Wauaji wa Mkuranga, Kibiti na Rufiji, kwanini hawaui wanawake?

Hawa sio magaidi n majambazi tu pia serikali inafanya kazi usiku na mchana we kaa kimya acha kupost upotoshaji na upuuzi hapa
 
Nawaza ikijatokea huku sumbakalesa sijui itakuaje maana hao waliopo jirani na ikulu wanauawa kila siku serikali iache mzaha nguvu ile ya kushughulikia upinzani ihamishieni pwani huko mnusuru raia hao wanao uawa kikatili bila kosa.
 
lakini unajua kua dini hairuhusu kuua wanawake na watoto? wanafuata mafundisho ya dini, hao nao huwa wanaswali pamoja na kwamba wanaua. na wanaamini wanamtumikia mungu.
 
Listen....kuna aina tatu Wa ADUI...
1.ADUI unae mjua na yeye hakujui....ADUI hyu atakupiga tu hata iweje.

2.ADUI unayemjua na yeye anakujua...hapa ni 50-50tu...timing yeyote yule anaweza kumshinda mwenzake..

3.ADUI unayemjua na yeye hakujui...huyu utampiga tu ...hata awe anamiliki silaha gani....

Sasa angalieni huyo ADUI Wa kibiti hapo....ameangukia namba ngapi ndo mtapata jibu
Maelezo yako nimeishayaeleza kupitia nukuu ya General Sun Tzu.
 
Mkuu hakuna Drone inayo weza kutambua waarifu wakiwa kwenye misitu minene, kumbuka siyo kwamba waarifu/mag.. hawa hawatembei wakiwa kwenye vikundi na wala hawavai sare ya kujitambulisha, sasa camera za Drone zikiona mtu mmoja au wawili, je, waongoza drones hizo wakiwa maofisini wanawezaje kutambua kwamba hao ni waarifu, je mmoja akivaa kiume na anaye fuatana naye kavaa hijabu Drone itatambuaje kwamba kumbe wote ni wanaume? Ngumu.

Mwisho wa siku human intelligence/upelelezi wa kibinadamu ndiyo unaweza kusaidia sana kukomesha matukio hayo - wenyeji wanajua kinacho endelea lakini 4 some reason hawataki kutoa ushirikiano wa kweli kwa vyombo vyetu vya usalama, tusipo kuwa makini matukio haya yanaweza ku-gather momentum tukashindwa ku-deal nayo kikamirifu - we have a choice wenyeji wakikataa kutoa ushirikiano basi wahamishiwe mikoa mingine ya Tanzania ambako wanaweza kudhibitiwa, watakao kahidi na kuendelea kijihusisha na matukio watatamburika kirahisi kwanza silaha watazipata wapi - hawa watu wamepania kutuletea balaa za Somalia, North Nigeria na Syria - miaka kama minne mitano Kenya iliwahi kutupa tahadhali kwamba wamewakamata vijana wanakwenda Somalia kujifunza mambo ya ndiyo sivyo - nani alichukulia seriously tip off ya Serikali ya Kenya??? Hawa watu si wa kawaida hata kidogo.
Ninashukuru kwa angalizo lako.

Kinachotakiwa katika mkoa wa Pwani ni akili kubwa na tekinologia ya kisasa.
 
Hao wanao uwawa kwa bastola...si zimesajiliwa hizo wa kitoa hz risasi katika miili ya marehemu hawawez kujua silaha iliyotumika utumiaji ni nan? Hapo wanaweza kuanzia..kingine interval ya muda toka kifo cha mtu mmoja hadi mwingine pia na maeneo tukio lina fanyika linaweza toa majibu kwamba wako u mbali gani toka hapo na bi usafir gan wanatumia kufika kwenye tukio.
 
Nianze na hii nukuu ya Mwanajeshi Generali wa China, Sun Tzu ambaye alisema,''If you know the enemy and know yourself, you need not fear the result of a hundred battles. If you know yourself but not the enemy, for every victory gained you will also suffer a defeat. If you know neither the enemy nor yourself, you will succumb in every battle''.

Bila kuwafahamu vizuri wauaji wa maeneo ya Mkoa wa Pwani hatuwezi kuwakamata au kuwashinda.

Wachunguzi wa mauaji katika maeneo ya Mkoa wa pwani lazima waangalie ‘’pattern’’ ya mauaji ili waelewe vizuri aina ya adui wanayepambana naye.

Moja ya ‘’pattern’’ ya wauaji mpaka sasa ni kutoua wanawake, watoto, wagonjwa na wazee wasiojiweza au kuiba mali zao. Hii ni ishara kuu inayoonyesha kwa vyombo vya ulinzi nchini kuwa kuna uwezekano mkubwa vinapambana na kikundi chenye mlengo fulani wa imani kali. Huu mlengo wa imani kali hautofautiani na Boko Haram, Al-Shabab, al-Qaeda na ISIS.

Wenye huu mlengo mkali wa imani wanaamini katika ‘’ doctrine’’ inayosema, ‘’inaruhusiwa katika vita vitakatifu kuua wanaume wote lakini hairuhusiwi kuua wanawake, watoto, wazee na wagonjwa iwapo hautumii mabomu au mauwaji makubwa kwa wakati mmoja (indiscriminate terror attacks or bombardment)’’. Wanawake na watoto wanaruhusiwa kuchukuliwa na kuwa watumwa.

Mpaka sasa katika watu 37 ambao wameuawa ni mwanamke mmoja tu ameuawa na kuuawa kwake kumetokana na shambulio (indiscriminate attack) la polisi wanane ambapo kwa ‘’doctrine’’ yao inaruhusiwa kuua mwanamke katika mazingira hayo (indiscriminate terror attacks).

Wanachofanya kwa sasa ni kutengeneza mazingira ya hofu na woga kwa wananchi wa maeneo hayo lakini kikubwa zaidi ni kuhakikisha hofu na uoga huo unasababisha kusiwepo viongozi wa serikali hasa wanaoshughulika na masuala ya ulinzi.

Kutokuwepo kwa viongozi wanaoshughulika na masuala ya ulinzi katika maeneno hayo kutawapa nafasi ya kuendesha mambo yao bila uoga na kufanya hivyo kutawawezesha kujijenga zaidi ili kutimiza malengo yao kama ilivyo kwa Boko Haram huko Nigeria na al-Shabab huko Somalia.

Kadri muda inavyokwenda ndivyo ambavyo wanapata nguvu ya kujiamini zaidi na katika kujiamini huko wataanza kufanya mauaji ya watu ambao ni ‘high profile’ nchini au sehemu ambayo ni ‘high profile’ kama shopping mall, bunge, ofisi za serikali, etc pindi mauaji yao yatakapokuwa ajenda ya kitaifa katika serikali na vyombo vya habari.

Serikali inatakiwa ifanye kazi kwa weledi lakini kimyakimya. Serikali na vyombo vya habari vinatakiwa vilifanye hili suala kuwa low profile ili wasiwape wauwaji platform ya kuwatangaza kwa sababu moja ya malengo yao ni kupata coverage ili wavutie maghaidi wa kimataifa kama ilivyotokea kwa vikundi vingine vya kigaidi vinavyotambuliwa kimataifa.

Swali la kujiuliza, kwa nini mauaji yanafanyika katika mkoa wa Pwani na hasa katika maeneo ya wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji?

Wataalam wa masuala ya kiuchumi na kigaidi wanakubaliana kuwa Umasikini, ukosefu wa usawa and uhaba wa fursa ni chanzo kikuu cha ugaidi duniani. Kuna uwezekano mkubwa ndivyo ilivyo katika maeneo ya Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji.

Lawama pia ziende kwa serikali kwa kutochukua tahadhari mapema wakati mauaji haya yanaanza na pia kwa kutosikiliza na kufanyia kazi chanzo cha mauaji na malengo ya mauaji.

Wahenga walisema, ‘’hata mbuyu ulianza kama mchicha’’ kwa maana kwamba, hiki kikundi kinaweza kukua zaidi kadri siku zinavyokwenda na tukajikuta kama taifa tunapambana na kikundi chenye nguvu kama Boko Haram, Al-Shabab, al-Qaeda na ISIS.

Serikali haijachelewa katika kukomesha mauaji haya kwa sababu bado yako kwenye hatua ya ‘low profile target’. Kinachotakiwa kwa sasa ni ujasiri, weledi na kujituma kwa kupitia ushirikishwaji wa wananchi wa maeneo hayo.

