Watu wengi wanaishi chini ya dola moja kwa siku

Watu wengi wanaishi chini ya dola moja kwa siku

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
24,881
Reaction score
60,912
Maisha yamekuwa magumu pesa imekuwa ngumu na watu wanapata kipato kidogo tu kwa siku. Vijana wengi ni tegemezi akishapata bundle lake la buku la Halotel anatulia nalo siku mbili tatu. Mwingine ni mvuta bangi akishapata buku mbili asi anaridhika msosi wa buku anakwara buku ananunulia mambo yake imeisha.

Mlevi yeye buku mbili analewa vizuri ndo maisha ya mtaani msicheke. Watu wengi wanalalamika hali imekuwa ngumu wanasema ni athari za covid.

Mpaka mahusiano sasa yamekuwa changamoto maana kama haungizi zaidi ya 5000 kwa siku utampata wapi mwanamke. Imefikia wakati mtaani huwezi kupata hela mpaka ucheze rough yaani madeal haramu haramu au la sivyo umtoke mtu. Ni hatari kidogo kwa usalama wa taifa dhiki na umasikini ukizidi hakutakuwa na upendo.

Toeni ajira haraka kunusuru hili genge la vijana ambao wameshachafukwa.Kama kweli miradi yenu mlioijenga ipo basi toeni ajira tuone.

Viwanja vya ndege vilivyojengwa waajiriwe watu wataalamu wa idara husika za pale. Kwanini mmekomaa na walimu na watu wa afya peke yake ina maana sekta nyingine mbona kuna upungufu mkubwa wa watumish na bado watu hawana matumaini sijui mnakwama wapi.
 
Mkuu ata hko unakosema kwenye ualimu kwamba wanapendelewa ni siasa tupu, zinatangazwa nafasi let say mia tano lkn kiuhalisia wanaopata hyo kazi ni ishirini tu au thelathini alafu wakitoka hapo wanaenda kujimwambafai kwenye majukwaa kuwa tumeajiri waalimu mia tano wakat sio kweli.
 
Back
Top Bottom