Kwa huzuni kabisa tuna hawa ndg zetu waliokua watumishi wa umma kabla hawajasitishiwa ajira na mishahara pia.hawa watumishi waliajiriwa na serikali hihii ya CCM. Kwa vigezo na sifa zote ,kwani wasingekua na hizo sifa wasingeajiriwa .waliajiriwa wakadhibitishwa kazini uwepo wao na barua ya ajira ya kudumu ,hadi chech no .walikua Nazo ajabu likatokea tamko ghafla kama msiba eti wale wote walio na elimu ya darasa LA saba waliopata ajira baada ya mei 20 watasitishiwA mishahara yao Mara moja .utadhani wezi.kwa maana hawana vyeti vya kidato cha NNE .nikajiuliza 2017 kule Kilimanjaro moshi mei mosi Raisi magufuli mwenyewe alisema kuhusu uhakiki wa watumishi walio na vyeti feki hauwagusi watumishi wa darasa LA saba kwani ndivyo vyeti walivyoajiriwA navyo.sasa tukashangaa kwa huzuni mkubwa bw ndumbaru analeta msiba kwa watu hao.kweli wameumia mno basi kama serikali haiwataki walipwe hela za mifuko waliokua wanachangia lakini serikali imekaa kimya kana kwamba hakuna kilichofanyika. Kwa hawa watumishi ambao kiuhakika ndio wanyonge wa kweli kwenye taiga hili kwani mtumishi ni MTU anaebeba watu wanaomtegemea wengi mno kwa namna tofauti .serikali iangalie hili.
