Watumishi tunatafunwa na laana ya kusaidia wizi wa kura?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
53,682
120,373
Hakuna siku ninakosa kusoma habari za watumishi wa umma kulalamikia serikali kuwatupa awamu hii.Hawa wanalalamika mishahara kutokupanda,wale wanalalamika promotion,huyu analalamikia matamko ya wanasiasa yasiyokoma,Mimi nalalamikia uhakiki usiokoma.......nk nk.Lakini yote ni dhahiri mtumishi ana maisha ya unyonge na magumu sana awamu hii.Hohe have

Nimefikiria na kutafakari sana.Kuna kitu kinaitwa Laana. Hiki humpata mtu anayemtendea mwenzie mabaya huku akijua.

Wakati wa chaguzi siye watumishi wa umma ndio watendaji katika chaguzi.Mambo yote mabaya katika kuchakachua ama kupindua masanduku ya kura ni lazima mtumishi wa umma atie mkono wake.Kuanzia mgambo mpaka DED mpaka mkurugenzi wa uchaguzi.

Na kula malalamishi toka Zanzibar mpaka bars kuwa "" CCM waliibiwa sana kura na UKAWA".Najaribu kujenga hisia kwamba pengine pengine laana za kusaidia wizi wa kura katika uchaguzi vinatutafuna watumishi wa umma

Chrismass njema wana JF wote,Lema na Ben Saanane ninakulilia
 
tangu niwe mtumishi wa umma miaka 9 iliyopita leo nakula xmass nikiwa sijapokea mshahara.
nimechinja mbuzi wangu namla taratibu.....
nilikosea sana kushabikia push up, kwa mila zetu kubinua makalio juu kwa mwanaume ni ishara mbaya sana..... najuta kwa kweli
....kubinua makalio juu kwa mwanaume ni dalili mbaya sana...... nimecheka balaaaa
 
Ukimsaidia mwizi kuiba...nawe atakuibia.
Ukisaidia muuaji kuua mwishowe atakuua tu.
 
Watumishi wa umma mnavuna mlichopanda. Tena bado mtakoma zaidi awamu hii!
Yaaani awamu hiii hakuna thamani ya mtumishi wa umma...mnazodolewa hadharani na akina Makonda, Mrisho...kiufupi hamna thamani tena katika jamii.
Kwa sasa machinga ndio watoto wa baba, wanaamua wanafunga barabara wanageuza kuwa soko.
Miji na majiji yamechafuka hakuna mfano...watoto wa mwenye nyumba wanafanya watakalo.
Watumishi wa umma mmegeuzwa kuwa taktak kwa sauti ya kidhungu
 
tangu niwe mtumishi wa umma miaka 9 iliyopita leo nakula xmass nikiwa sijapokea mshahara.
nimechinja mbuzi wangu namla taratibu.....
nilikosea sana kushabikia push up, kwa mila zetu kubinua makalio juu kwa mwanaume ni ishara mbaya sana..... najuta kwa kweli
15590599_10206990800883075_6256452481452088127_n.jpeg
Umetisha
 
Back
Top Bottom