Watu wote wenye msongo wa mawazo kuhusu January fanyeni yafuatayo mwakani msiwe vichaa

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
1. Kama unaishi nyumba ya kupanga make sure mkataba wako wa pango unaanza katikakati ya mwaka au mwishoni na Januari haupo kwenye list ya wadaiwa wa kodi

2. Kama umepanga eneo la biashara lipa kodi ya pango November au Desemba mwanzoni hautaweza kufanya matumizi makubwa kuzidi bajeti itakayobaki

3. Kama unasomesha, lipa ada zote kabla ya Desemba

4. Kama una madeni yalipe kabla ya 15 desemba

5. Usichukue mkopo Desemba

6. Nununua chakula cha ziada mwezi Desemba kwa ajili ya wageni lakini pia kwa ajili ya kula Januari

7. Kama upo single na umetimiza masharti 1-6 hapo juu.....tenga pato lakuchukulia demu mkali aidha wa kudumu naye au wakutumia desemba.

8. Kwa wadada waliopo single epuka sana mtongozo wa mwisho wa mwaka kwani vijana wengi watakuwa wanatumia mbinu Na. 7 hapo juu kukuchezesha watakavyo

9. Epuka sana kujiunga kwenye groups za whatsapp zinazoanzishwa kuanzia Oktoba, nyingi uanzishwa kwa ajili ya kutengeneza mazingira ya michango ya harusi ni

10. Zingatia yaliyoelezwa hapo endapo tu pesa zako ni za mawazo au zakudunduliza.
 
Back
Top Bottom