Unaweza pia kupitia hili andiko langu kuhusu suala la mauwaji mkoani Pwani;
Gonga Link>>Mauaji ya Pwani ni mbinu ya kuwachonga wananchi na serikali

Haya maarifa makubwa ambayo umeyatoa hapa nadhani ungeomba tu kuonana na Mamlaka husika hasa Jeshi la Police kupitia kwa IGP wake pengine kuna kitu very constructive ambacho ungekitoa na kingetumika katika kukabiliana na hali tete iliyopo na si ajabu hata kumaliza tatizo lililopo. Ufanyie Kazi huu ushauri wangu Mkuu kwani naamini kuna mengi unayajua na una uzoefu mkubwa na maarifa mapana mno ambayo yanaweza kuleta tija na baadae Tanzania ikakukumbuka kwa Uzalendo wako uliotukuka.
 
Serikali imeachwa nyuma kidogo lakini endeleeni kupandikiza undercover kwa speed.nanyie muwachukue vijana hapohapo muwafundishe wewe undercover.mkichukuwa wa mbali mtachelewa
 
Sidhani hili wazo lako la Drones kama litaleta mafanikio mazuri.

Mwenendo ulivyo, hawa wauaji wako maeneo hayo na wanafahamu vizuri mazingira ya maeneno hayo.

Kuhusu Jeshi, kama una maana ya JWTZ, Sikubaliani na hoja yako ya kupeleka JWTZ kwa sababu adui wa sasa sio 'visible enemy'. JWTZ ni weledi katika kupambana na 'visible enemy' na sio 'invisible enemy'.

Waingereza husema, ''fight fire with fire''. Tunachotakiwa kufanya ni kuwa na wapambanaji ambao pia ni invisible sorders wenye weledi na tekinologia ya kisasa.

Joblee alisema hili jambo muda mrefu sana. Kuna jamaa mmoja alimbishia hadi akaniudhi. SAsa leo aje hapa aombe msamaha kwa Joblee.
 
Mleta mada una akili sana.
Sio mkurupukaji mmoja et anaanza kuhusisha na siasa, yani uwezo wake wa kufikiri mdogo sanaaaa,Hata kindergarten anamzidi.

Hiyo ni pwani wameamua,vipi nchi nzima ikiamua?Dhuluma,uonevu,mabavu,na vitisho vikizidi matokeo yake ni haya.Na watanzania wote sasa wanaumia mioyoni tu,na roho za visasi zimewajaa
 
Nianze na hii nukuu ya Mwanajeshi Generali wa China, Sun Tzu ambaye alisema,''If you know the enemy and know yourself, you need not fear the result of a hundred battles. If you know yourself but not the enemy, for every victory gained you will also suffer a defeat. If you know neither the enemy nor yourself, you will succumb in every battle''.

Bila kuwafahamu vizuri wauaji wa maeneo ya Mkoa wa Pwani hatuwezi kuwakamata au kuwashinda.

Wachunguzi wa mauaji katika maeneo ya Mkoa wa pwani lazima waangalie ‘’pattern’’ ya mauaji ili waelewe vizuri aina ya adui wanayepambana naye.

Moja ya ‘’pattern’’ ya wauaji mpaka sasa ni kutoua wanawake, watoto, wagonjwa na wazee wasiojiweza au kuiba mali zao. Hii ni ishara kuu inayoonyesha kwa vyombo vya ulinzi nchini kuwa kuna uwezekano mkubwa vinapambana na kikundi chenye mlengo fulani wa imani kali. Huu mlengo wa imani kali hautofautiani na Boko Haram, Al-Shabab, al-Qaeda na ISIS.

Wenye huu mlengo mkali wa imani wanaamini katika ‘’ doctrine’’ inayosema, ‘’inaruhusiwa katika vita vitakatifu kuua wanaume wote lakini hairuhusiwi kuua wanawake, watoto, wazee na wagonjwa iwapo hautumii mabomu au mauwaji makubwa kwa wakati mmoja (indiscriminate terror attacks or bombardment)’’. Wanawake na watoto wanaruhusiwa kuchukuliwa na kuwa watumwa.

Mpaka sasa katika watu 37 ambao wameuawa ni mwanamke mmoja tu ameuawa na kuuawa kwake kumetokana na shambulio (indiscriminate attack) la polisi wanane ambapo kwa ‘’doctrine’’ yao inaruhusiwa kuua mwanamke katika mazingira hayo (indiscriminate terror attacks).

