MSIMISEKI SENIOR
JF-Expert Member
- Nov 1, 2014
- 459
- 287
Kwa mujibu wa ndugu yangu anayefanya kazi TAZARA ameniambia kwamba hawajapokea mishahara ya miezi 3 sasa. Kwa mujibu wa mtoa taarifa hizo ameeleza kuwa mgogoro umetokana na kugawanyika kwa TAZARA katika mikoa 2 ambayo ni mkoa wa TANZANIA na mkoa wa ZAMBIA ambapo wenzao upande wa ZAMBIA wanalipwa mishahara yao kama kawaida lakini kwa upande wa TANZANIA hali ni tofauti.
Endapo taarifa hizi ni za kweli basi serikali inatakiwa ishughulikie tatizo hili mara moja kwani ikumbukwe watu hawa wanafamilia zao zinawategemea ikiwa ni mahitaji ya nyumbani pamoja na majuku mengine ya kifamilia, je serikali ijiulize ndugu zetu hawa wanaishije?
Dr Mwakyembe, Bi Saada Mkuya na wengineo wote wanaohusika chukueni hatua mara moja msaidie ndugu zetu hawa kwani haiji akilini mtumishi anafanya kazi zaidi ya miezi 3 pasipo ujira wake hayo ni manyanyaso na hayakubaliki.