Wauaji wa Mkuranga, Kibiti na Rufiji, kwanini hawaui wanawake?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,740
2,000
Nianze na hii nukuu ya Mwanajeshi Generali wa China, Sun Tzu ambaye alisema,''If you know the enemy and know yourself, you need not fear the result of a hundred battles. If you know yourself but not the enemy, for every victory gained you will also suffer a defeat. If you know neither the enemy nor yourself, you will succumb in every battle''.

Bila kuwafahamu vizuri wauaji wa maeneo ya Mkoa wa Pwani hatuwezi kuwakamata au kuwashinda.

Wachunguzi wa mauaji katika maeneo ya Mkoa wa pwani lazima waangalie ‘’pattern’’ ya mauaji ili waelewe vizuri aina ya adui wanayepambana naye.

Moja ya ‘’pattern’’ ya wauaji mpaka sasa ni kutoua wanawake, watoto, wagonjwa na wazee wasiojiweza au kuiba mali zao. Hii ni ishara kuu inayoonyesha kwa vyombo vya ulinzi nchini kuwa kuna uwezekano mkubwa vinapambana na kikundi chenye mlengo fulani wa imani kali. Huu mlengo wa imani kali hautofautiani na Boko Haram, Al-Shabab, al-Qaeda na ISIS.

Wenye huu mlengo mkali wa imani wanaamini katika ‘’ doctrine’’ inayosema, ‘’inaruhusiwa katika vita vitakatifu kuua wanaume wote lakini hairuhusiwi kuua wanawake, watoto, wazee na wagonjwa iwapo hautumii mabomu au mauwaji makubwa kwa wakati mmoja (indiscriminate terror attacks or bombardment)’’. Wanawake na watoto wanaruhusiwa kuchukuliwa na kuwa watumwa.

Mpaka sasa katika watu 37 ambao wameuawa ni mwanamke mmoja tu ameuawa na kuuawa kwake kumetokana na shambulio (indiscriminate attack) la polisi wanane ambapo kwa ‘’doctrine’’ yao inaruhusiwa kuua mwanamke katika mazingira hayo (indiscriminate terror attacks).

Wanachofanya kwa sasa ni kutengeneza mazingira ya hofu na woga kwa wananchi wa maeneo hayo lakini kikubwa zaidi ni kuhakikisha hofu na uoga huo unasababisha kusiwepo viongozi wa serikali hasa wanaoshughulika na masuala ya ulinzi.

Kutokuwepo kwa viongozi wanaoshughulika na masuala ya ulinzi katika maeneno hayo kutawapa nafasi ya kuendesha mambo yao bila uoga na kufanya hivyo kutawawezesha kujijenga zaidi ili kutimiza malengo yao kama ilivyo kwa Boko Haram huko Nigeria na al-Shabab huko Somalia.

Kadri muda inavyokwenda ndivyo ambavyo wanapata nguvu ya kujiamini zaidi na katika kujiamini huko wataanza kufanya mauaji ya watu ambao ni ‘high profile’ nchini au sehemu ambayo ni ‘high profile’ kama shopping mall, bunge, ofisi za serikali, etc pindi mauaji yao yatakapokuwa ajenda ya kitaifa katika serikali na vyombo vya habari.

Serikali inatakiwa ifanye kazi kwa weledi lakini kimyakimya. Serikali na vyombo vya habari vinatakiwa vilifanye hili suala kuwa low profile ili wasiwape wauwaji platform ya kuwatangaza kwa sababu moja ya malengo yao ni kupata coverage ili wavutie maghaidi wa kimataifa kama ilivyotokea kwa vikundi vingine vya kigaidi vinavyotambuliwa kimataifa.

Swali la kujiuliza, kwa nini mauaji yanafanyika katika mkoa wa Pwani na hasa katika maeneo ya wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji?

Wataalam wa masuala ya kiuchumi na kigaidi wanakubaliana kuwa Umasikini, ukosefu wa usawa and uhaba wa fursa ni chanzo kikuu cha ugaidi duniani. Kuna uwezekano mkubwa ndivyo ilivyo katika maeneo ya Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji.

Lawama pia ziende kwa serikali kwa kutochukua tahadhari mapema wakati mauaji haya yanaanza na pia kwa kutosikiliza na kufanyia kazi chanzo cha mauaji na malengo ya mauaji.

Wahenga walisema, ‘’hata mbuyu ulianza kama mchicha’’ kwa maana kwamba, hiki kikundi kinaweza kukua zaidi kadri siku zinavyokwenda na tukajikuta kama taifa tunapambana na kikundi chenye nguvu kama Boko Haram, Al-Shabab, al-Qaeda na ISIS.

Serikali haijachelewa katika kukomesha mauaji haya kwa sababu bado yako kwenye hatua ya ‘low profile target’. Kinachotakiwa kwa sasa ni ujasiri, weledi na kujituma kwa kupitia ushirikishwaji wa wananchi wa maeneo hayo.

