Watumiaji wa gesi zingatieni usafi

Watumiaji wa gesi zingatieni usafi

Trainee

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
3,118
Reaction score
4,238
Habari zenu...
Waungwana hili jambo la kutumia gesi kupikia ni zuri na kiukweli limerahisisha sana maswala ya kupika hasa kwa sisi mabachela

Sambamba na kuwa gesi ni mkombozi wetu katika nishati ya kupikia lakini kama kawaida kila zuri halikosi ubaya, kasoro na changamoto zake

Mimi naileta changamoto/kero moja tu ambayo inaletwa na watumiaji wenyewe nayo ni uchafu tunaokumbana nao kwenye mitungi wakati wa kubadilisha

Muda mwingine mtu unapoenda kubadilisha hadi unatamani kukataa mtungi unaopewa aisee; unapewa mtungi umegandiana vyakula na uchafu mwingine kibao

Mfano mitungi mingine unakuta imegandiana uji, ngano, vinyesi vya wanyama, mafutamafuta au hata tope muda mwingine. Hivi ni kweli inashindikana kuzingatia usafi!?

Watu tunatofautiana bana sio kila mtu anaweza kustahimili hiyo hali. Mitungi hiyo inazunguka takribani kwa wateja wote wa gesi sasa msifanye kama hamtambui hilo

Watumiaji wa gesi zingatieni usafi bana ujue mnazingua!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kataa mitungi michafu tuhame ofisi yako tuone utakula nini

Kwani kwenye gari ukiwapa wanakataa?

Sitetei hili jambo ila nakupa angalizo haya maneno yako yaishie humu humu mitandaoni.

Mangi akipelekewa hata uliomwagikiwa na kiporo hupokea vizuri na kusema "nikupelekee hadi nyumbani au"

[emoji23][emoji23]
 
Habari zenu...
Waungwana hili jambo la kutumia gesi kupikia ni zuri na kiukweli limerahisisha sana maswala ya kupika hasa kwa sisi mabachela

Sambamba na kuwa gesi ni mkombozi wetu katika nishati ya kupikia lakini kama kawaida kila zuri halikosi ubaya, kasoro na changamoto zake

Mimi naileta changamoto/kero moja tu ambayo inaletwa na watumiaji wenyewe nayo ni uchafu tunaokumbana nao kwenye mitungi wakati wa kubadilisha

Muda mwingine mtu unapoenda kubadilisha hadi unatamani kukataa mtungi unaopewa aisee; unapewa mtungi umegandiana vyakula na uchafu mwingine kibao

Mfano mitungi mingine unakuta imegandiana uji, ngano, vinyesi vya wanyama, mafutamafuta au hata tope muda mwingine. Hivi ni kweli inashindikana kuzingatia usafi!?

Watu tunatofautiana bana sio kila mtu anaweza kustahimili hiyo hali. Mitungi hiyo inazunguka takribani kwa wateja wote wa gesi sasa msifanye kama hamtambui hilo

Watumiaji wa gesi zingatieni usafi bana ujue mnazingua!

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo la uchafu wa mitungi ya gas ni supplier ambaye anatakiwa achukue direct kutoka kwa kampuni inayomiliki hiyo mitungi.

Kampuni ina dhamana ya kusafisha ile mitungi na hata kuipaka rangi baada ya kujiridhisha na umadhubuti unaoonekana kuchakaa.

Acha kuchukua kwa makanjanja!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, ebu kuwa mfanya biashara mwenye adabu kwa sisi wateja wako
 
Kwa hiyo ukikuta chupa soda unayokunywa imegandiana uchafu utalaumu nani kati ya mtumiaji wa mwisho au kiwanda?
 
Petrol Station Fire kuna ndoo na sponge, ukipeleka mtungi mchafu unaambiwa uusafishe kwanza.
 
Habari zenu...
Waungwana hili jambo la kutumia gesi kupikia ni zuri na kiukweli limerahisisha sana maswala ya kupika hasa kwa sisi mabachela

Sambamba na kuwa gesi ni mkombozi wetu katika nishati ya kupikia lakini kama kawaida kila zuri halikosi ubaya, kasoro na changamoto zake

Mimi naileta changamoto/kero moja tu ambayo inaletwa na watumiaji wenyewe nayo ni uchafu tunaokumbana nao kwenye mitungi wakati wa kubadilisha

Muda mwingine mtu unapoenda kubadilisha hadi unatamani kukataa mtungi unaopewa aisee; unapewa mtungi umegandiana vyakula na uchafu mwingine kibao

Mfano mitungi mingine unakuta imegandiana uji, ngano, vinyesi vya wanyama, mafutamafuta au hata tope muda mwingine. Hivi ni kweli inashindikana kuzingatia usafi!?

Watu tunatofautiana bana sio kila mtu anaweza kustahimili hiyo hali. Mitungi hiyo inazunguka takribani kwa wateja wote wa gesi sasa msifanye kama hamtambui hilo

Watumiaji wa gesi zingatieni usafi bana ujue mnazingua!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nadhani wa kulaumiwa ni hao wamiliki wa gas. Wasafishe mitungi kabla ya kujaza upya.
chupa za soda tunarudisha chafu lkn wanaziosha Kwanza kabla ya kujaza tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao nao wamezidi uchafu unabebaje mtungi mchafu namna hiyo huoni aibu???? Jamani kitu kichafu kinavyotia kinyaa mtu anajibebea tu bila haya!?? Kwakweliii wabadilike naunga mkono hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HUU NI UGONJWA USIO NA DAWA.

BINAFSI ENEO NNALOBADILISHIA MTUNGI WAMESHANIELEWA KILA NIKIBADILISHA LAZIMA WANIPE WENYE HADHI YANGU.

VINGINEVYO NI TABIA YA WATUMIAJI WASIYO NA STAHA YAANI HAO HAWAJUI KUWA ULE MTUNGI NI MALI YAKE SO KWA SABABU UNABADILISHWA ANA AMUA KUHARIBU KWA UCHAFU.
 
Nilifungua haraka haraka nikidhani umesema watumiaji wa GESTI
 
Back
Top Bottom