Watumishi wa umma tumemkosea nini Rais Magufuli?

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,774
2,297
Unajua kuna vitu ktk maisha lazima ujiulize. Tangu rais achukue ofisi ya inchi ana hasira na wafanyakazi. Je tutamwelewaje wakati kuna vitu ni vya kawaida ktk utumishi wa umma mfano stahiki za watumishi ni jambo la msingi sana kuliko kitu kingine mana ndo matumaini yao. Lakini mkuu wa nchi anaona hakuna haja ya kuwapa.

Pili alizingua akijitetea na uhakiki wa watumishi hewa wakasubiri wakavumilia lakini inaonekakana habari hiyo imekuwa story ya zamani

Tatu ikaja ya uhakiki wa vyeti bado watumishi wakaona isiwe tabu lakini habari mwisho wake sijajua imefikia wapi lakini inaonekana imemshinda mana wakubwa wote ni magumashi.

Kubwa ni la mwezi huu wa pili kukata 15% kwa ajili ya wanufaika wa bodi ya mkopo. Hatukatai kulipa deni shida ni kwa nini iwe 15% badala 8%? Hapo ndipo tatizo lilipo lazima watu wajue kwa wazalendo hatukatai kulipa deni la mkopo. Kwanini anatukomoa watumishi? Na kama anataka tanzania ya viwanda na yenye neema ataipata kwa namna hii?

Wakati tunaomba mkopo makubaliano ilikuwa nikipata kazi nikatwe 8% kwa nin aongeze mpaka 15%? kwa hiyo unaona hasira yake kwa watumishi tunajiuliza tumemkosea nini?

Mwisho nchi inajengwa na watumishi wenye ari ya kufanya kazi kwa uwezo wao wote, akili yao yote, na nguvu zao zote. Sikitiko kubwa ni kwamba Rais ana hasira na watumishi wa umma tunajiuliza je malengo yake atafanikiwa kwa kuwa na watumishi ambao hawana raha na furaha moyoni mwao.

Hii post ni kwa wazalendo kweli kweli future ya tanzania imo katika kuhamasishana kupeana moyo, na kifatijiana huku tukikusanya nguvu zetu kwa ajili ya taifa.

Karibuni wadau
 
bwana huyu hana hata ubinadamu kura ni kweli ya moyo wa mtu na imani yake kwako watumishi kama walimkataa walikataa ccm sio yeye ila kuhamisha hasira yote kwa watumishi anatuonea bila kosa kama vp afute vyama vya upinzani
 
Anakusanya pesa kwa kasi atengeneze viwanda
Vumilieni soon mtaishi kama malaika
 
  • Thanks
Reactions: Qj_
Mkuu umeongea kwa machungu sana ila ujue kitu ,roho mbaya ni kansa..
Naipenda sana tanzania mkuu ila jamaa anakatisha tamaa sio kwamba mimi sina tatizo na mshahara wangu sina mkopo unatosha wengine wenzangu wanasikitika sana na kulaani mno
 
Dawa ya deni ni kulipa. Siku zote kukopa ni harusi kulipa mkopo ni matanga.

Ushauri wangu kwako na wenzako: kachukue mkopo mwingine benki ya biashara, halafu kalipe mkopo wote uliosomea kwa mkupuo mmoja na kubaki na kiasi ambacho utakizalisha kwa kufanya ujasiriamali baada ya saa zako za kazi ya serikali. Utaweza rejesha mkopo wa benki bila matatizo kwa faida utakayopata kwenye huo ujasiria mali. Dhamana ya mkopo benki ni hiyo salary slip yako ya serikali.

Hivyo acha kulalama. Shukuru serikali imekusomesha na imekupa kazi serikalini. Sasa chapa kazi, rudisha mkopo hata kwa mkupuo mmoja ili na vijana wengine waweze nao kupatiwa mkopo wa masomo. Acha kulalama, tumia Akili yako kujipanga. Kumbuka bila huo mkopo hungalisoma maana wazazi wako ni maskini. Shukuru serikali inayoongozwa na ccm kwani hungefika hapo ulipo. Hungeweza hata kupata hiyo laki 5 kwa mwezi unayopokea baada ya makato ya deni la masomo. Sana sana ungekuwa unapata elfu 30 kwa mwezi kwa kufanya kazi za unachinga.

