Watu weusi wana roho mbaya na fikra za hovyo sana, ni wachache sana wenye utu!

Paploman

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
1,720
3,237
Hizi ngozi nyeusi zina roho mbaya sana wakuu,

Mwaka fulani huko nyuma kuna taasisi ya nchini Norway ilikuja hapa nchini kuendesha mradi fulani hivi na kwa upande wa serikali ofisi yetu ndio ilikuwa msimamizi wa huu mradi. Hawa jamaa walikuwa na hela sana, kazi zao nyingi zilikuwa zinafanyika mikoani, na mimi ndio ilikuwa mara ya kwanza kufanya miradi na hawa wageni nikabahatika kuwemo kwenye team kutoka ofisini kwetu, ilikuwa ni kazi ya miaka 2, pamoja na kwamba tulikuwa tunalipwa mishahara na posho serikalini na wao pia wakawa wanatulipa sawasawa tunavyolipwa ofisini kwetu hivyo tukawa tunapokea posho na mishahara mara mbili kwa mwezi

Kufika kule site kukawa kunahitajika vibarua wengi tu kwa ajili ya mradi, Wazungu katika vikao vyao walikuwa na plan nzuri sana.. Walitaka waajiri vibarua wawalipe kwa siku 50k, wanunue gari ambazo zitakuwa zinawafuata kwenye vituo vya karibu na makazi yao ziwapeleke na kuwarudisha kutoka site na baada ya mradi kuisha hizi gari zilipangwa wapewe serikali, waajiri wapishi ambapo wafanyakazi na hawa vibarua tuwe tunakula for free huko site.

Huwezi amini, Management ya watu weusi ikakaa pembeni na hawa wazungu wakawaambia , Standard ya malipo ni hii (10k) kwa siku mkiwapa nyingi hizo watalewa na hawatafanya kazi kwa ufanisi, wakawashawishi kwamba hao vibarua watakaoajiriwa hadi chakula na usafiri wajitegemee lakini kipindi hichohicho wakashawishi sisi tuliokuwa na ajira rasmi za serikali tuwe tunapata huduma ya chakula na posho na malipo mengine kutoka kwao (nadhani hili walilitetea kwa sababu na wao linawagusa), kweli wazungu wale wakawasikiliza na kufata ushauri wao

Nilikuwa bado mdogo kipindi kile, lakini ilibidi nijiulize inakuaje mtu unakuwa na roho mbaya kiasi kile kwa pesa isiyokuwa yako? hebu fikiria pesa ni za mzungu wala sio za serikali katoka nazo kwao, wao wanaumia kuona ndugu zao weusi wanalipwa vizuri wanamshawishi mzungu awalipe malipo kiduchu huku wao wakilipwa vizuri.

Ni Africa tu aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa.

Adui wa Mwafrika ni Mwafrika mwenzake
 
Huu ndio ukweli wa walio wengi, hilo la kupunguza malipo lipo sana mtu anamshawishi muhisani kupunguza malipo utadhani hiyo pesa itaenda mfukoni mwake! Roho za choyo,roho za kwa nini, roho za wivu, mbaya sana.
kitu cha kuumiza hizo pesa zikibaki hao jamaa wanarudi nazo kwao.
 
Back
Top Bottom