Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 3,118
- 4,238
Habari zenu...
Waungwana hili jambo la kutumia gesi kupikia ni zuri na kiukweli limerahisisha sana maswala ya kupika hasa kwa sisi mabachela
Sambamba na kuwa gesi ni mkombozi wetu katika nishati ya kupikia lakini kama kawaida kila zuri halikosi ubaya, kasoro na changamoto zake
Mimi naileta changamoto/kero moja tu ambayo inaletwa na watumiaji wenyewe nayo ni uchafu tunaokumbana nao kwenye mitungi wakati wa kubadilisha
Muda mwingine mtu unapoenda kubadilisha hadi unatamani kukataa mtungi unaopewa aisee; unapewa mtungi umegandiana vyakula na uchafu mwingine kibao
Mfano mitungi mingine unakuta imegandiana uji, ngano, vinyesi vya wanyama, mafutamafuta au hata tope muda mwingine. Hivi ni kweli inashindikana kuzingatia usafi!?
Watu tunatofautiana bana sio kila mtu anaweza kustahimili hiyo hali. Mitungi hiyo inazunguka takribani kwa wateja wote wa gesi sasa msifanye kama hamtambui hilo
Watumiaji wa gesi zingatieni usafi bana ujue mnazingua!
Sent using Jamii Forums mobile app