Acha kabisa kukufuru. Hizo laki 5 unazopata kila mwezi uwe unapeleka angalao laki 1 kwa wazazi wako masikini huko kijijini kwenu ili nao waondokane na umaskini. Acha kutumia hela hiyo kwa anasa. Lengo kuu la mikopo hiyo ni kuondoa umasikini kwenye familia masikini za Watanzania kwa kuwasomeshea watoto wao ili waje waondoe umasikini kwenye hizo familia. Halafu hayo makato si indefinate, ni ya muda mchache tu.
 
Dawa ya deni ni kulipa. Siku zote kukopa ni harusi kulipa mkopo ni matanga.

Ushauri kachukue mkopo mwingine benki halafu kalipe mkopo wote uliosomea na kubaki na kiasi ambacho utakizalisha kwa kufanya ujasiriamali baada ya saa zako za kazi ya serikali. Utaweza rejesha mkopo wa benki bila matatizo. Dhamana ya mkopo benki ni hiyo salary slip yako ya serikali.

Hivyo acha kulalama. Shukuru serikali imekusomesha na umekupa kazi serikalini. Sasa chapa kazi, rudisha mkopo hata kwa mkupuo mmoja ili na vijana wengine waweze kupatiwa mkopo wa masomo. Acha kulalama, tumia Akili yako kujipanga.
unadhani mtu anayepokea laki moja kwa mwezi alikopa kujenga nyumba yake na huku ana familia atafanyanya kazi kwa ufanisi kweli umetoa utetezi mzuri ila ujue kazi onaendana na moyo wa mtu kuwa furaha kwanza hujampa stahiki zake atakuwaje na hamasa ya yakazi?
 
Mkuu mbona unapata shida sana kumwelewa mkulu?

Yeye alisema mapema kabla hata hajaukwaa,

Nanukuu

"..nitakuwa rais wa wanyonge na masikini.. "

"...nataka muishi kama mashetani.. "


Na kuna clip moja alisema "Mtalimia meno"
 
ccm tutawalaumu kwa matatizo yote tz hampend kuachia mamlaka ila iko hivi mwisho wenu utakuwa mbaya sana kwa kuwa akili hamtumii kwa ajili ya mchi mnatumia kulisha matvo yenu ingawa mmeaniwa
 
haina shida muda utamhukumu kiongozi wetu wala hakuna tatizo ila mjue nchi ni wana wa nchi that is all mwisho wa siku hapo ndo kila kitu je ajira iko wapi? ccm tupeni majibu
 
unadhani mtu anayepokea laki moja kwa mwezi alikopa kujenga nyumba yake na huku ana familia atafanyanya kazi kwa ufanisi kweli umetoa utetezi mzuri ila ujue kazi onaendana na moyo wa mtu kuwa furaha kwanza hujampa stahiki zake atakuwaje na hamasa ya yakazi?
Wanapokea zaidi ya laki 5 kwa mwezi hawa vijana baada ya hayo makato kutegemea na fani waliosomea na kazi walizoajiriwa serikalini. Kwa mfano madaktari ni zaidi ya million moja na nusu - starting salary. Tatizo la vijana wa siku hizi wanataka baada ya mwaka mmoja tu wa kuajiriwa wawe wanamiliki gari na wawe wamejenga nyumba na anasa kibao. Ni vijana wa fastjet hivyo akikatwa hiyo 15% anaona inamharibia anasa zake.

Maisha hayaendi hivyo. Enzi za Mwalimu despite kuwa elimu ilikuwa bure, kijana alikuwa akiajiriwa serikalini baada ya masomo yake ya chuo kikuu alikuwa akipokea only 25% ya mshahara wake kwa muda wa miaka miwii, hiyo nyingine ilikuwa ni makato ya jeshi la kujenga taifa(JKT). Yaani miaka miwili ya kwanzaa baada ya masomo alihesabika yuko JKT na kazini alivaa uniform ya JKT. Alipelekwa na kukaa kwanza JKT kwa miezi 3, na miezi 21 aliyoyobaki aliendelea na ajira yake akiwa kwenye combat na akipokea only 25% of his salary!!!
 
Back
Top Bottom