Watu Wanaopinga Maendeleo ya Magufuli

Na hili ndio tatizo kubwa sana. Kimsingi naamini uthamani wa watumishi umeondoshwa. Malalamiko ni MENGI sana ktk hili japo wahusika wapo kimya. Hakuna anayependezwa na kukaa miaka mingi bila ya kupandishwa madaraja. Hali si njema kwa kweli. Alionao Karibu hawamuelezi hili kiufasaha. Kina watumishi wamestaafu/wamekufa bila kupata stahili ZAO. Wanasononeka huko makwao na familia ZAO. Usishangae Baraka zikapungua pia
 
Gombea urais basi tujue moja.
 
Kichwa chako cha habari kinaonyesha watu wanapinga maendeleo ya Magufuli, mimi nimekuonyesha watu hawapigi maendeleo bali wanapinga tabia ya mleta maendeleo. Maendeleo yanaweza kuletwa na yoyote kwani ni kodi za wananchi na sio mshahara wa rais.
Ndiyo maana nimeomba mtupe mbadala, mngekuwa nyinyi mngefanya nini?
 
Ndiyo maana nimeomba mtupe mbadala, mngekuwa nyinyi mngefanya nini?

Zaidi ya hivi vinavyofanywa na kuheshimu demokrasia juu. Elimu ingekuwa bure mpaka chuo kikuu, tungeshusha bei ya vifaa vya ujenzi, tusingenunua ndege bali tungewekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji,wangalau miradi mitano mikubwa ya 150b@. Tungeruhusu wakulima wauze mazao yao popote watakapo, baada ya ghala la taifa kununua akiba ya kutosha tena yenye faida kwa mkulima. Tungeongeza ajira hasa kwa vijana. Tungeshusha viwango vya kodi ili kupanua wigo wa makusanyo.
 
Zaidi ya hivi vinavyofanywa na kuheshimu demokrasia juu.
Unawezaje kupata nafasi ya kumponda Magu hapa JF kama siyo demokrasia?
Elimu ingekuwa bure mpaka chuo kikuu,
Elimu ya chuo kikuu siyo lazima ndiyo maana serikali inachofanya ni kutoa mikopo. Kwa elimu ya awali na sekondari hiyo ni haki ya kila mwananchi na serikali inafanikisha hivyo kwa kuitoa bure.
tungeshusha bei ya vifaa vya ujenzi,
Tueleze tafadhali jinsi gani ya kufanya hivyo.
tusingenunua ndege bali tungewekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji,wangalau miradi mitano mikubwa ya 150b@.
Hivi ni nchi gani kubwa isiyo na shirika lake la ndege ukiacha Marekani?

Wizara ya maji imefanikisha kuvuta maji kutoka ziwa victoria mpaka Tabora na sasa wanayapeleka mpaka Dodoma. Mradi huo baadae unaweza kuboreshwa kutumika kwenye umwagiliaji.

Tungeruhusu wakulima wauze mazao yao popote watakapo, baada ya ghala la taifa kununua akiba ya kutosha tena yenye faida kwa mkulima.
Unaelewa dhana ya food security? Utawezaje kuuza chakula chako kwa jirani wakati watoto wako hawana?

Serikali inachotakiwa ni kuongeza bei ili wakulima wafaidike zaidi na kupata mtaji ili waongeze uzalishaji. Chakula ziada kinaweza ruhusiwa kuuzwa nje moja kwa moja na wakulima, hii itawapa motisha kuzalisha zaidi.
Tungeongeza ajira hasa kwa vijana.
Tupe njia ya kufanikisha hivyo tafadhali.
Tungeshusha viwango vya kodi ili kupanua wigo wa makusanyo.
Hilo nakubaliana nanwewe 100%
 

Ni hivi, hivyo nilivyokutajia vyote vinatekelezeka maana ni suala la mipango tu. Ndio maana tunasisitiza acheni wizi wa kura kisha kila mtu apate kura za halali halafu uone utekelezaji. Only five years youth will see the results. Kumponda Magufuli namponda bali simtukani, na nimeweza hilo maana natumia fake ID. Ila hilo hilo haliwezekani kwenye sehemu za wazi kwani usalama huko ni mdogo.
 
kama hakuna reli na barabara mazao na huduma za jamii zitawafikiaje walengwa?

Kama Walengwa hali zao zime Dorora kiuchumi watazinunua na nini ?.Mwisho Wakulima wanapata Hasara na Mazao yana oza kwa sababu ya kukosa wanunuzi.
 
Ni kweli kabisa...

Tatizo binadamu was siku hizi ni wabishi sana..

Wao wanaona muhimu kwanza ni kupandishwa madaraja na kuongezewa mishahara... Kupata stahiki zao mapema pale wanapostafu, kuacha kazi au kuachishwa kazi... kupata ajira zitakazowawezesha kujikimu...


Cc: mahondaw
 
Miundombinu ndio solution kubwa ya tatizo la ajira na umaskini... umaskini wetu unatokana na kukosa miundombinu...
Asilimia 80 tulime bila barabara hatuna pa kuuza na ndio maana almost 60yrs tuko palepale
Umeme utatuwezesha kuanzisha viwanda vidogovidogo hadi vijijini
Anafanya opportunity cost... katika list ya mahitaji ameanza na tatizo kubwa ili matatizo madogo yatajitatua yenyewe.....
Wote tunalia leo hali ni ngumu ila anachokifanya ni majibu ya hizo shida zote
 
Kama Walengwa hali zao zime Dorora kiuchumi watazinunua na nini ?.Mwisho Wakulima wanapata Hasara na Mazao yana oza kwa sababu ya kukosa wanunuzi.
Kuna kitu kinaitwa building blocks, ufanisi wa miundombinu kama barabara na reli hushusha gharama za usafirishaji. Na hivyo kupunguza gharama za bidhaa.

Ni hivi, hivyo nilivyokutajia vyote vinatekelezeka maana ni suala la mipango tu.
Bro, we have some tangibles already, this administration has delivered most of what was promised. What'd be your plan if you'd the same opportunity?
Kumponda Magufuli namponda bali simtukani, na nimeweza hilo maana natumia fake ID. Ila hilo hilo haliwezekani kwenye sehemu za wazi kwani usalama huko ni mdogo.
Niamini ndugu yangu, hizi ID si kitu, watu wakikuamulia wanaweza kukufahamu wewe ni nani. Nchi zisizo na demokrasia haziwezi ruhusu hata kuwa na tovuti kama hii.
 
CCM wanaiba kura..umeona leo mahakama kuu wanavyotoa mapovu kuhusu wakurugenzi...
 
Ndiyo maana nimeomba mtupe mbadala, mngekuwa nyinyi mngefanya nini?
Chamoto hapa utabishana na wadau mpaka kuna kucha,ni sawa saws na mchezo wa mpira wa miguu mashabiki wanajifanya wanajua mpira kuliko wachezaji na pale timu inapofungwa wanabaki kumlaumu Kocha.
cc.@Taifa Star Africon
 
Eti umesema uchguzi? hahahah chini ya polis ccm wizwiz wa wazi wazi halafu unaongea uupuz gani? barabara zilikuwepo anaongeza,,, hao madege yana run kwa loss na yatakufa bila kuingiza chochote,,,, maisha ya wananchi yamekua duni than ever, sio watuimishi, wala wakulima wote hali ni mbaya,,,bomu la ajira umeliweka wapi?
 
Hulka ya ubinaadam ni upinzani. Baadhi ya binaadam hupingana hata na muumba wao seuse binaadam mwenzao.

Tukitazama kwa kina suala la kupingana haliishii kwa binaadam pekee, si hasha hata wanyama hupingana na "the fittest of the fittest shall survive".

Umewahi kukisoma kisa cha " The Animal Farm" cha George Orwell? Kama hujakisoma, kitafute.


Tanzania tulifanya kupingana kuwe rasmi tulipoamua kuwa na mfumo wa vyama vingi vya "upinzani". Umeshajiuliza kwanini watawala wetu wa wakati huo, licha ya maoni ya Watanzania walio wengi walishauri iwe nchi ya chama kimoja tu, waliamua wafate wachache waliotaka vyama vingi?

Kupingana Tanzania ni halali na upinzani si lazima uwe wa kutoka kwa vyama pinzani. Hata ndani ya chama kupingana kuheshimiwe.

Unayoyaona wewe maendeleo wengine wanaona ni msiba. Usidharau maoni yao, wasikilize pengine wana sababu nzuri tu. Tupingane kwa kubadilishana mawazo na hoja ili hoja na wazo bora litekelezwe.

Sioni tatizo kwa watu kupinga miradi kwani si kila mradi ni maendeleo na si kila maendeleo ni mradi.
 
Unazungumzia maendeleo haya ya awamu ya 5 ama yepi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…