Watumiaji wa programu bandia za kumpyuta hatarini

Watumiaji wa programu bandia za kumpyuta hatarini

Kurunzi

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
10,198
Reaction score
11,631
WATUMIAJI wa kompyuta ambao hutumia haramia na bidhaa bandia za programu za
kompyuta nchini kwa matumaini ya kuokoa fedha, huongeza nafasi ya kupata
maambukizi ya virusi katika programu.

Hayo yalibainshwa katika utafiti uliofanywa na Kampuni ya Microsoft Corp na
Shirika la kimataifa la International Data Corporation.
Kuhusu matokeo ya maambukizi haya, utafiti unaonesha kuwa watumiaji binafsi
watatumia saa bilioni 1.5 na dola bilioni 22 kutambua, kukarabati na kuboresha
programu za haramia na bandia wakati makampuni ya kimataifa yatatumia dola
bilioni 114 ya kukabiliana na athari ya programu haramia na bandia.
Utafiti wa Global IDC ulichambua mitandao 270, downloads 108, 155 programu na
CD / DVD, na kuwahoji watumiaji 2,077 na mameneja IT au CIOs 258 kutoka nchi za
Brazil, China, Ujerumani, India, Mexico, Poland, Urusi, Thailand, Uingereza na
Marekani.

Watafiti wamegundua kwamba programu bandia ambayo haikuja na kompyuta,
asilimia 45 zinatokana na intaneti, na asilimia 80 ya programu hizo kutoka kwa
mitandao ya pamoja aina ya Spyware, zikiwamo pia Trojans na Adware kwa asilimia
36.

"Kulingana na utafiti wa 2011 BSA Global Software piracy, thamani ya
kibiashara ya programu bandia ambazo zimewekwa kwenye kompyuta binafsi katika
Afrika Mashariki na Kusini, ambapo Afrika Kusini haihesabiwi, zilikuwa dola
milioni 108 mwaka wa 2011, asilimia 83 ya programu zilizotumika zikiwa
bandia.

"Mbali na athari za kiuchumi, ukiukaji huu unaweza pia kuleta afya mbaya na
madhara ya usalama kwa umma, hasa ununuzi wa dawa feki, vipodozi, vifaa vya
upasuaji, chakula, sigara, kunywa pombe, magari na sehemu za ndege," alisema
Meneja Mkuu wa Microsoft Mashariki na Kusini mwa Afrika, Eric Odipo.
Naye Mshauri Mkuu wa Kituo cha IT-brottslighet Microsoft, David Finn, alisema
maharamia wanaharibu ‘code' halisi za bidhaa na badala yake kuweka ‘code' bandia
 
Kwan ukbadili code za program, cmptr inaharbika?
Hata kama una2mia software za kununua (orginal) ktk Pc lazma tu kuna cku itaharbka maana huwez kukaa na cmptr ile ile miaka 20+ hawa microsoft waache 2waibie cos security mechanism yao ni 'weak'
2kiachana hayo
hebu fikiria iwapo robo tatu ya software ulzonazo ktk Pc Yako utaznunua, je utakua ume2mia Tsh ngap?
Na kwa mfano Antivirus ya Kaspersky ununue kila mwaka kwa Tsh. 30,000/=
gharama n shlng ngap?
Ahaa bora iharbike tu then utatafuta nyngne tena hlf unaweka software za kuCRACK
maana gharama za software kwa ujumla znazid gharama ya Pc
n kama mfano wa Simu, 2nanua cm may be kwa Tsh. Elfu sabin lkn hela utakazo2mia kwa kunua Vocha (baada ya miaka miwili) itakua inazd ile ya cm,
sasa je 2ngekua 2na2mia vocha feki but znafanya kazi hlf baada ya miaka miwili au mitatu cm inakufa kisha unanua nyingne! C unaona 2ngeokoa gharama
 
hivi bila software piracy, tungekuwa tunaishije?
Windows 8 pro 119usd, + office + adobe creative suite + antivirus. Spati picha kwa kweli!!
 
hivi bila software piracy, tungekuwa tunaishije?
Windows 8 pro 119usd, + office + adobe creative suite + antivirus. Spati picha kwa kweli!!

mkuu hivyo vitu vimetengenezwa kwa watu wanaozalisha.

Unakuta mbongo ana adobe zote nyengine hata sku moja hajaitumia ana office collection yote then anatumia word tu, so sisi tunapenda kuinstall install tu.

Kila kitu kina alternative mkuu naamini inawezekana kabisa kuishi bila kuiba except kwa watu wachache.

1. Windows inakuja na computer tunza cd yako ya kurecover usitoe hio window tusingekua tunanunua windows.

2. Zipo office starter pack kama ile ya 2010 unapata word na excel (sina uhakika kama powerpoint ipo) ila hii starter pack ni bureee.

3. Its hard kumreplace adobe lakini kama unazalisha utanunua na kama huzalishi tuna assume matumizi yako madogo na kama una matumizi madogo then tunasema wewe unaweza ukapata alternative zipo freeware nyingi za matumizi madogo
 
kila kitu kina alternative kutimiza lengo mfano: ms office collection ina alternative kama open office na libre office ambazo ni bure,

adobe reader kuna pdf reader nyingi tu kama foxit reader na zinginezo

hata operating system za free zipo kibao, mie nimetumia ubuntu kwa mrefu sana kama alternative ya windows

na application kibao tu, so sio lazima kutumia pirate copies
 
microsoft office stater ni bure ila huwezi kuweka footnotes, huwezi kufanya review na kucomment hii ni kwa watu ambao wao hufungua tu documents na kusoma. mfano wanafunzi vyuoni wanaweza kutakiwa kuweka reference kwenye assignment zao au research, microsoft office stater haiwezi kuwa saidia.
microsoft word 2013 pekee ina uzwa dola 109 au office home and student 2013 ina uzwa usd139.

laptop (notebooks) affodable nyingi zinkuja bila OS au wakikusaidia sana ukute wameku wekea linux suse.
ili kupata windows yenye genuine licence inabi either unune windows 8 pro kwa 119usd au windows 7 ultimate kwa 319usd. mtu wa kawaida asiye tumia kwa biashara hawezi kumudu hizi gharama


Kila kitu kina alternative mkuu naamini inawezekana kabisa kuishi bila kuiba except kwa watu wachache.
sidhani kama kwa uchumi wetu kuna alternative ya ku download, ku crack na ku intall.
 
Back
Top Bottom