Wauaji walitumia, chai miavuli na hata sumu kuwaangamiza wapinzani

Kwakweli mleta uzi bado haujawa mwandishi anaeweza vuta usikivu wa msomaji, nimesoma nikisikipu sikipu maana ilikuwa haina mvuto

Imekaa kama dondoo za magazeti katika mtandao wa twitter lakin dondoo zisizotoa mshawasha wa kufatilia Habari yote. Jipange zaidi
Ni tag kwenye hata story moja ulio andika wewe na ikavutia!!! alafu nadhani wewe ni mfata upepo tu hujui hata maana ya hili jukwaa pole sana mkuu
 
Sijaja kushindana ila nimekuja kujifunza na kushare so usinipeleke upande wa mashindano ila Asante
sijakupeleka upande wa mashindano mkuu,mimi nimekupa big up sana kwa hatua uliuoianza,just imagine mimi niko humu JF since 2014 lakini sijawahi anzisha thread hata moja.what I did was a total appreciation mkuu.so, don't get it twisted.sawa mama?
 
Nashukuru sana ila hata wewe ukiamua unaweza ukawa hata zaidi ya ulivyo na mimi lengo langu ni kufanya jukwaa kuwa na Story za aina mbali mbali sio lazima ziwe ndefu na za kusisimua tu ila inaweza kuwa fupi ila ila funzo kubwa.. Nashukuru sana naamini itakuwa poa siku za usoni
 
Ni tag kwenye hata story moja ulio andika wewe na ikavutia!!! alafu nadhani wewe ni mfata upepo tu hujui hata maana ya hili jukwaa pole sana mkuu
Yan nisijue maana ya hili jukwaa kweli? Una akaunti ya mwaka 2016 nna akaunti ya mwaka 2011 na nnayo ya nyuma zaid ya hapo. Ungekuwa unaijua JF vizuri usinge hata uliza post zangu, unge browse to ukaona zote nilizo comment nakuandika kwa kuanzisha binafsi. Ili uwe bora kubali kutolewa kasoro. Karibu tena bibie

-Dumelang
 
Asili yako ni ubishi tu nishakuona ila usingalie kuwa mkongwe ila nyie ndio mnajaza server tu kama uliona kasoro usingehangaika kucomment alafu mimi sio wa 2016 kama unavyo view plof nina ID Za kutosha sana hebu naomba tuache mada zingine tufanye kama uzi unavyosema
 
24c6aed583bfe6b654c420e34a4c31a2.jpg

Kaka wa kambo wa Kiongozi Korea Kaskazini, Kim Jong-un ameuawa nchini Malaysia huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijajulikana.

Kaka huyo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Nam inasemekana muda wake mwingi alikuwa akiutumia nje ya nchi yake ,
Hakuna jambo jipya kuhusu mauaji ya mtu maarufu.Ni miongoni mwa njia zilizotumika kuwaondoa ulimwenguni watu waliokuwa na uwezo mwingi na watu hatari.

Lakini wauaji wengine walitumia njia za moja kwa moja kwa mfano Julius Caesar alidungwa kisu hadi kufa huku Abraham Lincoln akipigwa risasi.

Hivi sasa kuna uvumi kwamba kifo cha Kim Jong nam -ndugu wa kambo wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un huenda pia aliuawa.
Iwapo hilo limethibitishwa kuwa kweli, basi uvumi umezuka kwamba wanawake wawili waliomuwekea kitambaa cha kujifutia chenye sumu katika mdomo wake alipokuwa akitembea katika uwanja wa ndege mauaji yake yanaorodhshwa miongoni mwa watu wachache waliouawa kupitia njia zisizo za kawaida

Chai ya sumu ya Polonium.

eafad223cf8772cb36cbdbd55693dbfe.jpg

Kifo cha Alexander Litvinenko's kinadaiwa kuwa cha mtu maarufu katika miaka ya hivi karibuni.

Jasusi huyo wa Urusi alianza kuugua mnamo tarehe 1 mwezi Novemba 2006, saa chache tu baada ya kunywa chai katika hoteli ya Millenium huko Mayfair pamoja na majasusi wenzake wawili.

Baada ya kifo chake majasusi hao ndio waliokuwa washukiwa wakuu katika kifo chake.

Wakati bwana Litvinenko alipolazwa hospitalini mnamo tarehe 3 mwezi Novemba aliwaambia madaktari amepewa sumu.Baadaye, alimtaja rais Vladmir Putin akisema ''ndiye aliyesababisha kifo chake''.

Wakati huohuo nywele zake zilianza kuanguka huku viungo vyake vya mwilini vikishindwa kufanya kazi-huku madaktari katika hosptali ya chuo kikuu cha London nchini Uingereza wakishindwa kupata chanzo.

Baadaye ilibainika ni nini kilichomuua kwani wanasayansi bingwa wa Uingereza wanaofanya utafiti wa zana za nyuklia huko Aldermaston walifanikiwa kugundua kwamba tembe ya polonium 210 iliotumika katika bomu la kwanza la nyuklia ndio chanzo cha mauaji hayo.Hakuna kitu madaktari walichoweza kufanya.

Bwana Litvinenko alisema kwamba alikuwa akichunguza mauaji ya mwanahabari Anna Politkovskaya mwezi uliopita wakati aliposhambuliwa, Alifariki tarehe 23 mwezi Novemba.

Mwavuli uliowekwa sumu.

Raia wa Bulgaria Georgi Markov alikuwa akisubiri kupanda basi mnamo tarehe 7 mwezi Septemba wakati alipohisi amedungwa kisu katika paja lake.

Bwana Markov mwenye umri wa miaka 49 aliangalia nyuma na kumuona mtu ambaye alikuwa amebeba mwavuli akikimbia na kupanda teksi.

Ni baadaye alipokamilisha kazi yake ya huduma ya BBC nchini Bulgaria aliporudi nyumbani na kuanza kuugua.

Bwana Markov ambaye alikuwa mpinzani wa serikali ya kikomyunisti ya Bulgaria alifariki miaka minne baadaye.

Maafisa baadaye waligundua kwamba aliwekewa sumu ya ricin ambayo ilidaiwa kutiwa katika mwavuli huo.

Hakuna mtu aliyeshtakiwa kwa mauaji yake ikiwa ni mabaya zaidi katika vita baridi, lakini Bwana Markov alisema kuwa anaamini kwamba majasusi wa Urusi KGB walihusika katika shambulio lake.

Dubu aliyebeba shoka.

455b584073573628c0f9de94b81ba900.jpg

Jörg Jenatsch alikuwa muhubiri ambaye alibadilika na kuwa mwanasiasa maarufu katika vita vya miaka 30 nchini Switzerland.

Lakini licha ya mafanikio yake yote ni kifo chake mwaka 1639 katika nyumba moja ya kulala huko Chur ambacho kitakumbukwa sana.

Mwanasiasa huyo aliuawa na mtu aliyekuwa amevalia kama dubu mwaka 1639.

Bwana Jenatsch, ambaye alikuwa amesifika kwa huduma yake alikuwa katika sherehe wakati kundi moja la watu lilipowasili na kutaka kujiunga nao.

Kiongozi wa kundi hilo alikuwa amevaa kama dubu.

Kundi hilo liliruhusiwa kuingia na dubu huyo ambaye utambulisho wake haukujulikana kabla ya kumkata bwana Jenatsch hadi kufa kwa kutumia shoka.

Inadaiwa kuwa shoka lililotumiwa ndio hilo hilo alilotumia kumuua mpinzani wake.

Chuma cha moto.

217269f7e97eed6b53ca77cef32ca0ae.jpg

Zaidi ya miaka 700 huenda imepita tangu mfalme Edward wa pili alipouawa kati mji wa Gloucestershire, lakini bado tunaweza kukumbuka.

Tunachojua ni kwamba mfalme Edward wa pili alikamatwa na kulazimishwa kuwachia ufalme kwa niaba ya mwanawe ambaye alikuwa Edward wa tatu baada ya mkewe Isabella na mpenziwe Roger Mortimer kuvamia Uingereza mwaka 1326.

Edward wa pili baadaye alifungiwa huko Berkeley ambapo alifariki mwaka uliofuatia.

Wana historia wamehoji ni vipi Edward wa pili alifariki.

Lakini kulingana na habari zilizopitishwa kutoka kizazi kimoja hadi chengine hakufariki usingizini kama ilivyodaiwa.

Badala yake, habari zinasema kuwa alitiwa chuma cha moto katika tupu yake ya nyuma na hivyobasi kuchoma viungo vyake vya mwili bila kuwacha alama yoyote.

Habari hiyo huenda ilipingwa kuwa uvumi na wanahistoria wengi katika miaka iliofuata, lakini hatua hiyo haijawazuia wengine kuendelea kusambaza habari hiyo.

Njama ilopangwa ikapangika.

Mara nyengine hata mipango iliopangwa vizuri inaweza kuharibika.

Na kuna wakati ambapo pia chombo cha usaidizi wakati mpango huo unapofeli kinaweza kufeli.

Iwapo hilo linaaminika linaweza kutokea basi hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa watu waliopanga njama za kifo cha Grigory Rasputin 1916.

Inaonekana kuwa watu wachache hawakumpendelea mkulima huyo aliyependwa sana na kuamua kumuua.

