Watuhumiwa 65 madawa kuitwa Ijumaa ni kama Mtego, Huenda Wengi wakalala Selo....

kbosho

JF-Expert Member
Jun 4, 2012
13,030
6,562
Wana Jf...

Kwa mtazamo wa haraka haraka watuhumiwa 65 walio agizwa na Mkuu wa Mkoa kuripoti kituo kituo kikuu cha Polis...siku ya kesho, huenda wengi wao wasirudi nyumbani.

Maana naamini wapo ambao hawatapona na kutokana kesho ni siku ya Ijumaa mchakato wa dhamana utawabana kutokana na mda, hivyo kukosa dhamana na kulala Selo
 
Kwanini lengo liwe kulaza watu ndani bila ulazima wa kufanya hivyo.
Kwanini tunakuwa na roho mbaya kiasi hiki.
 
Wauza MADAWA Ya kulevya ni sawa na,'MAGAIDI' 'WAUAJI' kamwe sheria isiwaonee huruma
 
Kwanini lengo liwe kulaza watu ndani bila ulazima wa kufanya hivyo.
Kwanini tunakuwa na roho mbaya kiasi hiki.
mkuu kaka Gwajima na Manji wamelala jana...tujiulize wangeripoti leo ingekuwaje? wangelala mpaka juma tatu!!!!...
 
sasa kwa hao 65 si wahisiwa tu?
In this Country, you are GUILTY until proven otherwise.

Sasa watu walikamatwa, wakalala lupango wakinyea debe kwa siku tatu, then wakapelekwa mahakamani kwa kosa lisiloeleweka, then eti wakapewa onyo na kuambiwa watakuwa wanachunguzwa kwa mwaka mmoja ili kuona kama wao ni nuisance na kama watatishia ''peace and harmony'' kwenye jamii. Kama sio wehu ni nini hiki?

Wajanja wasiende leo. Kama mtu yupo mkoani sasa hivi kwenye issue zake za kuingiza mkwanja wanataka arudi fasta ili iweje kwa mfano?
 
Ebu nisaidieni lakini, kati ya polisi na mkuu wa mkoa ni nani anatoa wito mtu afike polisi kujibu tuhuma za uhalifu?
 
wanahamishia attention ya watu polisi kati ili mambo mengine yaende. wako strategic kuwalaza rumande hao. Kwa nini ijumaa tena saa tano. Duh. Wasioenda leo itakuwaje?
 
kwa u
Ebu nisaidieni lakini, kati ya polisi na mkuu wa mkoa ni nani anatoa wito mtu afike polisi kujibu tuhuma za uhalifu?
kwa
uelewa wangu nadhani kama kosa ni la kimashtaka basi Afisa wa polisi wanahusika. Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi anapaswa kutoa maelekezo ndani ya kamati yake ama maagizo kwa vyombo vya usalama kisha wao wafanyie kazi maagizo na kupeleka taarifa kwake. Sasa huyu hadi kwenye mahojiano ya kipolisi anakuwepo. Terrible!
 
Nina wasiwasi kama watafika wengi maana wengine wametajwa kwa aka au jina moja sasa sijajua hapo kisheria imekaaje?!!!
 
Back
Top Bottom