Watumishi matumbo joto, boss mpya Polisi yule...

Sifa za kiongozi ni pamoja na uadilifu wa matumizi ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania. Asiye na sifa hiyo hastahili kuwa mtumishi wa Watanzania.

Ni mapema sana kuyasema haya lakini hata tusiposema nani aseme...? Watu wengi wamekuwa wakisema juu ya Upole na busara za Rais Samia. Kwanini hapendi kufanya maamuzi ya haraka pale kunapotokea tuhuma dhidi ya viongozi wa Umma.

Rais Samia si mtu wa hekaya za abunuasi na hadithi za Esopo... kifupi hapendi porojo kwenye Taifa lililojaa wapenda ubuyu kuliko kazi.

Mauaji ya mfanyabiashara mkoani Mtwara yaliyosababishwa na Polisi. Yameonekana kumkasirisha Rais Samia kutokana na lawama zinazochafua taswira ya jeshi la Polisi nchini.

Akiwa njiani kuelekea Mara, Rais alitoa maagizo mazito kwa Jeshi la Polisi kutokana na kutuhuma zinazowakabili juu ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini mkoani Mtwara.

Rais ameifundisha Wizara ya mambo ya ndani kuwa uwajibikaji ni jambo la msingi kuliko kitu chochote kwa kulitaka jeshi la Polisi kujitafakari kwa vitendo wanavyohusishwa navyo vinachafua taswira ya safi ya Jeshi la Polisi.

Ni ukaidi wa VIONGOZI waandamizi wa Jeshi la Polisi kushindwa kutambua maana uwazi na uwajibikaji kutokana na kashfa inayowakabili Askari wa Jeshi hilo.

Anayeshupaza shingo huvunjika Taya, Tume iliyoagizwa kuundwa italifumua Jeshi la Polisi. Rais Samia ameagiza kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi itakayobaini chanzo cha mauaji hayo ukiachana na ile iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Kuchunguza tukio hilo la mauaji ya mfanyabiashara wa madini mkoani Mtwara. msisitizo wa Rais ulikuwa ni juu ya kutaka haki ipatikane. Kesi ya mbuzi hakimu hawezi kuwa Fisi kama Polisi ndiyo watuhumiwa namba moja hawapaswi kuwa ndiyo tume pekee ya uchunguzi.

Maamuzi ya Rais Samia yamefurahisha sana 90% ya Watanzania wamepata Tumaini kubwa kuwa Rais ni mtu wa kupenda haki na asiyeyumbishwa na watendaji wa hovyo.

Maamuzi ya kuundwa kwa Tume huru na kuwafukuza kazi Wakurugenzi wa halmashauri Nne (4 ) nchini kutokana na ubadhirifu wa Mali za Umma.

Yameonyesha picha mpya kuwa Rais Samia si mtu wa kuchezewa hata kidogo linapokuja suala la usalama wa raia na mali za Watanzania.

Wakurugenzi hao wamebainika kuwa na matumizi mabaya ya Pesa zilizotolewa kwenye halmashauri husika kwa ajili ya miradi ya maendeleo, Rais hapendi hekaya za Abunuwasi hata ziliposikika sauti kuwa Mkurugenzi Geita Vijijini kuwa naye ni Jipu.

Mkuu wa nchi akawatuliza Wananchi na kuwaeleza uchunguzi unaendelea mambo yakikamilika kama ni wa kubanikwa atabanikwa

Dalili zipo wazi muda si mrefu tunaweza kumpata Afande IJP mpya, Itachukua muda mrefu kufahamu sababu za matukio haya ya kinyama yanayotokea kwasasa nchini lakini jambo moja ni dhahiri; Rais Samia yupo kwa ajili ya Watanzania wote pamoja na Afrika na Dunia.

Rais Samia yupo katika ziara ya kikazi mkoani Mara na sherehe za miaka 45 ya chama cha mapinduzi, siku ya kesho anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji wa Butiama-Mugango-Kiabakari utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 10.7 za Kitanzania.
Ange anza Yeye aliyetoa hukumu ya mbowe kabla ya mahakama
 
Jeshi la polisi Tanzania limejaa majambazi yenye silaha ambazo wanazibeba muda wowote na mahali popote! Ni manyang'anyi yanapora yakiwa yamevaa nembo ya taifa kichwani na mabegani mwao! Ni wezi wanaovaa share zilizotokana na Kodi za wanyonge!
Majizi haya yamepora Mali, fedha na uhai wa wananchi wanyonge Hadi yakavimbiwa na kujenga majumba yenye makaburi ya kifahari!
Nashauri jeshi la polisi lifumuliwe na kuundwa upya pamoja na chombo mbadala Cha kufuatilia utendaji wake Kama zilivyo idara za elimu na afya
 
Maovu yote yanayofanywa na hawa Piga ua yamelelewa vyema na ccm wakati wanawapa maagizo wawagonge tu Wapinzani na kuwaua. Haya wapinzani wapo likizo kazi inaendelea kama motto yao inavyosema.
 
Sifa za kiongozi ni pamoja na uadilifu wa matumizi ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania. Asiye na sifa hiyo hastahili kuwa mtumishi wa Watanzania.

Ni mapema sana kuyasema haya lakini hata tusiposema nani aseme...? Watu wengi wamekuwa wakisema juu ya Upole na busara za Rais Samia. Kwanini hapendi kufanya maamuzi ya haraka pale kunapotokea tuhuma dhidi ya viongozi wa Umma.

Rais Samia si mtu wa hekaya za abunuasi na hadithi za Esopo... kifupi hapendi porojo kwenye Taifa lililojaa wapenda ubuyu kuliko kazi.

Mauaji ya mfanyabiashara mkoani Mtwara yaliyosababishwa na Polisi. Yameonekana kumkasirisha Rais Samia kutokana na lawama zinazochafua taswira ya jeshi la Polisi nchini.

Akiwa njiani kuelekea Mara, Rais alitoa maagizo mazito kwa Jeshi la Polisi kutokana na kutuhuma zinazowakabili juu ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini mkoani Mtwara.

Rais ameifundisha Wizara ya mambo ya ndani kuwa uwajibikaji ni jambo la msingi kuliko kitu chochote kwa kulitaka jeshi la Polisi kujitafakari kwa vitendo wanavyohusishwa navyo vinachafua taswira ya safi ya Jeshi la Polisi.

Ni ukaidi wa VIONGOZI waandamizi wa Jeshi la Polisi kushindwa kutambua maana uwazi na uwajibikaji kutokana na kashfa inayowakabili Askari wa Jeshi hilo.

Anayeshupaza shingo huvunjika Taya, Tume iliyoagizwa kuundwa italifumua Jeshi la Polisi. Rais Samia ameagiza kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi itakayobaini chanzo cha mauaji hayo ukiachana na ile iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Kuchunguza tukio hilo la mauaji ya mfanyabiashara wa madini mkoani Mtwara. msisitizo wa Rais ulikuwa ni juu ya kutaka haki ipatikane. Kesi ya mbuzi hakimu hawezi kuwa Fisi kama Polisi ndiyo watuhumiwa namba moja hawapaswi kuwa ndiyo tume pekee ya uchunguzi.

Maamuzi ya Rais Samia yamefurahisha sana 90% ya Watanzania wamepata Tumaini kubwa kuwa Rais ni mtu wa kupenda haki na asiyeyumbishwa na watendaji wa hovyo.

Maamuzi ya kuundwa kwa Tume huru na kuwafukuza kazi Wakurugenzi wa halmashauri Nne (4 ) nchini kutokana na ubadhirifu wa Mali za Umma.

Yameonyesha picha mpya kuwa Rais Samia si mtu wa kuchezewa hata kidogo linapokuja suala la usalama wa raia na mali za Watanzania.

Wakurugenzi hao wamebainika kuwa na matumizi mabaya ya Pesa zilizotolewa kwenye halmashauri husika kwa ajili ya miradi ya maendeleo, Rais hapendi hekaya za Abunuwasi hata ziliposikika sauti kuwa Mkurugenzi Geita Vijijini kuwa naye ni Jipu.

Mkuu wa nchi akawatuliza Wananchi na kuwaeleza uchunguzi unaendelea mambo yakikamilika kama ni wa kubanikwa atabanikwa

Dalili zipo wazi muda si mrefu tunaweza kumpata Afande IJP mpya, Itachukua muda mrefu kufahamu sababu za matukio haya ya kinyama yanayotokea kwasasa nchini lakini jambo moja ni dhahiri; Rais Samia yupo kwa ajili ya Watanzania wote pamoja na Afrika na Dunia.

Rais Samia yupo katika ziara ya kikazi mkoani Mara na sherehe za miaka 45 ya chama cha mapinduzi, siku ya kesho anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji wa Butiama-Mugango-Kiabakari utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 10.7 za Kitanzania.
Hata ukiangalia aliowatumbua leo ni baada ya kujiridhisha..

Aliyewekwa kiporo taarifa 2 zinasubiliwa afu ndio aamue, hapendi kufanya maamuzi kwa mihemko..
 
Katika marpc wote wa sasa, rpc ninayemuona ana busara ni rpc wa Geita, Henry Mwaibambe. Hata akizungumza anakuwa na utulivu. Ila kama vipi bora igp mpya achukuliwe kutoka jwtz.
 
Hivi Polisi mnashindwa nini kuwa kama JWTZ. Mbona wenzenu Wana heshima yao katika nchi lakini pia wengi wao hawapendi kufanya uonevu kama hao polisi au Div iv ya 33 ndio shida ya yote haya?
 
Andiko ni zuri ndugu yetu.

Kwa kauli ya Mama kuwa "Jeshi la Polisi Mjitafakari" Kama ningekuwa mimi ningeandika barua ya Kujiuzuru haraka. Tena sio hilo tu, Ikiwa kama kulivyo tokea vifo vya kufuatana na Raia, mikononi mwa Polisi, hilo tu ningejiuzuru mapema.

Kilicho muudhi Mh Rais, nadhani ni kitendo cha IGP kuunda Tume ya Uchunguzi, wakati waliofanya hayo mauaji ni maafisa wake wa Polisi, Tume ya nini wakati umewashika watuhumiwa na vielelezo vyote unavyo?

Kitendo cha Mama kusema iundwe Tume huru na sio hiyo ya polisi pekee, ni kumwambia IGP ondoka. Sasa kama IGP halioni hilo, asubiri kama yaliyomkuta Spika aliyejiuzuru mapema. Hali ilipofika, IGP hata afanye nini, nadhani Mh Rais kisha piga mstari mwekundu.

Narudia, ushauri wangu kwa heshima na kwa uelewa wangu mdogo...IGP ajiuzuru mapema, asisubiri hiyo ripoti ya hiyo kamati huru. Na ningekuwa mimi pia, hiyo kamati ya polisi ya uchunguzi, ningeifutilia mbali, ibaki hiyo ya Mh Rais, kwani hapo Rais amesha mtega tena IGP apime uelewa wake...utaendeleaje kwa na kamati yako ya uchunguzi wa jambo ambalo Bosi wako Mh Rais ameunda kamati yake kuchunguza jambo hilohilo? Hivi hata hilo IGP haoni kuwa ni mtego tena mtego wa kinidhamu zaidi?

Yangu ni hayo tu.
Ni mama yako?
 
Police kitaifa wanafanya kazi nzuri nzuri mno,niwapongeze kweli kweli,lakini tuelewe ndani yao wapo wachache ambao siyo safi,tuache unafiki watanzania,na endapo kutatakiwa kurekebishwa basis ni uwe uongozi wa kipolisi mkoa wa mtwara na haimaanishi ya kwamba askari wetu wote.
BINAFSI NALIPONGEZA SANA JESHI LETU,HAWALALI USIKU KUCHA NI PATROL KUHAKIKISHA USALAMA WETU.
 
Jeshi la polisi liongozwe na General wa JWTZ kama Wizara hiyo ilivyoongoza na Brigadier Muhidin Kimario miaka ya 80 ilitulia sana. Solution ni hiyo tu.
 
Jeshi la POLISI limesemwa toka zamani kwamba linatumia mfumo kikoloni watu wajinga wakawa wanakataa ikiwa ni pamoja na UVCCM ambao walisema wako bega kwa bega na jeshi la POLISI sasa leo Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania amesema iundwe tume tofauti na ile ya akina Siro.Ndani ya Jeshi la POLISI Kuna majambazi wengi sana wanaodhulumu watanzania mali zao watu wengi wenye kufanya biashara za madini waneuawa sana na jeshi la POLISI juzi tumeona marehemu Hamza amenyang'anywa madini yake na POLISI na baada ya Hamza kureact na kuuwa baadhi ya polisi jeshi la POLISI likaja na uchunguzi feki na wa kipumbavu kabisa kwamba marehemu Hamza alikuwa Gaidi huku wao wakificha Ujambazi na uharamia wanaowafanyia watanzania.Hili jeshi kwa wakati na karne tunayoishi limeshapoteza sifa kabisa na halifai.Limebaki na kazi ya Kuwabambikia KESI watanzania maskini na wanyonge,Angalia kesi ya Freeman Mbowe ni upumbavu mtupu ndio unaendelea pale mahakamani mashahidi wote ni wa kubumba tu.
 
Tatizo ni mfumo wa jeshi la Polisi na watumishi wake kukosa maadili.

Kubadili IGP hakutasaidia labda IGP atokee JWTZ ambako hakukulia kwenye maadili ya kipolisi.

Zaidi sana tutakua tunajifurahisha tu na tatizo kubakia pale pale.
Sio kweli, unakumbuka kipindi cha mahita jeshi lilikuwa kama kama yale magenge ya wauza madawa ya kulevya ktk jiji la mexico city, au bogota?lakini alipoingia said mwema mbona lilirudi kwenye mstari?tatizo la siro alipoteuliwa na meko, wote waliamini ktk falsafa ya utumiaji nguvu tu, na vitisho!!watu wangapi wameuawa mikononi mwa polisi?lakini utasikia tu eti walikuwa wanajibishana kwa risasi na polisi!!!
 
Back
Top Bottom