Watumia mitandao watakiwa kupendana

Watumia mitandao watakiwa kupendana

Joined
Aug 29, 2016
Posts
18
Reaction score
10
Watanzania wanaotumia mitandao ya kijamii, wameaswa kutotumia maneno ya lugha ya kuudhi dhidi ya mwingine. Badala yake wapendane hata kama hawafahamiani wala kuwahi kuonana.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwangalizi Mkuu wa Makanisa ya Baptist Tanzania alipokuwa akihubiri kukaribisha mwaka na kusimika wazee viongozi wa kanisa la Makole mjini Dodoma.

Mch Nhonya amesema Mungu alipotuumba alitupatia masikio mawili na mdomo mmoja, maana yake tusikilize zaidi kuliko kuzungumza.

"Wakati mwingine Kunyamaza nako ni hekima, busara, na ni ishara ya ukomavu kwa kiongozi, siku hizi Kumekuwa na tabia ya hovyo kabisa ya watu kujibizana vibaya na hata kutukanana na kusema maneno machafu na kuweka picha za maudhi, tena wanaofanya hivyo wengine ni watu wazima na viongozi katika jamii, ambao wanategemewa kuwa vielelezo kwa jamii na taifa hili ambalo asilimia kubwa ni vijana na watoto."

Mch Nhonya amekemea vikali wanaoweka picha chafu za uchi kwenye mitandao na wanaoandika maneno machafu dhidi ya wengine. Pamoja na uhuru wa kila mtu kuwasiliana na kutowa maoni yake, lakini nidhamu kwa jamii lazima isimamiwe.

Kila mahali pana nidhamu yake, heshima ya mavazi, staha katika maneno, na kauli nzuri kwa wengine zinahitajika.
Mch. Nhonya amesema, Mungu ametubariki kwa mawasiliano na wepesi wa maisha kwa kutumia vifaa vya kisasa tulivyo navyo siku hizi tofauti na wenzetu wa Zamadani. Hivyo tuitumie vema, tupendane, kuheshimiana na kutii sheria zilizowekwa za mtandao.

Sisi kama kanisa hatutaacha wajibu wetu kuhubiri, kuwaonya, kuwakemea na kuwashauri watu wote, maana ndiyo kazi tuliopewa na Mungu kuifanya.

Aidha Mch Michael Nhonya amesema Kuna wakati wa kanisa kunyamaza na kuna wakati wa kusema. (Mhubiri 3:1-5)
 
Upendo Wa Agape.
Kutibuana kweny mitandao ni kawaida tu km ilivyo kwenye jamii zingine. Kuna watu wastaarabu na wasiowastaarabu.
Ushajiuliza kwann mtu anajiita Kichwa Kichafu? Km ameweza kwann msitibuane?
Natania tu mkuu. Tumeambiwa tupendane sana zaidi ya sana.
Habari za saa hizi kijana!
 
Kutibuana kweny mitandao ni kawaida tu km ilivyo kwenye jamii zingine. Kuna watu wastaarabu na wasiowastaarabu.
Ushajiuliza kwann mtu anajiita Kichwa Kichafu? Km ameweza kwann msitibuane?
Natania tu mkuu. Tumeambiwa tupendane sana zaidi ya sana.
Habari za saa hizi kijana!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] watu wanajitoa ufahamu mda na mda.


Salama kabisa Boss
 
Mambo mengine yanasikitisha sana...

Mch: anakemea povu/mapovu...

Siyo rahisi wote tukapendana... Ni kuvumiliana tu...


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom