Watuhumiwa ugaidi wachafua hali ya hewa kortini

Watuhumiwa ugaidi wachafua hali ya hewa kortini

albuluushiy

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2013
Posts
1,404
Reaction score
687
KIONGOZI wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Farid Hadi Ahmed (43), ametoa shutuma nzito dhidi ya Jeshi la Polisi akidai kuwa limewafanyia ukatili kwa kuwapiga, hali inayowafanya baadhi yao wajisaidie damu.

Sheikh Farid alitoa madai hayo jana, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Riwa, wakati kesi ya tuhuma za ugaidi inayowakabili ilipokuwa ikitajwa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Peter Njike, alidai kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi haujakamilika na wanaomba hati ya kuwachukua washtakiwa saba, akiwamo Sheikh Farid kwa ajili ya mahojiano.

Hakimu Riwa alikubali maombi hayo na kuahirisha kesi hadi Septemba 3, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Hali hiyo ilisababisha washtakiwa kuomba kutoa maelezo yao.

"Mheshimiwa wametuomba kwenda kutuhoji tena, mara ya kwanza tulipohojiwa, polisi hawakutumia ustaarabu wala ubinadamu, ni ushenzi na ukatili, walituhoji uchi wa mnyama na kutupiga.

"Kiongozi Mkuu wa Uamsho, Sheikh Mselem Ally Mselem, mwenye heshima, mfasiri wa Kur'ani, alinihadithia alipohojiwa walimfanya nini, tumepigwa na hatukutibiwa, magereza wamejitahidi, lakini hawana nyenzo za matibabu.

"Watu wameumizwa vibaya, mengine hayasemeki, wanajisaidia haja ndogo damu wiki moja hadi mbili, tunaomba tufanyiwe uchunguzi wa afya zetu, ipo siku mahakamani italetwa maiti.

"Tumekamatwa sababu hatutaki Muungano, hiyo ndiyo kesi ya msingi, tunawaambia ukweli katika mihadhara na watu wanatuamini, tunaomba Sheria ya Mabadiliko ya Katiba iletwe mahakamani tuijadili," alidai Sheikh Farid.

Mshtakiwa wa 12, Salum Alli Salum, aliomba mahakama imwite daktari ili aweze kufanyiwa uchunguzi wa afya yake kwani ameingiliwa kijinai kwa nguvu.

"Mheshimiwa tunalazimishwa kutoa maelezo wanayoyataka wao, wanatuingilia kinyume cha maumbile, wanaingiza majiti, chupa, wengine wanavuja nyuma, kama unaweza hakimu twende faragha nikakuonyeshe.

"Askari ameniingilia kisha akaniingiza jiti mpaka likakatika, kungekuwa na sehemu ningekuonyesha, Jeshi la Polisi la kwanza kuvunja sheria, waliofanya madhila haya wanawatukanisha Watanganyika na kufanya waonekane wabaya," alidai mshtakiwa huyo.

Baada ya washtakiwa hao kutoa malalamiko yao, mahakama iliwaahidi washtakiwa hao waende wakahojiwe na muda wote watakuwa katika mazingira salama.

Sheikh Faridi na wenzake 19 wanashtakiwa kwamba kati ya Januari 2013 na Juni 2014 maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walikula njama ya kutenda kosa la kuingiza watu nchini kufanya ugaidi.

Shtaka la pili linawakabili washtakiwa wote, wakidaiwa kuwa katika kipindi hicho walikubaliana kumuingiza Sadick Absaloum na Farah Omary nchini ili kushiriki kutenda makosa ya ugaidi.

Katika shtaka la tatu linalomkabili Sheikh Farid, anadaiwa kati ya Januari 2013 na Juni 2014 maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku akijua ni kosa, alimuingiza nchini Sadick na Farah kufanya ugaidi.

Sheikh Farid pia anadaiwa kuwahifadhi Sadick na Farah, huku akijua watu hao walitenda vitendo vya kigaidi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Jamal Swalehe, Nassoro Abdallah, Hassan Suleiman, Anthari Ahmed, Mohammed Yusuph, Abdallah Hassani, Hussein Ally na Juma Juma.

Wengine ni Saidi Ally, Hamisi Salum, Saidi Amour Salum, Abubakar Mngodo, Salum Ali Salum, Salum Amour Salum, Alawi Amir, Rashid Nyange, Amir Hamis Juma, Kassim Nassoro na Said Sharifu.

Wakati huohuo, kesi nyingine ya ugaidi inayomkabili Kiongozi Mkuu wa JUMIKI, Sheikh Mselem Ali Mselem na mwenzake, Abdallah Said Ali, imeahirishwa hadi Septemba 3, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa kwa sababu Sheikh Mselem hakuwapo anaumwa.

CHANZO:
MTANZANIA
 
Usiombe kuhojiwa na polisi. Hivi hakunaga namna nyingine ya kuwafanya wakiri maana hiyo siyo Afrika tu, hata kule Guantanamo bay ilikuwa unyama wa kufa mtu.
 
biinafsi chai haipiti
Wewe kama gaidi haiwezi kupita na yale waliyokuwa wanafanya yangelenga ndugu zako ungejua kuwa hawa siyo watu na waliyofanyiwa ni sawa tena inatakiwa iwe zaidi ya hapo.
 
Usiombe kuhojiwa na polisi. Hivi hakunaga namna nyingine ya kuwafanya wakiri maana hiyo siyo Afrika tu, hata kule Guantanamo bay ilikuwa unyama wa kufa mtu.

gaidi hawezi kuhojiwa kistaarabu.
 
Usiombe kuhojiwa na polisi. Hivi hakunaga namna nyingine ya kuwafanya wakiri maana hiyo siyo Afrika tu, hata kule Guantanamo bay ilikuwa unyama wa kufa mtu.
Mkuu ujue waharifu wajinga sana mtu anakataa ukweli uliodhahili sasa hapo unatengemea nini zaidi ya kumtengeneza tu.
 
gaidi hawezi kuhojiwa kistaarabu.

kwa sheria gani acha kukurupuka hapa hatuzungumzi kwa kutumia ******** km unavyofanya ww,then je unaweza kuleta ushahidi wa ugaidi wao coz uplelezi haujakamilika sasa kama una ushahidi unafaa na ww kuhojiwa na polisi
 
utaisha watakapoacha ugaidi


nami nikifanya ugaidi sawa tu.


Gaidi wa kwanza kuwekwa ktk HISTORIA
anapatikana kwenye BIBLIA.
Huyu GAIDI jina lake Aliitwa SAMSON.
Alijitoa MUHANGA kwa kuangusha nguzo za nyumba
KAFA YEYE na WATU WASIO NA HATI ZAIDI YA 3000!
Unamjua? Au nikupe andiko?
Manake nyie wagalatia andiko lenu pia hamlijui.
Kasome WAAMUZI 16:29 uone mnavyouwa watu
wasio na hatia yyt.
Halafu mnatunga na nyimbo za Kumsifu GAIDI
Samsoni.
Na wa pili ni YESU! aliyejitoa Roho yake mwenyewe.
Anasema.
YOHANA 10:17
Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai
wangu ili niutwae tena.-
18-Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa
mwenyewe.
YAANI KAJIUA MWENYEWE!
Nyie ndio mmefundisha watu Mambo ya KUJITOA
MUHANGA.
 
Nimekuja mbio mbio nikijua wamejamba kumbe ni porojo tu!
 
Gaidi wa kwanza kuwekwa ktk HISTORIA
anapatikana kwenye BIBLIA.
Huyu GAIDI jina lake Aliitwa SAMSON.
Alijitoa MUHANGA kwa kuangusha nguzo za nyumba
KAFA YEYE na WATU WASIO NA HATI ZAIDI YA 3000!
Unamjua? Au nikupe andiko?
Manake nyie wagalatia andiko lenu pia hamlijui.
Kasome WAAMUZI 16:29 uone mnavyouwa watu
wasio na hatia yyt.
Halafu mnatunga na nyimbo za Kumsifu GAIDI
Samsoni.
Na wa pili ni YESU! aliyejitoa Roho yake mwenyewe.
Anasema.
YOHANA 10:17
Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai
wangu ili niutwae tena.-
18-Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa
mwenyewe.
YAANI KAJIUA MWENYEWE!
Nyie ndio mmefundisha watu Mambo ya KUJITOA
MUHANGA.

Wanasema akili ya kuambiwa changanya na yakwako pamoja na vifungu vya mandiko ya kwenye bible ulivyovisema/kalili umesikia ni mkristo gani aliyejitoa mhanga kwa kufuata maandiko hayo wakristo wanauelewa wakuchambua mambo siyo nyinyi mnadanganywa eti ukiwauwa watu/makafiri unapata dhawabu na unaenda kuzawadiwa mabikra 70,je na mwanamke anayejitoa mhanga anaenda kupewa wanaume wagapi iliwakamgegede?
 
Askari wetu wanavunja Katiba ni vizuri waheshimu Haki za Binadamu,Mamlaka husika zichukue hatua dhidi ya Askari wote waliofanya vitendo hivyo viovu.
 
Nina hofu na mashaka kwani naona watu wanazima moto kwa kutumia petrol.Hili jambo linahitaji hekima sana kuzima ukatili kwa ukatili ni balaa na laana mbaya sana kwa binadamu!!
 
kwa sheria gani acha kukurupuka hapa hatuzungumzi kwa kutumia ******** km unavyofanya ww,then je unaweza kuleta ushahidi wa ugaidi wao coz uplelezi haujakamilika sasa kama una ushahidi unafaa na ww kuhojiwa na polisi
hao ni watuhumiwa ushahidi ndio unatafutwa. hakuna kukurupuka hapo. kule znz aliuliwa padre, masheikh kumwagiwa tindi kali etc. tumeona mtuhumiwa mahakamani anatabasamu na kuashiria ushindi V.
sasa bila shaka wanasaga meno.
 
Back
Top Bottom