Watumishi NBC wadai kudhalilishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watumishi NBC wadai kudhalilishwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Apr 5, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  BAADHI ya wafanyakazi wa Benki ya NBC,Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam, wamedai kudhalilishwa na mabosi wao kwa kuvuliwa nguo zote.Wakizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, wafanyakazi hao walisema walifanyiwa hivyo Ijumaa iliyopita.

  Tukio la wafanyakazi hao kufanyiwa unyama huo, tayari limeripotiwa polisi na kupewa kumbukumbu namba CD/RB/4073/2011 na CD/IR/1319/2011.

  Mmoja wa wafanyakazi hao, Michael Matayo, alisema wafanyakazi waliofanyiwa udhalilishaji huo ni watano na kwamba ni wale wa kitengo cha usafirishaji fedha.Alisema siku ya tukio, walikuwa wanajiandaa kwenda kula na kwamba kabla ya kutoka lazima upite mageti matatu na kukaguliwa na mlinzi.

  "Tulipofika geti la mwisho meneja wetu alituita akatuuliza mnajua tunachotaka kufanya, tukamwambia hatujui akasema tumsubiri nje,"alisema Matayo.Alisema baadaye waliitwa na kuingia chumba cha kubadilishia nguo chenye kamera ya CCTV na kwamba baada ya kutoka kwenye chumba hicho waliingia katika chumba kingine ambacho hakina kamera ya CCTV na kuanza kusachiwa.


  Mfanyakazi mwingine aliyedai kudhalilishwa ni Ramadhan Mbwana, ambaye alisema kitendo hicho, kilidumu kwa dakika 20 na kwamba waliamriwa kuvua nguo zote na kubaki uchi na kuchuchumaa.

  Alisema unyama huo ulifanywa na Mkuu wa Kitengo cha Usafirishaji Fedha katika benki hiyo ambaye ni raia wa Ghana."Baada ya kutusachi na kuridhika kuwa hatujaiba hela alituachia,"alisema Mbwana.

  Wafanyakazi hao pia walidai kuwa Machi 19 mwaka huu, walifanyiwa udhalilishaji mwingine ambapo waliamriwa kunyanyua mikono juu kwa zaidi ya nusu saa, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kusachiwa.

  Licha ya kuvuliwa nguo, wafanyakazi hao wamesema wamekuwa wakinyanyaswa kwa kutukanwa kudharauliwa na kufanyishwa kazi kwa muda mrefu.Hata hivyo, Meneja Uhusiano wa benki hiyo Robi Matiko,alisema hana taarifa kuhusu tukio hilo.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, aikiri kuwa na taarifa kuhusu tukio hilo lakini alisema hawezi kuzieleza kwa undani zaidi kwa sababu hawajapata taarifa kamili.Uongozi wa NBC makao makuu nao ulisema hauna taarifa.
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Nbc kuna mambo. Siku si nyingi nimesikia wanataka kugoma. Ujio wa Mafuru na Maharage Chande una kasoro.
   
 3. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Ndani ya nchi yetu? Nimesikia migodini, hata site senta?
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  tumewaleta hawa waghana waje wafanye kazi then wanaanza kutubagua weusi wenzao tena hapahapa kwetu
   
 5. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2011
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Poleni wapiganaji wenzetu!hivi mimi naomba kuuliza swali moja tuu!hivi hawa wageni wa kiafrika wanaokuja kufanya kazi hapa nchini wanakuwa wapo juu ya sheria?manake hata ukienda sehemu ambazo kuna maboss ambao ni raia wa nchi jirani mfano Kenya wanatudharau sana sisi wabongo!hivi hicho kiburi wanakitoa wapi?hivi M bongo ukienda Kenya achilia mbali kupata kazi inakua ngumu kuupata huo u boss usahau kabisa!lakini kwa hapa kwetu kila kitu tambarare!
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  we hebu acha uchochezi bana...
   
 7. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  nchi yetu imekua kama shamba la bibi lisilo na mwenyewe ndio maana tunaendeshwa na kila mtu yaani wabongo hatuna msimamo kabsa na hatujiamini nadhani falsafa hii tunajengewa toka tukiwa shule yaani tumekua watu wa kunyanyaswa na kila mtu kisa eti tuna utu moyoni kweli jamani tuamke na tusimame kutetea haki zetu tuache uoga
   
 8. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Kuna haja ya sisi nasi kuwabagua wageni
   
 9. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hawa mbona wamezoea kunyanyaswa!
  Kunawakati nilisikia hawaruhusiwi kuingia mlango mmoja wala kupanda kwenye lift moja na wazungu wa South, pia kupark magari ndani ya fence, ni wazungu tu wanao ruhusiwa.
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nazjaz sounds like she's working at NBC
   
 11. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,084
  Likes Received: 881
  Trophy Points: 280
  poleni sana ndugu zanguni wa NBC. ushauri ni kwamba tusiogope kutoa taarifa yanapotokea mambo kama hayo. ni udhalilishaji usiokuwa na mantiki yoyote ile. hata kama ni security ya fedha zao,kwani wameanza kusafirisha pesa leo? miaka yote walikuwa wanatumia mbinu gani kukagua staff wa kitengo hicho? usikute huyo mghana anamind kuchungulia dada zetu if nao wapo ktk department hiyo.
   
 12. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  l used to work there, sera za ubaguzi zikanikimbiza.
   
 13. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa NBC walisharudisha ile Server waliyoifunga south africa?
  Branches na operations zote zinafanyika Tanzania iweje Server ikae south africa?
  Yaani watanzania ni watumwa kwenye nchi yetu.
   
 14. p

  pointers JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Sijui kwa nini watanzania tunanyanyasika ndani ya nchi yetu, tulizoea kwenye viwanda watu wanalalamika leo ni kwenye mabank ambamo tunaamini watu waliomo huko wengi wamesoma na wana uelewa na kujua haki zao na kuwa na uwezo wa kujitetea. sasa mtu anaambiwa anyunyue miko juu kwa muda mrefu hivyo na yeye anakubali.........hapo ipo kazi.
   
 15. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Dawa yao ndogo tu hao,

  Ni kutembeza mkono tu, kama huwezi mkono hata stuli ikushinde!!??
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mbona umenichanganya??

  Ubaguzi ulikuondoa pale... lakini tena unasema Maharage na Mafuru kuja ndio mambo yakaharibika, sasa mbaguzi ni mafuru na maharage au hao foreigners?

  I thought ujio wa mafuru na marage ndio unaashiria kupunguza ubaguzi?? hebu nisaidie dadangu
   
 17. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nazjaz hebu tusaidie kwa hili dada yetu
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ni kweli nahitaji msaada ili nielewe, dadangu nasjaz ananichanginyi
   
 19. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Faida ndogo ndogo za kuwakumbatia wanaoitwa wawekezaji toka nje,huu ni unyama...
   
 20. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180

  Yani Robi nae ndio jibu la kutoa?kwanini asingeendelea kwa kusema atafuatilia kiundani?! halafu ni mbongo,agrrrr!!
  Kama hili tukio ni kweli ni unyanyasaji wa hali ya juu!
   
Loading...