Watumishi wa umma sasa kufanya mazoezi mara moja kila wiki

Jaluo_Nyeupe

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
2,697
1,962
Watumishi wa Umma wametakiwa kufanya mazoezi ya viungo Mara moja kwa wiki ili kujiepusha na magonjwa yasioambukiza ili kujenga watumishi wenye afya imara kwa maendeleo ya taifa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa magonjwa yasioambukiza (NCD) Prof. Ayoub Magimba wakati wa kufunga mkutano Wa siku tatu wa Madaktari na wadau wa afya ngazi ya Mkoa na wilaya katika kupata mpango mkakati wa kujikinga na magonjwa yasioambukiza uliofanyika mkoani Morogoro.

“Katika mkutano huu wa kupata mpango mkakati wa kujikinga na magonjwa yasioambukiza tumeazimia kua na Sera inayoelekeza watumishi wote wa Umma wafanye mazoezi ya viungo siku moja kwa wiki ikiwa ni sehemu ya majukumu yao”alisema Prof. Magimba.

Aidha Prof. Magimba amesema kuwa mazoezi hayo ni sehemu ya majukumu ya watumishi wa umma ili kuwasaidia wale wanaokosa muda wa kufanya mazoezi majumbani kwao ili kujikinga na magonjwa hayo.

Mbali na hayo Prof. Magimba amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuepuka matumizi ya Mara kwa mara ya Sigara na vileo kwa pamoja na badala yake wajikite kwenye mazoezi na utumiaji wa vyakula asilia.

Kwa upande wake Daktari bingwa Wa magonjwa ya ndani Dkt. Meshack Shimwela ambaye ni mshiriki wa mkutano huo amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuzingatia na utekelezaji wa Sheria za barabarani ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na ajali mpaka kufikia mwaka 2030.

Source: Mtembezi
 
“Katika mkutano huu wa kupata mpango mkakati wa kujikinga na magonjwa yasioambukiza tumeazimia kua na Sera inayoelekeza watumishi wote wa Umma wafanye mazoezi ya viungo siku moja kwa wiki ikiwa ni sehemu ya majukumu yao”alisema Prof. Magimba


Wafanyie wapi? Saa ngapi? Je kama ni katika mazingira ya kazi, watajenga mabafu? watatoa sabuni, mataulo? hatupingi ila waweke mipango yenye mashiko na siyo kutoa matamko tata, itakuwa ni matumizi mabaya ya rasilimali za taifa
 
Wengine hizo mambo ni hobby zetu,daily asubuhi lazima niamshe,kibaka akijichanganya kwangu nitamkimbiza kutoka Dar-Chalinze tutafika na mwendo wa speed kali na sio ya kunyata Kama kinyonga
..
 
Hebu watuache sasa tupumuwe! Mbona tunapiga sana bed tennis kwani hiyo haitoshi kutuweka fit?
 
basi hapo utasikia makondo anakurupuka na agizo la mchakamchaka kwa watumishi kila ijumaa
 
basi hapo utasikia makondo anakurupuka na agizo la mchakamchaka kwa watumishi kila ijumaa
Hahahhaaa! Ila sio mbaya. Sijawahi kumuona Daktari anakataza mazoezi. Labda kama kuna sababu maalum za kiafya. Hivyo ni jambo jema tu ikibidi iwe sheria ya nchi kila wiki mara moja wajumbe wawe na madaftari ya wahudhuriaji.
 
pia kula tusile mchana watumishi wa umma.yani unakuta umekula wali maharage ni kusinzia tu ofisini .kazi haiendi.yani ata kunyanyua kalamu unaona kama unanyanyua mfuko wa cement
 
pia kula tusile mchana watumishi wa umma.yani unakuta umekula wali maharage ni kusinzia tu ofisini .kazi haiendi.yani ata kunyanyua kalamu unaona kama unanyanyua mfuko wa cement
Hahahaa si ubadili chakula mkuu! Nadhani kumbi za mikutano zitafaa sana kufanya mazoezi ya cardio.
 
Back
Top Bottom