Unaweza pia kupitia hili andiko langu kuhusu suala la mauwaji mkoani Pwani;
Gonga Link>>Mauaji ya Pwani ni mbinu ya kuwachonga wananchi na serikali
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
39,329
2,000
Msemajiukweli naomba nikuunge mkono kwenye suala la kwamba serekali haijawa makini kwenye haya mauaji. Kwa mfano jana Lowassa amekwenda kuhojiwa, polisi walikuwa wengi mpaka ikawa kero kupita. Sasa tujiulize kama sio jeshi la polisi kugeuka chama cha siasa, kulikuwa na haja gani ya ulinzi wote kwa mtu aliyekwenda mwenyewe bila hata wembe? Ni wapi tulitarajia kuona jeshi la polisi likidhatiti vile kama sio huko kibiti. Awamu hii ya Magufuli kama anavyojinasibisha sio mtu wa siasa mbona hatuoni kwa vitendo anachokisema? Mimi naona yuko kwenye siasa zaidi kuliko anachoongea mdomoni.
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,740
2,000
Wanunue Drones.
ama hayo maeneo yazingirwe na jeshi wawe wanakuja kukutana kila mwanaume anapimwa kama amewahi kushika bunduki. Vifaa hivyo vipo tu vingi Russia. Kama uliwahi kushika bunduki vinaonyesha.
Sidhani hili wazo lako la Drones kama litaleta mafanikio mazuri.

Mwenendo ulivyo, hawa wauaji wako maeneo hayo na wanafahamu vizuri mazingira ya maeneno hayo.

Kuhusu Jeshi, kama una maana ya JWTZ, Sikubaliani na hoja yako ya kupeleka JWTZ kwa sababu adui wa sasa sio 'visible enemy'. JWTZ ni weledi katika kupambana na 'visible enemy' na sio 'invisible enemy'.

Waingereza husema, ''fight fire with fire''. Tunachotakiwa kufanya ni kuwa na wapambanaji ambao pia ni invisible sorders wenye weledi na tekinologia ya kisasa.
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
88,481
2,000
Ninadhani anayefanya vitendo vya mauaji sio mtu mmoja.

Inawezekana wauaji ni serial killer lakini 'pattern' yake inaonyesha ni zaidi ya malengo ya serial killer.

Sawa.

Lakini kutoku-rule out anything mpaka ujue kwa uhakika chanzo ni nini na wahusika ni akina nani ni good law enforcement practice.

Mpaka sasa sidhani hata kama kuna profile ya hao wahalifu.
 

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
7,962
2,000
Sidhani hili wazo lako la Drones kama litaleta mafanikio mazuri.

Mwenendo ulivyo, hawa wauaji wako maeneo hayo na wanafahamu vizuri mazingira ya maeneno hayo.

Kuhusu Jeshi, kama una maana ya JWTZ, Sikubaliani na hoja yako ya kupeleka JWTZ kwa sababu adui wa sasa sio 'visible enemy'. JWTZ ni weledi katika kupambana na 'visible enemy' na sio 'invisible enemy'.

Jeshi JWTZ wanazingira mkoa mzima mzima, harafu wana close in toward each other wakiwa navifaa vya kupima wanaume wote ndani kijiji kwa kijiji kama waliwahi kushika bunduki.

Pili wanakuwa na sapper ambao wana detect hata bunduki iliyofichwa remotetly. Mbona vifaa vingi sana Russia. ni Kazi ya mwezi wanawafinya wote.
Seek and destroy: Russian sappers demine Aleppo
 

Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,585
2,000
"Magaidi wote uliowataja, wanaua kila umri, njisia" Sema mazingira na sababu za mtu anayekuwa kwenye hoja zao inaweza ikakufanya uandike hivyo.

Ila, hao wauaji hawatatenda hivyo daima ni lazima watatiwa tu nguvuni.
 

Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
28,571
2,000
Jeshi JWTZ wanazingira mkoa mzima mzima, harafu wana close in toward each other wakiwa navifaa vya kupima wanaume wote ndani kijiji kwa kijiji kama waliwahi kushika bunduki.

Pili wanakuwa na sapper ambao wana detect hata bunduki iliyofichwa remotetly. Mbona vifaa vingi sana Russia. ni Kazi ya mwezi wanawafinya wote.
Seek and destroy: Russian sappers demine Aleppohata mtu aliyekwenda JKT atashikwa ???
 

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
7,962
2,000
Wakanunue teknolojia mambo ya intelijensia sijui kujipenyeza kwa wananchi nao wauwaji wana intelenjesia yao. Wakiona mgeni anaulizia ulizia wanamtwanga risasi ama huyo anayeulizwa. Wenda wananchi wako terrorized kwa staili hiyo ndo maana hawatoi ushirikiano.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom