Watu wenye moyo Mpweke...

mbenda said

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
443
1,000
Asalam alaykum,

Nimekuja na mada ya watu wenye moyo mpweke nikimaanisha watu ambao waliiingia katika mahusiano kisha kupitia hayo mahusiano yakawatenda sanaaaaa kiasi cha kutoka na kuamu kuishi maisha ya upweke yaani moyo hautamani tena kuingia ktk mahusiano, unakaribishwa kusimulia kisa chako hapa ili uweze kushauliwa nk ,lakini kusimuli jambo linalokuumiza ,kulia au kuongea kwa kugombeza hupunguza hasira kiasi Karibu sana.

Naleta kisa hiki nilichosimuliwa na rafiki yangu ambacho ndio kilinishawishi niweke Uzi huu,

Hadija aliolewa baada tu ya kumaliza kidato cha nne akiwa bado binti wa miaka 19, baada ya ndoa alikuja dar es saalam ambako mumewe ndik alipokuwa akiishi na kufanya kazi , mumewe Hadija alikuwa amepanga chumba na sebule mitaa ya temeke, baada ya miaka kadhaa walifanikiwa kujenga nyumba yao huko buza, wakati Hadija anaishi ktk nyumba ya kupanga alikuwa na rafiki yake mpendwa alikuwa akiitwa maria.

Hadija na mumewe walivyoamia ktk nyumba yao waliamua mabanda ya uwani wapangishe na ktk kupata watu wa kupanga akaja kupanga na maria na mume wake, maisha yakaenda Hadija akapata mtoto WA kwanza ,akapata mtoto wa pili na wa tatu hali kadhalika pia maria akapata mtoto wa kwanza na baadae wakapata mtoto wa pili ,cku moja mfanyakaz wa ndani wa Hadija akamfuata Hadija na kumwambia ya kwmba mwenyendo wa maria na mumewe Hadija hauwelewi.

Hadija baada ya kuambiwa hivyo itabidi afanye achunguzi ndio akagundua ya kwmba mumewe Hadija anauhudiano wa kimapenzi na maria na mbaya zaid hata wale watoto wa maria amezaa na mumewe Hadija hali ile ilimuuma sana Hadija na ugomvi ukawa mkubwa mpka mumewe na maria akajua kwa kuepusha Shari maria na mumewe Wakahama.

Maisha yakasonga Hadija alikuwa na mdogo wake aliekuwa nasoma kidato cha sita mgodo wa Hadija alikuwa akisomeswa na mumewe Hadija likiz moja baada ya mdogo wa Hadija kufunga shule akaenda kijijini kwao , kitendo kile hakikuwa cha kawaida maaana kila likizo mdog wa Hadija hurudi kwa dada yake anakaa kisha ratiba nyingine zinaendelea ,kupitia lile itbidi Hadija amuulize mdogo wake kwanini ndio mdogo wa Hadija akafunguka kwamba shemeji yake alimbaka likizo ya mwisho kabla ya hii aliorudi kwao ,Hadija kwa hasira akaenda kumuuliza mumewe kilikoni mumewe akajibu pesa yangu ya ada ninayomlipia mdogo wako itarudi vp bila kufanya vile? Kupitia hilo Hadija akafunga virago vyake na kurudi kwao.

Hiyo ni simulizi ya kweli na hata leo ukitaka nakupele kwa huyo Hadija maana aliludi kivyake kupambana kimaisha, lkn tu hayo majina nimetumia sio yenyewe kwa kutunza siri ya wahusika.

Je, ushaumizwa katika mapenzi kiasi hutamani tena kuwa katika mahusiano (moyo wako ni mpweke?) Njoo hapa utusimulue ilikuwa kuwaje?
 

CHIEF WINGIA

JF-Expert Member
Jul 12, 2013
1,040
2,000
Kwanza mshauri huyo Hadija akapambanie haki zake i mean mgawanyo wa mali kisha ndio afanye maisha yake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom