NUCLEAR BOMB
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 342
- 323
Dawa ya deni ni kulipa. Siku zote kukopa ni harusi kulipa mkopo ni matanga.
Ushauri wangu kwako na wenzako: kachukue mkopo mwingine benki ya biashara, halafu kalipe mkopo wote uliosomea kwa mkupuo mmoja na kubaki na kiasi ambacho utakizalisha kwa kufanya ujasiriamali baada ya saa zako za kazi ya serikali. Utaweza rejesha mkopo wa benki bila matatizo kwa faida utakayopata kwenye huo ujasiria mali. Dhamana ya mkopo benki ni hiyo salary slip yako ya serikali.
Hivyo acha kulalama. Shukuru serikali imekusomesha na imekupa kazi serikalini. Sasa chapa kazi, rudisha mkopo hata kwa mkupuo mmoja ili na vijana wengine waweze nao kupatiwa mkopo wa masomo. Acha kulalama, tumia Akili yako kujipanga. Kumbuka bila huo mkopo hungalisoma maana wazazi wako ni maskini. Shukuru serikali inayoongozwa na ccm kwani hungefika hapo ulipo. Hungeweza hata kupata hiyo laki 5 kwa mwezi unayopokea baada ya makato ya deni la masomo. Sana sana ungekuwa unapata elfu 30 kwa mwezi kwa kufanya kazi za unachinga.
Acha kabisa kukufuru. Hizo laki 5 unazopata kila mwezi uwe unapeleka angalao laki 1 kwa wazazi wako masikini huko kijijini kwenu ili nao waondokane na umaskini. Acha kutumia hela hiyo kwa anasa. Lengo kuu la mikopo hiyo ni kuondoa umasikini kwenye familia masikini za Watanzania kwa kuwasomeshea watoto wao ili waje waondoe umasikini kwenye hizo familia. Halafu hayo makato si indefinate, ni ya muda mchache tu.
Non Sense, vapour,