Watumishi wanaoacha kazi kipindi hiki cha uhakiki wamulikwe

Ng'wanambula

Senior Member
Oct 2, 2011
197
54
Habarini wana jamvi,

Binafsi naridhishwa na hatua zinazochuliwa na JPM binafsi pamoja na serikali kushughulikia tatizo la watumishi hewa. Hawa wamekuwa chanzo cha watanzania wenye sifa kukosa ajira na pia upotevu wa fedha za umma.
Hata hivyo, kipindi hiki cha uhakiki kuna taarifa za baadhi ya watumishi kuacha kazi ili kukepa kunaswa.

Napenda kutoa taarifa kuwa wengi wa wale wanaoacha kazi ni watumishi waliokuwa na ajira mbili, na serikalini walikuwa wakilipwa mshahara pamoja na kuwa hawaripoti kazini. Hawa waliomba kazi serikalini, wakaajiriwa na kupangiwa kazi lakini wakati huo huo wakawa na ajira sehemu nyingine. Kwa hiyo walikuwa na ajira na mishahara miwili.

Hili limeripotiwa kwenye mikoa ya Shinyanga na Mwanza. Wanaohusika na uhakiki wachukue tahadhari kuhusu wale walioacha kazi hivi karibuni baada ya kusikia kuna uhakiki.

Baadhi ya watumishi wamekuwa wakichukua mishahara kwaa zaidi ya miaka 2, lakini leo wanaacha kazi na kuambiwa kurudisha mshahara mmoja wakati wameiba ka miaka yote hiyo.

Fuatilieni hili hasa Shinyanga manispaa na mtagundua ninachokisema.
 
Back
Top Bottom