Watumishi wa umma tumemkosea nini Rais Magufuli?

..halafu linategemea watumishi hao hao wa umma kufanikisha malengo yake...this is ironic to say the least...alafu utasikia yanasema watumishi kuweni wazalendo...my foot!!..uzalendo wafanye wao kwanza kulipa stahiki za watumishi.....
 
Dawa ya deni ni kulipa. Siku zote kukopa ni harusi kulipa mkopo ni matanga.

Ushauri wangu kwako na wenzako: kachukue mkopo mwingine benki ya biashara, halafu kalipe mkopo wote uliosomea kwa mkupuo mmoja na kubaki na kiasi ambacho utakizalisha kwa kufanya ujasiriamali baada ya saa zako za kazi ya serikali. Utaweza rejesha mkopo wa benki bila matatizo kwa faida utakayopata kwenye huo ujasiria mali. Dhamana ya mkopo benki ni hiyo salary slip yako ya serikali.

Hivyo acha kulalama. Shukuru serikali imekusomesha na imekupa kazi serikalini. Sasa chapa kazi, rudisha mkopo hata kwa mkupuo mmoja ili na vijana wengine waweze nao kupatiwa mkopo wa masomo. Acha kulalama, tumia Akili yako kujipanga. Kumbuka bila huo mkopo hungalisoma maana wazazi wako ni maskini. Shukuru serikali inayoongozwa na ccm kwani hungefika hapo ulipo. Hungeweza hata kupata hiyo laki 5 kwa mwezi unayopokea baada ya makato ya deni la masomo. Sana sana ungekuwa unapata elfu 30 kwa mwezi kwa kufanya kazi za unachinga.

Acha kabisa kukufuru. Hizo laki 5 unazopata kila mwezi uwe unapeleka angalao laki 1 kwa wazazi wako masikini huko kijijini kwenu ili nao waondokane na umaskini. Acha kutumia hela hiyo kwa anasa. Lengo kuu la mikopo hiyo ni kuondoa umasikini kwenye familia masikini za Watanzania kwa kuwasomeshea watoto wao ili waje waondoe umasikini kwenye hizo familia. Halafu hayo makato si indefinate, ni ya muda mchache tu.
Hakuna benki inayokopesha mfanyakazi wa serikali anayepokea take home chini ya1/3 ya mshahara wake!
 
Safi sana mh Rais

Nyie watumishi wa umma mlikuwa na viburi sana awamu iliyopita

Hebu fikiria mimi nilienda moja ya ofisi,tulikuwa tumepanga foleni lakini cha ajabu yule mtumishi alituambia tusimsumbue akaingia ndani na kujifungia sijui alikuwa anachati huku siye tukiwa hatuna la kufanya tena asubuhi saa tatu-nne akina mama wapo kwenye foleni wameacha shughuli zao lakini wanajibiwa kidharau halafu huyo mtumishi anajifungia mlango.

Magufuli big up ..washikishe adabu hawa watumishi walikuwa wajeuri sana awamu iliyopita
 
Kazi hamfanyi,kila siku faili halionekani na hakuna anaejali,halafu mnataka nyongeza!badilikeni
Kuongeza makato in kuharakisha Pesa zirudi ili wengine wasome, hiyo 8% mlidhani sadaka,hakuna aliewahi kuuliza mbona sikatwi,
 
Wanapokea zaidi ya laki 5 kwa mwezi hawa vijana baada ya hayo makato kutegemea na fani waliosomea na kazi walizoajiriwa serikalini. Kwa mfano madaktari ni zaidi ya million moja na nusu - starting salary. Tatizo la vijana wa siku hizi wanataka baada ya mwaka mmoja tu wa kuajiriwa wawe wanamiliki gari na wawe wamejenga nyumba na anasa kibao. Ni vijana wa fastjet hivyo akikatwa hiyo 15% anaona inamharibia anasa zake.

Maisha hayaendi hivyo. Enzi za Mwalimu despite kuwa elimu ilikuwa bure, kijana alikuwa akiajiriwa serikalini baada ya masomo yake ya chuo kikuu alikuwa akipokea only 25% ya mshahara wake kwa muda wa miaka miwii, hiyo nyingine ilikuwa ni makato ya jeshi la kujenga taifa(JKT). Yaani miaka miwili ya kwanzaa baada ya masomo alihesabika yuko JKT na kazini alivaa uniform ya JKT. Alipelekwa na kukaa kwanza JKT kwa miezi 3, na miezi 21 aliyoyobaki aliendelea na ajira yake akiwa kwenye combat na akipokea only 25% of his salary!!!
sasa mkuu wew unaona iko sahihi mkuu wetu snachofanya?
 
Mkuu mbona unapata shida sana kumwelewa mkulu?

Yeye alisema mapema kabla hata hajaukwaa,

Nanukuu

"..nitakuwa rais wa wanyonge na masikini.. "

"...nataka muishi kama mashetani.. "
Duh. Saaa tukiishi kama mashetani wotw nani atalipa kodi?
 
Safi sana mh Rais

Nyie watumishi wa umma mlikuwa na viburi sana awamu iliyopita

Hebu fikiria mimi nilienda moja ya ofisi,tulikuwa tumepanga foleni lakini cha ajabu yule mtumishi alituambia tusimsumbue akaingia ndani na kujifungia sijui alikuwa anachati huku siye tukiwa hatuna la kufanya tena asubuhi saa tatu-nne akina mama wapo kwenye foleni wameacha shughuli zao lakini wanajibiwa kidharau halafu huyo mtumishi anajifungia mlango.

Magufuli big up ..washikishe adabu hawa watumishi walikuwa wajeuri sana awamu iliyopita
hujui unachoshabikia unadhani ili ihudumiwe vizr ni lazima nikomolewe?

watumishi wengine tunakuumiza wewe je unajisikiaje umegharimia kwa miaka minne mtoto wako alafu akafeli? wew huna akili kabisa umepata hasara ya maisha ambayo huwezi kufidia milele ndo tunayolalamika huelewi umechangia nini acha ushabiki ndug ysngu
 
Hakuna benki inayokopesha mfanyakazi wa serikali anayepokea take home chini ya1/3 ya mshahara wake!
Siyo kweli. Kwanza hiyo 1/3 ya mshahara umeitoa wapi kwani 15% is not 1/3. Sawa hata kama ni 1/3 ukijumulisha na makato mengine hususani PAYE na NHIF (zote hazifiki 1/3) kama wewe kwa mfano ni daktari ambaye mshahara wake si chini ya 1.5 million hiyo 2/3 itakayobaki ni 1.0 million. Wachini kabisa kwenye fani zingine tunachosema hiyo 2/3 au take home income yake si chini ya laki 5. Sasa kwa nini benki ya biashara ikatae kumkopesha mtu ambaye inauhakuka home income yake ya uhakika is over 5 lakis per month? Zinakopesha hata wale ambao take home income zao ni chini ya hapo. Usitake kudanganya. Benki wanachoangalia cha mhimu ni uwezo wako wa kulipa hicho kiasi cha pesa unazotaka ukope. Halafu kuna tasisi nyingi tu zinazokopesha kama unataka. Na si lazima ukakope na kulipa deni lako la masomo kwa mkupuo. Ishi kwa bajeti hiyo ya take home income na wapelekee kiasi wazazi wako. Baada ya miaka 2 au 3 utakuwa umemaliza hilo deni.

Cha mhimu utakachokopa benki si uende ukanunulia gari la matanuzi au kujenga nyumba ya kuishi. Kaizalishe hiyo hela kwa kuiwekeza kwa ujasiriamali. Usiwe na haraka, gari, nyumba na kadhalika utakujaga kuyapata tu huko mbeleni, tena mazuri zaidi kama utajipanga vizuri. Rome was not built in one day. Karibu kila mtumiIshi wa serikali alianzia maisha kwenye nyumba au chumba cha kupanga na usafiri wa daladala kwa muda si chini ya 10 years kabla ya kupata nyumba na usafiri wake mwenyewe. Kwa nini wewe unataka immediately? Ndiyo maana mnafanya wizi na ufisadi. Lazima mfundishwe kuishi kulingana na kipato.
 
Ulipokuwa unasoma ulikuwa unataka huo mkopo. Asilimia 15% ndio mapovu yote haya. Dawa ya deni ni kulipa na kulimaliza, hii mikopo wengi walikuwa wanapiga danadana. Wacheni longolongo, nchi haiendeshwi kwa mabua.
Elewa hoja sio unakuja na wivu hapa.
Deni lilipwe kwa kuzingatia mkataba uliosainiwa wakati wa makubaliano ya kupata mkopo.
Usiwe mkurupukaji kwa vitu usivyovijua.
Unaelewa madhara ya watu kufanya kazi huku wakiwa hawana furaha?
Hata wewe na familia yako(kama unayo) utaathirika.
Usitumie kichwa chako kutenganishia masikio na kufugia nywele tu, kifikirishe pia.
 
Kazi hamfanyi,kila siku faili halionekani na hakuna anaejali,halafu mnataka nyongeza!badilikeni
Kuongeza makato in kuharakisha Pesa zirudi ili wengine wasome, hiyo 8% mlidhani sadaka,hakuna aliewahi kuuliza mbona sikatwi,
Unadhani makato hayo yataboresha huduma au yatazorotesha kabisa?
 
mwisho wa siku anatakiwa kuonyesha maendeleo ya nchi lakin tunaona uporokaji kuliko hatua ya kwenda mbele je kutukomoa ndo ataendeleza tanzania?
 
Mkulu haeleweki anachokitaka
Anaeleweka mkuu,labda ninyi ndio hamtaki kumuelewa.Anataka Watanzania tubadilike.No longolongo.Tatizo ni kwamba awamu ya pili,ya tatu na ya nne ziliwazoeza WaTZ kuishi beyond their means.Madili yalizidi mkuu. JPM has said no to that nonsense.Sasa mwanzo ni mgumu,ila tutazoea.
 
Anawachukia sababu Mlimpigia kura wakati yeye alikuwa anabeep ...ndio maana I wishi ikuldi bi igp
 
Back
Top Bottom