watu wapenda kusifiwa na waasi wa Fikra za Mwalimu


Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2007
Messages
2,505
Likes
32
Points
135
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2007
2,505 32 135
Kwa takribani wiki mbili nimekuwa nikifuatilia nini kinaendelea katika Bunge letu na chama cha Mapinzduzi kwa Ujumla,Suala la Kusafishwa kwa aliyekuwa Waziri Mkuu,Maarufu kwa jina la Mamvi na wabunge na Baadhi ya viongozi wa chama,na watu ambao wote wamenyang’anywa mawazo yao na kupandikizwa maawazo ya kutamani madaraka limeonekana ni kero kwa watu wengi.Kimsingi inasikitisha sana watu kutetea suala ambalo hata ndodocha anafahamu kuwa ni wizi na ufujaji wa mali katika nchi yetu.


Historia ya nchi yetu inaoneshana Hata MWalimu Nyerere alishawahi kutia shaka Utajiri wa huyu mtu na alimwambia amwambie Pesa alizonazo alizitoa wapi?na mpaka Mwalimu Anakufa hakuwahi kufanya hivyo.Na kama mtakumbuka Mwalimu alipoombwa na Mzee Kawawa aje amsafishe ,Mwalimu aliwajibu Msiwe Wajinga.


Sasa Watu kama kina Serukamba,Mwang'onda na wenzie wanapokuja kumsafisha Mtu amabye alishachafuka siku nyingi ana nia nalengo lipi.Kwa uzoefu nilioa nao,Wale wote walio na ni ana kumsafisha Mavi ni wapenda Kusiwa na wale wanofikiri walizaliwa ili wawe viongozi na hakuna mtu mwingine anaweza kuwa kiongozi zaidi yao.Na hili ndilo lengo lao hasa ya kwamba Mavi lazima awe Rais,Rejea maneno yake..Tatizo ni Uwaziri Mkuu...na lengo lao wanapanga kambi ya 2015.

Mpaka sasa kwa tetesi zinazoenea mitaani ni kwamba wanajipanga na uchaguzi wa 2015 na wengine kama Kina Serukamba,Malima wanataka nasfai za Uwaziri na kwa kuona hivyo wanaona wao kuwa na Mamvi itawasaidia wao kuwa watawal ambo ndiyo lengo lao hawa wapenda kusifiwa.Wanapingana na kambi ambayo haawana shida ya uongozi.

MWalimu Nyerere alisimamia Maadili ya Uongozi ambayo watu wengi leo hasa hawa wapenda kusifiwa wanyaona ni kama upuuzi kwao,wanfikiri kuwa matajiri na kutajirisha ndugu zao huku wakiwacheka watanzania masikini,wanawatusi na kuwatisha watanzania kwa kuwadanganya mambo wanayoyajua.wanatulazimisha tumpende mtu ambaye ni MWalimu alimuona ni Mvunjaji wa Maadili ya Uongozi.

Naomba kutoa Hitimisho kwa hili,Mzee Mwanakijiji alishasema Kama wanataka Kutuzuga basi wajiandie kutuzuga ili tuzugike.ila kwa kutufanya siye Mandondocha huku wao ndiyo mandondocha wa wakubwa wao mwisho iwe leo na kamwe watanzania hawatawapa nafsai tena ya kujaribu kuchezea akili zao hapo 2010.

Na Nawaomba tuanze kampeni ya kuhakisha wabunge hawa ambao wantete ufisadi wang'oka.na naombma kuanza kutoa majina yao hapa hapa na hata kama majioimbo yasipoenda kwa wapinzani basi yaende kwa watu walio tayari kulinda maslahi ya nchi kwanza

1.Peter Serukamba-Kigoma
2.Malima
3.Mbunge wa buchosa
4.Mzindakaya
5.John Komba
6.Chenge
7.Lowassa
8.Karamagi
9.....................Nimethubutu kuwasema na sitathubutu kuwatetea na kama mnaona nimewaonea basi niandikieni gembe@jamiiforums.com au gembe@jamboforums.comImetosha
 
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2007
Messages
2,505
Likes
32
Points
135
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2007
2,505 32 135
Na habari nilizopenyezewa hivi sasa ni kwamba,wana Mpangao wa kumuaanda Masha kama Mamvi akishindwa kusafishika kwa ajili ya 2015.Tusipokuwa makini basi nadhani Tuandako..
 
Sam GM

Sam GM

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Messages
536
Likes
6
Points
35
Sam GM

Sam GM

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2008
536 6 35
Gembe,

Kwa vile unamuongelea mtu anayejulikana si ungekuwa direct forward kusema ni yupi. sioni kama kuna siri hapo. nafikiri Nyerere alisema bila kuficha kuhusu Lowassa na kwa mtazamo wangu ungetumia jina lake halisi kutoa hoja yako.
 
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,134
Likes
73
Points
145
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,134 73 145
Mhh kwa stahili ya kusafishana kwenye NEC mpaka 2010 na 2015 si atakuwa ametakata huyu?
 
Kana-Ka-Nsungu

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2007
Messages
2,260
Likes
81
Points
135
Kana-Ka-Nsungu

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2007
2,260 81 135
Mamvi kwa jinsi alivyochafuka hata wakimloweka kwa 'jiki' kuanzia sasa hadi hiyo 2015 bado atakuwa mchafu tu!
 
Pundit

Pundit

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2007
Messages
3,741
Likes
40
Points
145
Pundit

Pundit

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2007
3,741 40 145
watu wapenda kusifiwa na waasi wa Fikra za Mwalimu
Heading haijatulia, iko ambiguous.

Inaweza kumaanisha unawachambua watu walioasi fikra za mwalimu ambao wanapenda kusifiwa ,

Lakini pia inaweza kumaanisha watu wanaopenda sifa kutoka kwa waasi wa fikra za Mwalimu.

Vilevile inaweza kutafsiriwa kumaanisha kwamba unaweka mafungu mawili, moja la watu wanaopenda kusifiwa na lingine la waasi wa fikra za Mwalimu.

Tuhurumie!
 

Forum statistics

Threads 1,238,299
Members 475,878
Posts 29,315,235