Watumishi wa Umma waliotia nia kugombea Ubunge 2020 wakumbukwe kwenye uteuzi wa ma-DAS na ma-DED

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,818
21,425
Wanachama wa CCM walio waajiriwa wa Serikali na wenye sifa za utumishi wa umma na waliogombea nec 2017 na kugombea au kutoa Nia kugombea ubunge kupitia majimbo ninashauri wakumbukwe kwenye uteuzi wa madas na maDED.

Tukumbuke kuwa watumishi hao kwa kipindi cha miezi mitatu walikatwa mishahara yao na walikichagia chama kwa moyo mmoja. Pia watumishi hao ni makada wa chama tena wa muda mrefu. Wakurungenzi waliopo wengi wao ni wachumia tumbo na hawakijali chama Wala hawaijui ilani ya CCM.

Pia, Rais akumbuke kuwa watumishi hao hao mwaka 2025 ndio watakao kipigania na kukifia chama. Ili wahulikane waliko watafutwe Jimbo kwa Jimbo watapatikana.
 
Kuingiza makada kwenye utumishi wa umma hapana, ni kinyume na standing order.Kwa maoni yangu mtumishi wa umma akigombea cheo Cha kisiasa astaafishwe mazima
 
Salaam!!!

Nafasi hizi ni lazima zitumike kwa watumishi wa Umma na isiwe nafasi za kisiasa kama zilizotangulia

Ni kweli kama ikizingatiwa weredi na uzoefu na utumishi uliotukuka basi sheria zitafuatwa maeneo ya kazi na utumishi hivyo kuchochea tija tofauti na awali

Tunaendelea kuomba teuzi za MaDC's juzi tumeziona tumezipokea

Sasa tunaomba kwa nafasi za DED's na DAS's watumishi wa Umma wawekwe wenye sifa bila kujali uchama na upendeleo mwingine mwingine. Hii nchi ni yetu sote lengo liwe ni kujenga na kuwaletea maendeleo wananchi

Natamani kuona watu wenye uzoefu wao na wenye career zilizo makini na zenye mchango wa mustafi wa jamii kupitia utumishi wa umma ndio tuwaone kwenye safu ya mama

With regards!!
 
Tatizo lipo ser

Tatizo mfumo wa utumishi wa umma umeanza kuharibiwa, juzi nimemsikia naibu waziri wa utumishi kwamba Kuna zaidi ya watumishi 1000+ wanakaimu kwenye maofisi ya umma na hawana sifa zaidi ya miaka mitatu, wakuu wa maeneo husika hawapeleki taarifa utumishi, ili wawekwe wenye sifa ingawa wapo.Ni vizuri utumishi wakawa na database ya watumishi wao wote, ili wenye sifa wapewe nafasi
 
Tatizo la nchi yetu kama huna network kwakheri!

Kama huna mtu wa kukusemea imeisha hiyo!!

Kama huna godfather kawasalimie!!!

Hizi sifa za kufikia vigezo vya Ukuu wa Idara ni Usanii hasa kigezo cha DARAJA la mshahara

Maana kazi umefanya weee mwajiri hakupandishi DARAJA kwa wakati unafanyaje?

Maana hata shule unajiendeleza weee kumaliza unaambiwa endelea na kazi zaidi ya kukatwa na bodi hamnapo jipya
 
Hii nchi ni ya wote, Ila ntoa mada ni mbaguzi.
Ina maana watu wa vyama vingine au wasiokuwa na vyama hawapaswi kuteuliwa DED au DAS. Huu ndio ule tunasema kila siku uchama, uchama badala ya utaifa.

Kama taifa no letu sote Basi wote wenye sifa ya kuwa kwenye nafasi hizo wapewe na sio kuangalia sijui chama gani.

Uchaguzi uliopita ukiharibiwa na hii thinking ya uchama na tusipokuwa makini tunaliharibu kabisa hiki taifa kwa Mambo ya uchama. Chadema nao wakija watafanya hivyo hivyo, ACT nao watafanya hivyo hivyo tutakuwa tumekwisha
 
Yaani una ajira halafu utake kukimbilia siasa uangukie pua halafu upewe nafasi nyingine....ilitakiwa wasimamishwe kazi kabisa, mama endelea na mkeka wako wasikupangie 🤣
 
Kuna jamaa yangu anaitwa Mwl Philbert akiiona hii atakuja kutusimulia kijiweni.

Mwl upo K p/s.... Nimeona kwenye simu yako una app ya jf
 
Back
Top Bottom