Watu wengi wanakula ila hawalimi.

Watu wengi wanakula ila hawalimi.

kilimo kina gharama sana mkuu yaani utafte mashamba,wafanyakazi,mbegu,mbolea na mwisho wa siku kuna suala la ushuru si unaweza kufa na madeni
Ni kweli mkuu kilimo kina gharama.

Lakini inategemea unataka kulima nini mfano mtu akitaka kulima viazi, maharage, njegere, mahindi, njugu au karoti hayo mazao hapo juu hayahitaji pesa nyingi ili wewe uweze kulima.

Muhimu ni kuwa na Nia plus information sahihi kuhusu mazao unayotaka kuyalima then kila kitu kitawezekana tu.
 
Ogopa sana mtu anae ona, watu nyuma ya Sreen ya laptop wanacheza/Chezea ila yeye na jembe lake ndo anafanya kazi.

Kilimo chenyewe kila siku wana lialia, mara Mvua, mara mbegu, mara bei ya soko, mara wadudu.

Nway, nyie limeni sisi tutakuja kununua, na muache kuwasema sema wateja wenu.
 
Hellow wana JF.

Ukitazama kwa umakini katika hii Dunia ya sasa watu wengi wanakula ila hawalimi. Hata wasomi wengi walio somea kilimo wanataka kukaa maofisini kwenye kiyoyozi na feni zenye upepo mzuri hawataki kabisa kujihusisha na kilimo.

Ukizunguka kwenye mashule na mavyuo mbalimbali ulimwenguni katika wakufunzi milioni moja ni wakufunzi wachache sana watakao kuwa wanawaza kufanya kilimo(katika hiyo milioni moja wanaweza kujitokeza wakufunzi 10 au 20 watakao kuwa wana penda/mpango wa kufanya kilimo 10 au 20 tu) walio bakia wote watakuwa wanawaza kukaa maofisini kuchezea kompyuta na ajira nyingine ila sio kufanya kilimo.

Kila siku asubuhi watu wanahitaji heavy breakfast, kila mchana watu wanahitaji lunch, kila usiku watu wanahitaji dinner and yet hawataki kulima kabisa.

However katika mipango yako ya kila siku jaribu kulitazama hili la kilimo, Aise kilimo chenye tija kamwe hakita kutupa kwani Demand yake ni kubwa mno mno na Demand yake haitakuja kuisha zaidi ya kuongezeka siku mpaka siku.

Kuongezeka kwake ni kwasababu watu wengi wanakula ila hawalimi na hawana mpango wakulima kabisa.
Ni mgawanyiko wa kazi, kuna kukaa ofisini na kulima shambani. Huko ofisini unamsaidia mkulima kuhusu kilimo bora, na udongo unaofaa kisayansi. Mkulima nae anakupa chakula ili uendelee kufanya utafiti.
 
Unfortunately hilo haliwezi kutokea mkuu .

Kila mmoja inatakiwa apambane kwa njia anazo ziweza yeye pamoja na familia yake.
Ndo maana nikisikia kiongozi anataka kupunguza umaskini huwa najiuliza anamlenga nani, amejipangaje mwisho wa siku wanatoa hela vijana wakauze mitumba na sendo za kina dada kariakoo
 
Ni mgawanyiko wa kazi, kuna kukaa ofisini na kulima shambani. Huko ofisini unamsaidia mkulima kuhusu kilimo bora, na udongo unaofaa kisayansi. Mkulima nae anakupa chakula ili uendelee kufanya utafiti.
Hoja ya jamaa ni kwamba ratio ya ofisini vs shambani haiko sawa maana vijana wengi wanakimbilia maofisini sasa mtakuwa wote ma afsa kilimo.?
 
Ogopa sana mtu anae ona, watu nyuma ya Sreen ya laptop wanacheza/Chezea ila yeye na jembe lake ndo anafanya kazi.

Kilimo chenyewe kila siku wana lialia, mara Mvua, mara mbegu, mara bei ya soko, mara wadudu.

Nway, nyie limeni sisi tutakuja kununua, na muache kuwasema sema wateja wenu.
😀 hakuna alipo semwa mtu mkuu ni mtazamo wako tu.

Unaweza ukalima huku ukichezea laptop yako ofisini naona kama haujaelewa mada.
 
Ni mgawanyiko wa kazi, kuna kukaa ofisini na kulima shambani. Huko ofisini unamsaidia mkulima kuhusu kilimo bora, na udongo unaofaa kisayansi. Mkulima nae anakupa chakula ili uendelee kufanya utafiti.
Of course mkuu mada haijasema watu waache kazi zao nyingine ili wakafanye kilimo.

Unaweza kuwa Doctor lakini pia mkulima, unaweza kuwa askari magereza lakini pia ukafanya kilimo.
 
Back
Top Bottom