ya kifo chake majasusi hao ndio waliokuwa washukiwa wakuu katika kifo chake.
Wakati bwana Litvinenko alipolazwa hospitalini mnamo tarehe 3 mwezi Novemba aliwaambia madaktari amepewa sumu.

Baadaye, alimtaja rais Vladmir Putin akisema ''ndiye aliyesababisha kifo chake''.

Wakati huohuo nywele zake zilianza kuanguka huku viungo vyake vya mwilini vikishindwa kufanya kazi-huku madaktari katika hosptali ya chuo kikuu cha London nchini Uingereza wakishindwa kupata chanzo.

Baadaye ilibainika ni nini kilichomuua kwani wanasayansi bingwa wa Uingereza wanaofanya utafiti wa zana za nyuklia huko Aldermaston walifanikiwa kugundua kwamba tembe ya polonium 210 iliotumika katika bomu la kwanza la nyuklia ndio chanzo cha mauaji hayo.

Hakuna kitu madaktari walichoweza kufanya
Bwana Litvinenko aliambia BBC Urusi kwamba alikuwa akichunguza mauaji ya mwanahabari Anna Politkovskaya mwezi uliopita wakati aliposhambuliwa, Alifariki tarehe 23 mwezi Novemba.

Mwavuli uliowekwa sumu.
Raia wa Bulgaria Georgi Markov alikuwa akisubiri kupanda basi mnamo tarehe 7 mwezi Septemba wakati alipohisi amedungwa kisu katika paja lake.

Bwana Markov mwenye umri wa miaka 49 aliangalia nyuma na kumuona mtu ambaye alikuwa amebeba mwavuli akikimbia na kupanda teksi.

Ni baadaye alipokamilisha kazi yake ya huduma ya BBC nchini Bulgaria aliporudi nyumbani na kuanza kuugua.

Bwana Markov ambaye alikuwa mpinzani wa serikali ya kikomyunisti ya Bulgaria alifariki miaka minne baadaye.

Maafisa baadaye waligundua kwamba aliwekewa sumu ya ricin ambayo ilidaiwa kutiwa katika mwavuli huo.

Hakuna mtu aliyeshtakiwa kwa mauaji yake ikiwa ni mabaya zaidi katika vita baridi, lakini Bwana Markov alisema kuwa anaamini kwamba majasusi wa Urusi KGB walihusika katika shambulio lake.
Dubu aliyebeba shoka.
Jörg Jenatsch alikuwa muhubiri ambaye alibadilika na kuwa mwanasiasa maarufu katika vita vya miaka 30 nchini Switzerland.

Lakini licha ya mafanikio yake yote ni kifo chake mwaka 1639 katika nyumba moja ya kulala huko Chur ambacho kitakumbukwa sana
Bwana Jenatsch, ambaye alikuwa amesifika kwa huduma yake alikuwa katika sherehe wakati kundi moja la watu lilipowasili na kutaka kujiunga nao.

Kiongozi wa kundi hilo alikuwa amevaa kama dubu.

Kundi hilo liliruhusiwa kuingia na dubu huyo ambaye utambulisho wake haukujulikana kabla ya kumkata bwana Jenatsch hadi kufa kwa kutumia shoka.

Inadaiwa kuwa shoka lililotumiwa ndio hilo hilo alilotumia kumuua mpinzani wake.

Chuma cha moto
Zaidi ya miaka 700 huenda imepita tangu mfalme Edward wa pili alipouawa kati mji wa Gloucestershire, lakini bado tunaweza kukumbuka.

Tunachojua ni kwamba mfalme Edward wa pili alikamatwa na kulazimishwa kuwachia ufalme kwa niaba ya mwanawe ambaye alikuwa Edward wa tatu baada ya mkewe Isabella na mpenziwe Roger Mortimer kuvamia Uingereza mwaka 1326.

Edward wa pili baadaye alifungiwa huko Berkeley ambapo alifariki mwaka uliofuatia.
Lakini kulingana na habari zilizopitishwa kutoka kizazi kimoja hadi chengine hakufariki usingizini kama ilivyodaiwa.

Badala yake, habari zinasema kuwa alitiwa chuma cha moto katika tupu yake ya nyuma na hivyobasi kuchoma viungo vyake vya mwili bila kuwacha alama yoyote.

Habari hiyo huenda ilipingwa kuwa uvumi na wanahistoria wengi katika miaka iliofuata, lakini hatua hiyo haijawazuia wengine kuendelea kusambaza habari hiyo.

Njama ilopangwa ikapangika
Mara nyengine hata mipango iliopangwa vizuri inaweza kuharibika.

Na kuna wakati ambapo pia chombo cha usaidizi wakati mpango huo unapofeli kinaweza kufeli. Iwapo hilo linaaminika linaweza kutokea basi hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa watu waliopanga njama za kifo cha Grigory Rasputin 1916.

Inaonekana kuwa watu wachache hawakumpendelea mkulima huyo aliyependwa sana na kuamua kumuua. Lakini baada ya kumpeleka hadi katika jumba la mwanamfalme Felix Yusupov huko St Petersburg mambo yalianza kwenda mrama. Wauaji wake ,mwanamfalme Yusupov na Vladimir Purishkevich, ambaye alikuwa mbunge kwanza walimlisha keki iliokuwa na sumu. Keki hiyo haikumuathiri na hivyobasi wauaji hao wakaamua kutumia bunduki zao. Risasi walizotumia zilishindwa kumuangusha na ngumi zao katika kichwa chake pia hazikufaulu.
  • Je aliuawa vipi?
Iwapo wauaji wake wanafaa kuaminiwa ilichukua risasi nyengine nne kufanikiwa kumuua Rasputin, ijapokuwa uvumi mwengine unasema kuwa walilazimika kumzamisha majini.

Lakini madaktari waliochunguza kifo chake wanasema kuwa alipigwa risasi moja katika tumbo na hivyobasi kupoteza damu nyingi

MWISHO
 
2.jpg
Mauaji ya aliyekuwa jasusi wa Urusi Alexander Litvinenko mwaka 2006 nchini Uingereza huenda yaliidhinishwa na rais Vladimir Putin ,kulingana na uchunguzi.

Bwana Putin huenda alitia saini sumu ya mauaji ya bwana Litvinenko ya polonium-210 kutokana na uhasama kati yao, ulisema uchunguzi.

Mjane wa Bwana Litvinenko,Marina aliunga mkono ripoti hiyo akitaka bwana Putin kuwekewa marufuku ya usafiri huku Urusi ikiwekewa vikwazo.

Hatahivyo waziri wa maswala ya kigeni wa Urusi amesema kuwa uchunguzi huo umeingiliwa kisiasa.

''tunajuta kwamba kesi hiyo ya uhalifu imeingiliwa kisiasa na kuathiri mazingira ya uhusiano wa kibishara''.
Amesema kuwa Uchuguzi huo haukuwa wazi hivyobasi hawakudhania kwamba matokeo yake hayangekuwa na upendeleo.

Bwana Litvinenko alifariki akiwa na umri wa miaka 43 mjini London mwaka 2006,siku kadhaa baada ya kuwekewa sumu.

Alikuwa jasusi wa zamani wa Urusi lakini alitorokea nchini Uingereza ambapo alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Putin.

Mwanadishi wa BBC wa maswala ya usalama Gordon Corera,amesema kuwa kulikuwa na mshangao mkubwa ndani ya mahakama wakati ripoti hiyo ilipotolewa.

Akizungumza nje ya mahakama ya London,bi Litvinenko alisema:Maneno ambayo mume wangu alizungumza katika kitanda chake cha mauti akimshtumu bwana Putin yamethibitishwa na mahakama moja ya Uingereza.
Katika taarifa,bi Litvinenko aliitaka serikali ya Uingereza kuwatimua majasusi wote wa Urusi na kuiwekea Urusi vikwazo vya kiuchumi.

Aliongezea kwamba bado ana matumaini kwamba haki itapatikana kwa wale waliotekeleza kifo hicho.

Katibu wa maswala ya ndani nchini Uingereza Theresa May anatarajiwa kutoa jibu la ripoti hiyo kwa serikali ya Uingereza katika ripoti yake kwa bunge la Uingereza.
 
Hapana chezeya Putin, ni level ingine. Wakati USA inaifanya mbinu za kumwangamiza jasusi wao msaliti Edward Snowden huku Putin yeye anawamaliza maaduhi zake kwa kuwachinja kama kuku.
 
Huwa nawaambia watu hao jamaa (warusi) ni nouma kwenye mambo ya ujasusi, hawabahatishi; bahati mbaya sana huwa hawanielewi!
 
Kwakweli mleta uzi bado haujawa mwandishi anaeweza vuta usikivu wa msomaji, nimesoma nikisikipu sikipu maana ilikuwa haina mvuto

Imekaa kama dondoo za magazeti katika mtandao wa twitter lakin dondoo zisizotoa mshawasha wa kufatilia Habari yote. Jipange zaidi
 
Back
Top Bottom