Watu wamiminika kwa wingi kwenda kupata utajiri wa haraka Meatu - Simiyu

Wakuu salamu.

Idadi kubwa ya watu wanamiminika kwenda Wilaya ya Meatu Kata ya Mwandoya kwa bibi kupata Ndagu ya utajiri.

Watu kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini, wakiwemo wafanya biashara, wafanyakazi, wakulima na wafugaji wamefika kwa bibi huyo kupewa dawa ya utajiri.

Wafanyabiashara wakubwa wa maduka ya jumla katika Miji ya Arusha, Mwanza, Musoma, Bariadi, Shinyanga, kahama, Nzega na Igunga wamefika kwa bibi huyo.

Waliofanikiwa wanarudi na magari, mabati na pesa za shukrani kumshukuru bibi huyo.

Hivi huwezi kupata utajiri mpaka utumie ushirikina?

Ccm imeshikwa kubaya kila siku swaga mpya
 
Weka picha maneno matupu hayavunji mfupa,tuone wamebeba mabati na huyo bibi pia,acha kuleta hisia hapa na uvumi wa mtaa fulani.asante najua utaleta nilivyo kuomba, we mleta mada
 
mleta mada tupe masharti ya hizo dawa za kuleta utajiri, tuanze kuangalia kwa namna moja au nyingine
 
Mimi kwenye huu uzi nimekumbuka enzi flani nilitembelea sana maeneo hayo..... Sakasaka, Mwandoya, Igobe, ikungu lyankoma, zebeya........
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa " Mungu "

Hakuna nchi duniani iliyoendelea kwa Ndumba au mambo ya Babu wa Loliondo

..... vipi Tanzania?
..... sijui hadi jioni hii wamekusanya damu mapipa mangapi na lengo lao ni kukusanya mapipa ngapi?
...... kilio cha ndugu zetu albino ni kikubwa
.
 
jamaa anatangaza biashara huyo bibi ni picha tu.vijana ugumu wa maisha utatupeleka pabaya huu uzi wa kutoa promo tu
 
Wakuu salamu.

Idadi kubwa ya watu wanamiminika kwenda Wilaya ya Meatu Kata ya Mwandoya kwa bibi kupata Ndagu ya utajiri.

Watu kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini, wakiwemo wafanya biashara, wafanyakazi, wakulima na wafugaji wamefika kwa bibi huyo kupewa dawa ya utajiri.

Wafanyabiashara wakubwa wa maduka ya jumla katika Miji ya Arusha, Mwanza, Musoma, Bariadi, Shinyanga, kahama, Nzega na Igunga wamefika kwa bibi huyo.

Waliofanikiwa wanarudi na magari, mabati na pesa za shukrani kumshukuru bibi huyo.

Hivi huwezi kupata utajiri mpaka utumie ushirikina?

All these are signs of a very backward nation.
 
Kuchanjiwa chale kwenye zizi la ng'ombe Tsh 150000 Kuchanjiwa mlangoni mwa nyumba 50000 Unakaa ndani masaa 24 bila kutoka ndani, ukitoka hapo mambo yako Super.
 
Ulinzi Shirikishi Nendeni Mkasake Viungo Vya Albino Kwahuyo Kigagula Wa Mwandoya!
 
Mimi kwenye huu uzi nimekumbuka enzi flani nilitembelea sana maeneo hayo..... Sakasaka, Mwandoya, Igobe, ikungu lyankoma, zebeya........
mimi umenikumbusha miaka Mingi iliopita kuanzia unapopanda basi la Mwanhuzi, ukipitia Mhunze,mwakidiga,Lalago,Gula,Sangamwalugesha,Sanga Itinje,mwanindo,Minyanda,Mbalagane,Lubiga,Iponanabholo-Mwandoya,Igobe,Mwakisandu,Tindabuligi,Sakasasaka mpaka Butuli. Duuu haya mambo.....
 
Nlkuwa bize kuangalia kama wa MOSHI kaenda...... Kumbe hawajaenda...... Hiyo ni feki
 
Back
Top Bottom