OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,066
- 114,553
Pamoja na changamoto za maslahi na vitendea kazi lakini watumishi wa umma tulikuwa tumezidi.Nadhani ndio maana hata vyama vya wafanyakaizi vinapata kigugumizi kupigania maslahi ya wafanyakazi kwa kuwa wanajua wengi wa wanachama wao ni SIFURI.
1. Kulikuwa na utamaduni kwamba ukiajiriwa serikali imetoka mpaka kustaafu au kufariki bila kujali utendaji wako
2. Kuna watu ambao ilikuwa ukifuatilia mienendo yao ofisi za umma ni ya ajabu sana.Kwanza anafika ofisini saa tatu asubuhi badala ya saa 1.30, akifika asubuhi anaanza kupita maofisi kukusanya ubuyu(umbea na stori za majungu), ikifika saa tano anaenda chai na saa 8 lunch na ikifika saa 9 ndo anajifanya kuwa bize sana, hapo atazingua mpaka saa 10:30 anatafuta posho ya masaa ya ziada
3. Kuna idara kwa mfano maafisa Maendeleo ya jamii na maafisa utamaduni, hawa watu waliweza kudoji kazini hata wiki hakuna wa kufuatilia.
4. Kuna watu walikuwa wazembe balaa, ukimpa kazi jumatatu na ukamtaka akupe ripoti jumatano hiyo kazi ataanza kuifanya jumatano…….jumatatu na jumanne utamuona anazunguka tu ofisini mara huku na huko na vikao vya malalamiko
5. Kuna mtumishi utamuona kimya nyuma ya keyboard ukidhani anafanya kazi za ofisi,thubutu anafanya kazi binafsi na mitandaoni.
6. Matumizi ya simu za ofisi yalikuwa yanatia kinyaa. Unakuta PS anaongea na simu binafsi kutwa. Full kilugha kwenye simu ya ofisi.Mwisho wa mwezi bili laki tano.
7. Kuna mabosi walikuwa wazembe jamani, wakikuwa wanatelekeza kazi kwa watu wa chini, yeye yuko bize na miradi yake. Kazi hafanyi ila kwenye vikao vya posho humkosi.Anawasilisha ripoti ambayo hata haifanhamu vizuri kwa sababu hajaifanyia kazi wala kuipitia.
8. Bosi anageuza gari ya ofisi kama roli la nyumbani. Asubuhi inapeleka watoto shule. Jioni unalikuta baa.Wikend kubeba mikaa toka nje ya mji. Jumapili unaweza kulikuta limebeba wanakwaya.
9. Kutokana na kutofanya mambo kwa wakati ilisababisha wawe waoga sana wanapokuja kukaguzi wa wakaguzi wa nje. Mtumishi anamuona mkaguzi kama Mungu mtu mpaka kero.Hii ilisababisha sana kwa wakaguzi wasio na maadili kuvuta mshiko kwa wakuu wa idara wazembe……..maana mkuu anazileta mwenyewe bila shuruti.
MY TAKE
Magufuli umeshakaza inatosha, tuongezee maslahi Mkuu Rais, tunadhalilika mwaka huu.