Sifa za kiongozi ni pamoja na uadilifu wa matumizi ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania. Asiye na sifa hiyo hastahili kuwa mtumishi wa Watanzania.
Ni mapema sana kuyasema haya lakini hata tusiposema nani aseme...? Watu wengi wamekuwa wakisema juu ya Upole na busara za Rais Samia. Kwanini hapendi kufanya maamuzi ya haraka pale kunapotokea tuhuma dhidi ya viongozi wa Umma.
Rais Samia si mtu wa hekaya za abunuasi na hadithi za Esopo... kifupi hapendi porojo kwenye Taifa lililojaa wapenda ubuyu kuliko kazi.
Mauaji ya mfanyabiashara mkoani Mtwara yaliyosababishwa na Polisi. Yameonekana kumkasirisha Rais Samia kutokana na lawama zinazochafua taswira ya jeshi la Polisi nchini.
Akiwa njiani kuelekea Mara, Rais alitoa maagizo mazito kwa Jeshi la Polisi kutokana na kutuhuma zinazowakabili juu ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini mkoani Mtwara.
Rais ameifundisha Wizara ya mambo ya ndani kuwa uwajibikaji ni jambo la msingi kuliko kitu chochote kwa kulitaka jeshi la Polisi kujitafakari kwa vitendo wanavyohusishwa navyo vinachafua taswira ya safi ya Jeshi la Polisi.
Ni ukaidi wa VIONGOZI waandamizi wa Jeshi la Polisi kushindwa kutambua maana uwazi na uwajibikaji kutokana na kashfa inayowakabili Askari wa Jeshi hilo.
Anayeshupaza shingo huvunjika Taya, Tume iliyoagizwa kuundwa italifumua Jeshi la Polisi. Rais Samia ameagiza kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi itakayobaini chanzo cha mauaji hayo ukiachana na ile iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Kuchunguza tukio hilo la mauaji ya mfanyabiashara wa madini mkoani Mtwara. msisitizo wa Rais ulikuwa ni juu ya kutaka haki ipatikane. Kesi ya mbuzi hakimu hawezi kuwa Fisi kama Polisi ndiyo watuhumiwa namba moja hawapaswi kuwa ndiyo tume pekee ya uchunguzi.
Maamuzi ya Rais Samia yamefurahisha sana 90% ya Watanzania wamepata Tumaini kubwa kuwa Rais ni mtu wa kupenda haki na asiyeyumbishwa na watendaji wa hovyo.
Maamuzi ya kuundwa kwa Tume huru na kuwafukuza kazi Wakurugenzi wa halmashauri Nne (4 ) nchini kutokana na ubadhirifu wa Mali za Umma.
Yameonyesha picha mpya kuwa Rais Samia si mtu wa kuchezewa hata kidogo linapokuja suala la usalama wa raia na mali za Watanzania.
Wakurugenzi hao wamebainika kuwa na matumizi mabaya ya Pesa zilizotolewa kwenye halmashauri husika kwa ajili ya miradi ya maendeleo, Rais hapendi hekaya za Abunuwasi hata ziliposikika sauti kuwa Mkurugenzi Geita Vijijini kuwa naye ni Jipu.
Mkuu wa nchi akawatuliza Wananchi na kuwaeleza uchunguzi unaendelea mambo yakikamilika kama ni wa kubanikwa atabanikwa
Dalili zipo wazi muda si mrefu tunaweza kumpata Afande IJP mpya, Itachukua muda mrefu kufahamu sababu za matukio haya ya kinyama yanayotokea kwasasa nchini lakini jambo moja ni dhahiri; Rais Samia yupo kwa ajili ya Watanzania wote pamoja na Afrika na Dunia.
Rais Samia yupo katika ziara ya kikazi mkoani Mara na sherehe za miaka 45 ya chama cha mapinduzi, siku ya kesho anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji wa Butiama-Mugango-Kiabakari utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 10.7 za Kitanzania.