Lakini baada ya kumpeleka hadi katika jumba la mwanamfalme Felix Yusupov huko St Petersburg mambo yalianza kwenda mrama.

c99aca689bc5f53f8c1a2c682b5af466.jpg

Grigory Rasputin, raia wa Siberia aliyedaiwa kuwa na nguvu za kuponyesha watu aliuawa 1916
Wauaji wake ,mwanamfalme Yusupov na Vladimir Purishkevich, ambaye alikuwa mbunge kwanza walimlisha keki iliokuwa na sumu.

Keki hiyo haikumuathiri na hivyobasi wauaji hao wakaamua kutumia bunduki zao.

Risasi walizotumia zilishindwa kumuangusha na ngumi zao katika kichwa chake pia hazikufaulu.

Je aliuawa vipi?
Iwapo wauaji wake wanafaa kuaminiwa ilichukua risasi nyengine nne kufanikiwa kumuua Rasputin, ijapokuwa uvumi mwengine unasema kuwa walilazimika kumzamisha majini.

Lakini madaktari waliochunguza kifo chake wanasema kuwa alipigwa risasi moja katika tumbo na hivyobasi kupoteza damu nyingi.
 
What is your target? Unaleta habari hizi kwa mintarafu gani?!! Hauna habari nzuri ya kuwezesha watu kupiga hatua ya maendeleo?!!
Maendeleo huambatana na kutanuka kwa Akili inayojazwa upana wa ufahamu wa mambo kupitia kujuzwa matukio ya mambo mbalimbali ktk nyanja tofauti duniani.Sio kila siku kuzungumzia uvunaji wa mkaa huko Mikese.
 
Hahahahaha kwa uzi huu waalike waje wasome watakuelewa tu Urusi sio watu wa mapenzi Mubashra
Hahaha, Mubashara tena!... Urusi ni wajamaa wale lakini so linapokuja maslahi ya taifa lao wanachora red line ukivuka hiyo line tu basi umechokoza nyuki sasa.

Halafu na Martin Luther King Jr naye aliuawa kikatili pia na hadi leo haijulikani vizuri ni nani aliyetenda unyama ule vipi mtoa mada wajua chochote?
 
Ngoja niutafte uzi nakutag
 
Hakuna jambo jipya kuhusu mauaji ya mtu maarufu.

Ni miongoni mwa njia zilizotumika kuwaondoa ulimwenguni watu waliokuwa na uwezo mwingi am watu hatari.

Lakini wauaji wengine walitumia njia za moja kwa moja kwa mfano Julius Caesar alidungwa kisu hadi kufa huku Abraham Lincoln akipigwa risasi.

Hivi sasa kuna uvumi kwamba kifo cha Kim Jong nam -ndugu wa kambo wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un huenda pia aliuawa.

Iwapo hilo limethibitishwa kuwa kweli, basi uvumi umezuka kwamba wanawake wawili waliomuwekea kitambaa cha kujifutia chenye sumu katika mdomo wake alipokuwa akitembea katika uwanja wa ndege mauaji yake yanaorodhshwa miongoni mwa watu wachache waliouawa kupitia njia zisizo za kawaida

Chai ya sumu ya Polonium
Kifo cha Alexander Litvinenko's kinadaiwa kuwa cha mtu maarufu katika miaka ya hivi karibuni.

Jasusi huyo wa Urusi alianza kuugua mnamo tarehe 1 mwezi Novemba 2006, saa chache tu baada ya kunywa chai katika hoteli ya Millenium huko Mayfair pamoja na majasusi wenzake wawili.

Baada ya kifo chake majasusi hao ndio waliokuwa washukiwa wakuu katika kifo chake.
Wakati bwana Litvinenko alipolazwa hospitalini mnamo tarehe 3 mwezi Novemba aliwaambia madaktari amepewa sumu.

Baadaye, alimtaja rais Vladmir Putin akisema ''ndiye aliyesababisha kifo chake''.

Wakati huohuo nywele zake zilianza kuanguka huku viungo vyake vya mwilini vikishindwa kufanya kazi-huku madaktari katika hosptali ya chuo kikuu cha London nchini Uingereza wakishindwa kupata chanzo.

Baadaye ilibainika ni nini kilichomuua kwani wanasayansi bingwa wa Uingereza wanaofanya utafiti wa zana za nyuklia huko Aldermaston walifanikiwa kugundua kwamba tembe ya polonium 210 iliotumika katika bomu la kwanza la nyuklia ndio chanzo cha mauaji hayo.

Hakuna kitu madaktari walichoweza kufanya
Bwana Litvinenko aliambia BBC Urusi kwamba alikuwa akichunguza mauaji ya mwanahabari Anna Politkovskaya mwezi uliopita wakati aliposhambuliwa, Alifariki tarehe 23 mwezi Novemba.

Mwavuli uliowekwa sumu.
Raia wa Bulgaria Georgi Markov alikuwa akisubiri kupanda basi mnamo tarehe 7 mwezi Septemba wakati alipohisi amedungwa kisu katika paja lake.

Bwana Markov mwenye umri wa miaka 49 aliangalia nyuma na kumuona mtu ambaye alikuwa amebeba mwavuli akikimbia na kupanda teksi.

Ni baadaye alipokamilisha kazi yake ya huduma ya BBC nchini Bulgaria aliporudi nyumbani na kuanza kuugua.

Bwana Markov ambaye alikuwa mpinzani wa serikali ya kikomyunisti ya Bulgaria alifariki miaka minne baadaye.

Maafisa baadaye waligundua kwamba aliwekewa sumu ya ricin ambayo ilidaiwa kutiwa katika mwavuli huo.

Hakuna mtu aliyeshtakiwa kwa mauaji yake ikiwa ni mabaya zaidi katika vita baridi, lakini Bwana Markov alisema kuwa anaamini kwamba majasusi wa Urusi KGB walihusika katika shambulio lake.
Dubu aliyebeba shoka.
Jörg Jenatsch alikuwa muhubiri ambaye alibadilika na kuwa mwanasiasa maarufu katika vita vya miaka 30 nchini Switzerland.

Lakini licha ya mafanikio yake yote ni kifo chake mwaka 1639 katika nyumba moja ya kulala huko Chur ambacho kitakumbukwa sana
Bwana Jenatsch, ambaye alikuwa amesifika kwa huduma yake alikuwa katika sherehe wakati kundi moja la watu lilipowasili na kutaka kujiunga nao.

Kiongozi wa kundi hilo alikuwa amevaa kama dubu.

Kundi hilo liliruhusiwa kuingia na dubu huyo ambaye utambulisho wake haukujulikana kabla ya kumkata bwana Jenatsch hadi kufa kwa kutumia shoka.

Inadaiwa kuwa shoka lililotumiwa ndio hilo hilo alilotumia kumuua mpinzani wake.

Chuma cha moto
Zaidi ya miaka 700 huenda imepita tangu mfalme Edward wa pili alipouawa kati mji wa Gloucestershire, lakini bado tunaweza kukumbuka.

Tunachojua ni kwamba mfalme Edward wa pili alikamatwa na kulazimishwa kuwachia ufalme kwa niaba ya mwanawe ambaye alikuwa Edward wa tatu baada ya mkewe Isabella na mpenziwe Roger Mortimer kuvamia Uingereza mwaka 1326.

Edward wa pili baadaye alifungiwa huko Berkeley ambapo alifariki mwaka uliofuatia.
Lakini kulingana na habari zilizopitishwa kutoka kizazi kimoja hadi chengine hakufariki usingizini kama ilivyodaiwa.

Badala yake, habari zinasema kuwa alitiwa chuma cha moto katika tupu yake ya nyuma na hivyobasi kuchoma viungo vyake vya mwili bila kuwacha alama yoyote.

Habari hiyo huenda ilipingwa kuwa uvumi na wanahistoria wengi katika miaka iliofuata, lakini hatua hiyo haijawazuia wengine kuendelea kusambaza habari hiyo.

Njama ilopangwa ikapangika
Mara nyengine hata mipango iliopangwa vizuri inaweza kuharibika.

Na kuna wakati ambapo pia chombo cha usaidizi wakati mpango huo unapofeli kinaweza kufeli. Iwapo hilo linaaminika linaweza kutokea basi hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa watu waliopanga njama za kifo cha Grigory Rasputin 1916.

Inaonekana kuwa watu wachache hawakumpendelea mkulima huyo aliyependwa sana na kuamua kumuua. Lakini baada ya kumpeleka hadi katika jumba la mwanamfalme Felix Yusupov huko St Petersburg mambo yalianza kwenda mrama. Wauaji wake ,mwanamfalme Yusupov na Vladimir Purishkevich, ambaye alikuwa mbunge kwanza walimlisha keki iliokuwa na sumu. Keki hiyo haikumuathiri na hivyobasi wauaji hao wakaamua kutumia bunduki zao. Risasi walizotumia zilishindwa kumuangusha na ngumi zao katika kichwa chake pia hazikufaulu.
  • Je aliuawa vipi?
Iwapo wauaji wake wanafaa kuaminiwa ilichukua risasi nyengine nne kufanikiwa kumuua Rasputin, ijapokuwa uvumi mwengine unasema kuwa walilazimika kumzamisha majini.

Lakini madaktari waliochunguza kifo chake wanasema kuwa alipigwa risasi moja katika tumbo na hivyobasi kupoteza damu nyingi

MWISHO
Hata muhammad aliwekewa sumu ktk mnofu wa nyama
 
Back
Top Bottom