Watumishi 2,000 Elimu wapandishwa vyeo

Watumishi 2,000 Elimu wapandishwa vyeo

comrade igwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2015
Posts
7,295
Reaction score
3,952
Bunge limeelezwa kuwa Jumla ya watumishi 2,272 walipandishwa vyeo katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kipindi cha 2015/16 huku miongoni mwao 71 walitoka Chuo cha Ualimu Korogwe.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda (CCM), aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwapandisha daraja wale waliostahili na kuwa lini itawalipa madai yao ya fedha za likizo ambazo watumishi hawajalipwa kwa muda mrefu na wamekuwa wakishindwa kuzipata kwa wakati.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri huyo alibainisha serikali inaendelea kulipa madeni, ikiwamo fedha za likizo kwa walimu au watumishi katika sekta ya Elimu, ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi Juni 2016, jumla ya Sh. Bilioni 22.7 zililipwa kwa walimu 63,814.

Aidha, alisema katika kipindi cha mwaka 2016/17 hadi Machi 2017, Sh. Bilioni 10.5 zimelipwa kwa walimu 22,420, hivyo kufanya jumla ya walimu waliolipwa katika kipindi hicho kufikia 86,234 na kwamba katika fedha hizo, Sh. Bilioni 13.4 zililipwa kwa ajili ya madeni ya
fedha za likizo kwa watumishi 6 wa Chuo cha ualimu Korogwe.

“Uhakiki wa madeni ya miaka ya nyuma unaendelea kuratibiwa na mamlaka husika na taratibu za malipo zitakamilishwa kwa wale
watakaostahili,” alisema.

Chanzo: Muungwana
 
Hivi wizara ya elimu imeshabadilishwa tena?
Ni wizara ya elimu sayansi, technolojia na mafunzo ya ufundi?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hakuna cha kupandishwa vyeo wala cha madaraja. Labda kama walipandishwa kwa kuangalia wewe ni mtoto wa nani! Tangu January 2012 mpaka leo sijaona daraja na mchahara ni ule ule.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hao walopandishwa vyeo wamepewa na nyongeza za vyeo?
 
waliolipwa pesa za likizo uhakiki wao ulishakwisha coz wao co wa nchi hii, ila madaraja wao wanaishi koromije watasubir sanaa mpk uhakiki uishe..
 
Bunge limeelezwa kuwa Jumla ya watumishi 2,272 walipandishwa vyeo katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi katika kipindi cha 2015/16 huku miongoni mwao 71 walitoka Chuo cha Ualimu Korogwe.

Back
Top Bottom