Wanachofanya kwa sasa ni kutengeneza mazingira ya hofu na woga kwa wananchi wa maeneo hayo lakini kikubwa zaidi ni kuhakikisha hofu na uoga huo unasababisha kusiwepo viongozi wa serikali hasa wanaoshughulika na masuala ya ulinzi.

Kutokuwepo kwa viongozi wanaoshughulika na masuala ya ulinzi katika maeneno hayo kutawapa nafasi ya kuendesha mambo yao bila uoga na kufanya hivyo kutawawezesha kujijenga zaidi ili kutimiza malengo yao kama ilivyo kwa Boko Haram huko Nigeria na al-Shabab huko Somalia.

Kadri muda inavyokwenda ndivyo ambavyo wanapata nguvu ya kujiamini zaidi na katika kujiamini huko wataanza kufanya mauaji ya watu ambao ni ‘high profile’ nchini au sehemu ambayo ni ‘high profile’ kama shopping mall, bunge, ofisi za serikali, etc pindi mauaji yao yatakapokuwa ajenda ya kitaifa katika serikali na vyombo vya habari.

Serikali inatakiwa ifanye kazi kwa weledi lakini kimyakimya. Serikali na vyombo vya habari vinatakiwa vilifanye hili suala kuwa low profile ili wasiwape wauwaji platform ya kuwatangaza kwa sababu moja ya malengo yao ni kupata coverage ili wavutie maghaidi wa kimataifa kama ilivyotokea kwa vikundi vingine vya kigaidi vinavyotambuliwa kimataifa.

Swali la kujiuliza, kwa nini mauaji yanafanyika katika mkoa wa Pwani na hasa katika maeneo ya wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji?

Wataalam wa masuala ya kiuchumi na kigaidi wanakubaliana kuwa Umasikini, ukosefu wa usawa and uhaba wa fursa ni chanzo kikuu cha ugaidi duniani. Kuna uwezekano mkubwa ndivyo ilivyo katika maeneo ya Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji.

Lawama pia ziende kwa serikali kwa kutochukua tahadhari mapema wakati mauaji haya yanaanza na pia kwa kutosikiliza na kufanyia kazi chanzo cha mauaji na malengo ya mauaji.

Wahenga walisema, ‘’hata mbuyu ulianza kama mchicha’’ kwa maana kwamba, hiki kikundi kinaweza kukua zaidi kadri siku zinavyokwenda na tukajikuta kama taifa tunapambana na kikundi chenye nguvu kama Boko Haram, Al-Shabab, al-Qaeda na ISIS.

Serikali haijachelewa katika kukomesha mauaji haya kwa sababu bado yako kwenye hatua ya ‘low profile target’. Kinachotakiwa kwa sasa ni ujasiri, weledi na kujituma kwa kupitia ushirikishwaji wa wananchi wa maeneo hayo.

Unaweza pia kupitia hili andiko langu kuhusu suala la mauwaji mkoani Pwani;
Gonga Link>>Mauaji ya Pwani ni mbinu ya kuwachonga wananchi na serikali
Maneno meengi, jamaa wanaua viongozi wa serikali na askari (polisi)...basss ! Wala hawajawahi kuua mjeshi !
 
Bora awamu zilizopita zilizoruhusu maandamano na mikutano ya kisiasaa....watu walikuwa na sehemu za kutapikia nyongo zao!!
Huyu hataki maandamano wala mikutano ya kisiasa kwa kisingizio cha kuepusha uvunjifu wa amani...

Sasa nini hiki??? Amani??
Nani alikudanganya chanzo cha ugaidi ni kutokuwa na maandamano na mikutano ya kisiasa?

Huko Europe au Amerika ambao wanahangaika na ugaidi kila siku hawaruhusu maandamano na mikutano ya kisiasa?

Inaniwia vigumu kukubaliana na hoja yako.
 
Imetokea tena!

Wauaji wamefanya ninachokisema!

Wameua mwanamme na kuacha mwanamke!

Low level terrorism!

Sign is ticking!
 
Unaposema Hawaii wanawake,watoto na wazee sijui unamaana wanaume wafuasi wa vyama vingine ukiacha ccm wamo katika kundi la wanawake, watoto na wazee? Kwanini hatutaki kuamini vile vipeperushi vilivyodaiwa kupatikana siku za mwanzo zikiwashutumu polisi na ccm kuhusu uchaguzi uliopita? Kuleta madai ya imani za kidini ni kupotosha kunakoweza usipatikane ufumbuzi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom